Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Nga...
Nyerere analaumiwa kwa kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA ili Waislam wasiwe na Chuo Kikuu kwani wakati ule EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu.

Akamkamata Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na kumfukuza Tanganyika asirejee tena.
Unaweza ukataja ambacho unaweza ukamsifia nacho..!!?? Kwa maneno mengine, unaweza ukayataja mazuri ya Nyerere..!!?? AU hana mazuri?
 
ndo maana ulipokuwa UDSM Prof. Msabaha Mzaramo mwenzako alikupa maksi ulizostahili ukaanza kumshambulia ati anaringa! Kumbe kakupa maksi kutokana na upeo wako na si chuki ulizokuwa unaendesha dhidi ya Ma-professor wa kanda ya Kaskazini!
 
Mwaka 1929 kweli hao wazee waliunda African Association, lakini ilikuwa ni kama kijiwe cha kucheza bao la kete na karata na dhumna. Mpaka alipokuja kafliri JKNyerere na kuwafungua macho
 
Nga...
Nyerere analaumiwa kwa kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA ili Waislam wasiwe na Chuo Kikuu kwani wakati ule EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu.

Akamkamata Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na kumfukuza Tanganyika asirejee tena.
Mkuu Nyerere aliondoka madarakani lini? Nyerere alifariki lini? Mbona hadi leo hamna hicho chuo? Mmeshindwa nini kukijenga kama Nyerere alikuwa kikwazo
 
Kinj...
Hakuna tatizo ndugu yangu.
Ukiwa unaona unajua basi.

Mimi niko hapa tunakijadili kitabu cha Abdul Sykes toka 2008.
 
Mkuu Nyerere aliondoka madarakani lini? Nyerere alifariki lini? Mbona hadi leo hamna hicho chuo? Mmeshindwa nini kukijenga kama Nyerere alikuwa kikwazo
Kinyungu,
Katika miaka ya 1970 OIC walitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Serikali ya Tanzania ilikataa kutoa kibali.

Chuo kikapelekwa kujengwa Mbale, Uganda.
 
Kwa hiyo hili ni jibu la swaoi langu!
 
Mwaka 1929 kweli hao wazee waliunda African Association, lakini ilikuwa ni kama kijiwe cha kucheza bao la kete na karata na dhumna. Mpaka alipokuja kafliri JKNyerere na kuwafungua macho
Stux...
Baada ya kuunda African Association wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)mwaka wa 1933.

Vyama hivi viwili vilishurikiana katika kupambana na madhila yote ya ukoloni.

Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilijenga Muslim School ambayo ndiyo shule waliyosoma wazee wetu waliokuja kuwa viongozi wa TAA na wanachama wa mwanzo wa TANU.

Mweka Hazina wa kwanza wa TANU Iddi Faiz Mafungo alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya.

Huyu ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO.

Kadi yake ya TANU ni No. 24 na ya ndugu yake Iddi Tosiri ni No. 25 na ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya ambae yeye ni binamu yao.

Usiandike kihuni kutumia maneno "kafiri," na mfano wa haya.

Unalifuja darasa.

Jichukulie uko darasani mwalimu anafundisha.

Historia hii nimesomesha vijana wenzako wengi na wengine sasa ni walimu vyuo vikuu.
 
ndo maana ulipokuwa UDSM Prof. Msabaha Mzaramo mwenzako alikupa maksi ulizostahili ukaanza kumshambulia ati anaringa! Kumbe kakupa maksi kutokana na upeo wako na si chuki ulizokuwa unaendesha dhidi ya Ma-professor wa kanda ya Kaskazini!
Geza...
Hili ndilo kwanza nalisikia.
Mimi si Mzaramo mimi Mmanyema.

Wala sijapata kumchukia mtu katika maisha yangu.

Sikuumbwa hivyo.
Alhamdulilah.

Huna la kusema kuhusu waraka niliokuwekea la ubaguzi?

Unadhani ningekosa radhi ya waalimu wangu pale chuoni ningeweza kufanya haya ya kuandika vitabu, research papers na kuzungumza katika Vyuo Vikuu Afrika, Ulaya na Marekani?

Au hujui kuwa kitabu cha Abdul Sykes mtu wa kwanza kukipitia alikuwa mwalimu wangu wa historia Prof. Fredrick Kaijage?

Hii ni dalili ya mwanafunzi dhaifu aliyekuwa akipewa alama za chini na walimu wake?

Mimi nina radhi ya waalimu wangu wote walionisomesha kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Dar-es-Salaam na Cardiff.

Nina radhi ya wazazi wangu.

Huwezi kunivunjia heshima yangu kwa maneno ya kipuuzi.


Kulia: Dr. Ibrahim Msabaha, Prof. Emmanuel Bavu na Mohamed Said

Kulia: Paul Sozigwa, Mohamed Said na Prof. Bavu Prof. Bavu alinitembelea nyumbani kwangu
 
Mohamad said najifunza mengi kwako likiwemo la uungwana na ustahimilivu. Lakini napata shida na hoja zako.

1. kila kitu kwako ni black and white. Kwako hii nchi ni ya wa Islam na wakristo. Ukweli ni kwamba zipo Imani nyingine pia ambazo zinawaumini Watanzania. Ambazo kwako siyo Muhimu.
2. katika hoja zako, hakuna mazuri ya Nyerere/Serikali kwa waislam.
3. waislam ndo wamenyanyasika kuliko raia wengine. Ukweli ni kwamba kwa miaka mingi sana, Elimu imekuwa changamoto kubwa sana hapa Tanzania, na wote tumekuwa wahanga wa hili. Mfano kwa miaka mingi, chuo kikuu kilikuwa UDSM. kuna Wilaya walikuwa wanafaulu/ wanachaguliwa wanafunzi si Zaidi ya 20 kwenda form one! Na kwa sababu hizi wilaya hazikuwa na shule za secondary walitegemea hisani ya wilaya nyingine. Hiki nacho ni kipengele, maana wengi walikosa fursa.
4. ndo maana humu wengi wanakushambulia kwa sababu mengi unayoyaongea, kiukweli uhalisia ni mdogo, maana sulba na changamoto za elimu tumezipitia wengi humu.
Personally, nilifaulu nikakosa shule. Nikaenda seminar. sijawahi Kulaumu popote.
5. wewe unaamini ndo mwenye uelewa wa historia kuliko wengine. Hapana, jitahidi kuwa accommodative na kujua kwamba you ain’t infallible. Wengi wanajua mengi usiyoyajua. Na si sahihi kutuaminisha kwamba uhuru wa tanganyika ulipiganiwa na waislam pekee.
6. kuna mdau hapo juu amekuuliza, ni changamoto Zipi za kielimu zinampata mtoto wa kisalmu,kwa sasa? Hukujibu. Ukweli ni kwamba changamoto za elimu ni za kitaifa. We are all suffering, from poor decisions by our politicians. Kwako hili hulioni.
7. mwisho St. Augustine University na MUM, sijui kipi kilianza, lakini tukilinganisha ubunifu na uwekezaji, majibu unayo.
8. Bado Naamini kuna waislam smart na wamefanya mambo makubwa nchi hii. Lakini, tunakwama na tutakwama tukitaka kuchanganya dini na maisha ya raia wetu ya kila siku.
9. Swali la kizushi kwako, unaamini Necta ikiongozwa na waislamu, fursa za waislamu kielimu zitabadilika?
 
Ndugu mwandishi tatizo la udini kwenye kazi yako ya sanaa ndio inafanya kazi zako zisifike mbali, nimekuwa nikikusoma sana, hebu sema ni lini wizara ya elimu inapofanya selection za watoto wanatumia kigezo cha dini? Ninavyojua kigezo cha ufaulu ndicho kinacho zingatiwa, sasa mtoto atafaulu vp kwenye hizo shule za kiislam zinazo kumbatia elimu ahela zaidi? Atafaulu vipi kwa kukaa na kobasi wenziwe na kukosa ushindani? Maana nani asie jua shule za kiislamu zimekumbatia ubaguzi wa dhahiri kwa kusomesha walio waislamu tu, tena uislamu upo zaidi kwenye jamii zilizo duni kielimu kama pwani. Tatu nani akasome chuo cha kiislamu moro chenye kila aina ya kukosa uhuru wa mtangamano na kuacha chuo kama st francis nk ambavyo watoto wanakuwa huru ku changamana na kushindana? Haya yote sidhani kama kwa usomi wako huyajui, shida ni ile elimu nyingine ya kimapokeo ambayo ina kinzana na mitizamo ya ki karne ya 21
 
Sasa naanza kuelewa kwanini sasa hivi necta inaongozwa na mzanzibari, nafikir aliwekwa kwa minajiri ya kupunguza hayo lakini sidhani kama itabadili kitu, elimu yetu ina changamoto zake za kiasili
 
Hivi hili la mfumo wa namba kwenye mitihani lilianza wakati gani? Nakumbuka Kaka yangu alitumia mfumo huu Mwaka 1982 ila hapa Mzee Said anasema uliasisiwa na Kighoma Malima!
 
Mzee wangu Mohamed Said

Mimi nimesoma shule ambazo asilimia kubwa ya wanafunzi walikuwa waislamu, na mpaka leo rafiki zangu wengi sana tu ni waislamu. Hili tatizo la "Waislamu kufelwishwa" linatokea kwenye Islamic Schools peke yake au kote?

Shule zote nlizosoma, waislam waliofaulu tuliendelea nao kwenye hatua zinazofuata, na waliofeli, Wakristo kwa waislamu walibaki.

Wanaohujumiwa ni "Students wa Islamic Schools" au "Islamic Students" wote?
 
Masanja,
Mimi nimesahihisha historia iliokuwapl toka uhuru iliyowafuta wazee wangu katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ikambakiza Julius Nyerere peke yake.

Hizo imani nyingine ni zipi na zilikuwako katika kuunda African Association, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa)na TANU?

Unaniuliza kuhusu mazuri ya Nyerere kwani nimeandika ubaya gani dhidi yake?

Nifahamishe.

Waislam na Ubaguzi wa Elimu nimekuwekea hapo una waraka kama huu kutoka kwengine kutaka maelezo kutoka serikalini?

Changamoto za Waislam ni NECTA na yalifanyika maandamano mwak wa 2012.

Unataka kufananisha MUM na vyuo vya makanisa vinavyopokea fedha za Memorandum of Understanding?
 
Mtama,
Soma hapa kuna waraka kuhusu ubaguzi Wizara ya Elimu.
 
Hivi hili la mfumo wa namba kwenye mitihani lilianza wakati gani? Nakumbuka Kaka yangu alitumia mfumo huu Mwaka 1982 ila hapa Mzee Said anasema uliasisiwa na Kighoma Malima!
Ni mfumo wa zamani sana tangu wakati wa Uhuru; Malima alikuwa anajua ku-sensionalize wafuasi wake sana hasa kwa vile alikuwa Profesa. ALikuwa waziri wa Elimu wakati mimi namaliza Chuo kikuu na miaka yote huko nilikopitia kuanzia Mock ya std7, STD7 kwenda Secondari, Mock ya Form 4, Form 4 na Form 6 tulikuwa tunatumia namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…