Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Akikujibu hivi kitabu chake kitakosa soko.Yeye keshajipa kazi ya Kumlaumu Nyerere.Hayo ya kuwakomboa.waislamu hayamhusu
 
Tupatie suluhisho kwa matatizo ya waislam na si kurudika biography.
 
Ila mzee wangu unanifurahishaga sana.Bakwata si waislam?
Nan...
Sijasema kuwa BAKWATA si Waislam.
Ninachosema na kuna research paper nimeandika, "Islam and Politics in Tanzania," (1989) nimeeleza kuwa serikali iliivunja EAMWS kuzuia wasijenge Chuo Kikuu.

Kuanzia hapo serikali haitambui jumuia yoyote ya Waislam na kuna kundi kubwa la Waislam limejiweka mbali na BAKWATA.
 
Mrangi,
Shida iko katika kuzuia Waislam kujenga Chuo Kikuu.
Kwani mmezuiwa kujenga chuo kikuu mpaka sasa? Hii generation mpya ya waislam post independence wanafanya nini kuhusu maendeleo ya waislamu kijamii na kiuchumi? Mkijenga chuo kikuu kiendeshwe kwa misingi ya kidini hakiwezi kukua (MUM), watanzania wana dini ila nchi ni secular. Hata taasisi za kidini za wakristo zimejikita zaidi kwenye kutoa huduma za kijamii zaidi kuliko kukomaa na misimamo ya kidini .
 
Bila control ya taasisi za kiislam tungekuwa na Alshabab Tanzania,serikalia kuwafosi kuwa na taasisi moja inyitambulika rasmi sio mbaya . There is a very thin line between Islamic extremism and liberal islam tuliyonayo Tanzania.
 
Tupatie suluhisho kwa matatizo ya waislam na si kurudika biography.
Nan...
Hizi ghadabu za nini?

Nimekuwekea hayo kukuaminisha kuwa nimetafiti haya niandikayo hapa.
Mimi nikupatie wewe suluhisho ya matatizo ya Waislam?

Halafu iwe nini?

Waislam wana taasisi zao nje ya BAKWATA ndiyo hizi unaona leo tuna radio, TV Stations, magazeti tunajenga shule nk. nk.

Ndiyo leo unaona ndani ya Bunge tunauliza haya:

''Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''

Waziri wa Elimu hakuwa na jibu.

Serikali inatambua kuwa hii ni fitna kubwa na inagawa wananchi katika makundi mawili makubwa kwa imani zao.

Serikali inayajua haya na imekuwa kimya kwa hofu.

Ndugu yangu jiweke wewe kwenye hali hii ya Waislam kama ilivyoelezwa hapo juu ndiyo utaelewa tatizo hili.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)​



Mwandishi akimhoji Kitwana Kondo kipindi cha TV nyumbani kwake Upanga 2012​
 
Kutafuta solution ndio msingi na si kulalamika
Nan,
Wala silalamiki.
Mimi naandika historia nina vitabu kadhaa na nina makala inakisiwa 10,000.

Kuna mchapaji vitabu anatafiti niliyoandika anataka kuchapa kitabiu ndiye aliyeniambia kuwa ziko makala zinakaribia 10,000.

Mimi hapa nasomesha kuwafahamisha wasiojua yale yaliyoko na yaliyopita.

Naamini wewe umejifunza mengi kutoka kwangu.
 
Waislamu wa karne hii wanataka haki ya kula kitimoto na kusuka rasta ndefu na kuonyesha umbo la makalio, vyuo vya kiislam vitapata wanafunzi wachache sana kama chaguo la mwisho. Hata huko Iran wadada wanataka haki ya kuonekana nywele zao.
 
Kwanini tusiifahamu wakati babu zetu wengine wapo wakati nchi kabla hadi nchi inapata uhuru

Ova
 
Huko Uganda na kenya EAMWS bado ipo?
 
Huko Uganda na kenya EAMWS bado ipo?
Nan...
Mgogoro ulipokuwa umeshamiri Aga Khan akajiuzulu kama Patron.

Mufti wa Tanganyika akakamatwa na kufukuzwa nchini.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS.
EAMWS ilikuwa na matawi mengi na wafuasi wengi Tanzania.

Kenya na Uganda haikuweza kuendesha EAMWS peke yao ikafa.
 
Huko Kenya na Uganda mbona miundombinu ya taasisi za Kiislam siyo nyingi kama ilivyo Bakwata?
 
Unapewa darsa za historia uijuwe nchi yako ilipotokea ili uamuwe unaelekea wapi una sema analia lia.

Ni kipi alicholia hapo? Unashindwa kujibu hoja zake unamvaa yeye binafsi?
 
Huko Kenya na Uganda mbona miundombinu ya taasisi za Kiislam siyo nyingi kama ilivyo Bakwata?
Unaweza kututajia hiyo 'miundombinu" ya Waislam wa Kenya, Uganda na Tanzania? Wengine hatuifahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…