MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Mkuu... kuna theory na uhalisia.Mtama,
Soma hapa kuna waraka kuhusu ubaguzi Wizara ya Elimu.
Kichuguu,Ni mfumo wa zamani sana tangu wakati wa Uhuru; Malima alikuwa anajua ku-sensionalize wafuasi wake sana hasa kwa vile alikuwa Profesa. ALikuwa waziri wa Elimu wakati mimi namaliza Chuo kikuu na miaka yote huko nilikopitia kuanzia Mock ya std7, STD7 kwenda Secondari, Mock ya Form 4, Form 4 na Form 6 tulikuwa tunatumia namba.
Yaani unaokoteza Historia ya miaka 50 unajibu maswali ya Sasa! Najiuliza Leo hii Kuna mtoto au kijana wa Kiislam anakosa Elimu kwa vikeazo ya kimfumo?! Mbona wamejaa kwenye Shule na Vyuo vya Kanisa! Acha kuwatia upofu Waislam wachache ambao bado wamelala! Inawezekana changamoto zilkuwepo huko nyuma lakini Sasa watu wameamka wanasoma bila hofu...Nina Imani hata wewe ukiambiwa uchague Kati ya St Augustine ,Tumaini au St.Joseph University dhidi ya Muslm University pale Msamvu utachagua chaguo la kwanza!Maku...
Hukulipenda jibu hilo?
Huna ulichojifunza?
Hawaishi lalamika hata matokeo ya CSEE 2012 waliandamana kuwa wanaonewaMsikiti tu wa mtambani pale kinondoni,lilikuwa eneo la posta
Ben mkapa huyo huyo aliwaachia
Mjenge pale
Hebu tupunguze kulalamika
Ova
hii takataka imekosa hoja inajibu swali kwa hotuba ya maamuma sheikh pondaMtama,
Soma hapa kuna waraka kuhusu ubaguzi Wizara ya Elimu.
Mtama,Mkuu... kuna theory na uhalisia.
Huu waraka unaousema, umeandikwa na nani?
Mimi nakisema nilichoishi kwenye elimu ya Tanzania, sijawahi kuona muislam aliyekuwa anafanya vizuri shule, akafeli mtihani wa taifa; ever. Ndio maana nauliza tatizo ni shule za kiislamu au wanafunzi wa kiislamu?
Nimesoma Dar na Pwani maisha yangu yote tena shule za serikali, hakukuwa na maajabu kwenye mtihani wa taifa, top 10 ya darasani ndio ilikuwa top 10 kwenye NECTA.
Yaani unaokoteza Historia ya miaka 50 unajibu maswali ya Sasa! Najiuliza Leo hii Kuna mtoto au kijana wa Kiislam anakosa Elimu kwa vikeazo ya kimfumo?! Mbona wamejaa kwenye Shule na Vyuo vya Kanisa! Acha kuwatia upofu Waislam wachache ambao bado wamelala! Inawezekana changamoto zilkuwepo huko nyuma lakini Sasa watu wameamka wanasoma bila hofu...Nina Imani hata wewe ukiambiwa uchague Kati ya St Augustine ,Tumaini au St.Joseph University dhidi ya Muslm University pale Msamvu utachagua chaguo la kwanza!
Nga....hii takataka imekosa hoja inajibu swali kwa hotuba ya maamuma sheikh ponda
Umeghadhibika.hii takataka imekosa hoja inajibu swali kwa hotuba ya maamuma sheikh ponda
Kwa heshima sana...Mtama,
Nadhani unayafahamu yaliyotokea NECTA hadi kusababisha maandamano.
Mtama,Kwa heshima sana...
Najaribu kuelewa, conspiracy iko wapi hasa? Naomba uchukulie kama swali la mtu anayetafuta kufahamu, siyo kubishana. Am trying to understand; maana nimeishi na kusoma shule zenye waislamu wengi tu, mtihani wa darasa la IV, VII, form II, form IV na form VI; sikuona muislamu anayefanya vizuri darasani akifeli... ndio maana najaribu kuuliza, hili jambo linatokea wapi?
Mtama,
Waislam wamefikisha tatizo hili serikalini ili wapate majibu rasmi ya serikali.
Conspiracy iko wapi?
Hakuna majibu mpaka leo.
Hadithi nyiiingi haya sasa mkurugenzi wa Necta sasa ni muislamu ,acheni visingizio nyanyueni watoto wenu kielimu we hujiulizi kwanini mikoa yenye waislamu wengi ndio yenye dropout kubwa ya wanafunzi je ni hujuma pia?,waislamu mna taasisi gani imara za kielimu? hakuna ,elimu sio lelemamaTuanze hapa tulipo hivi sasa kisha nitaweka tulipotokea baada ya uhuru:
TUJIKUMBUSHE
Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.
Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.
Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.
Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.
Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.
Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?
Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.
Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.
Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.
Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.
Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.
Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.
Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.
Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.
Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.
Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.
Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.
Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.
Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.
Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.
Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.
Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.
Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.
Na hii ni kwa masomo yote.
Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.
Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.
Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.
Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:
1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.
Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.
3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.
Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.
Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.
Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.
Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.
Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.
Tunaomba kuwasilisha,
Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Sasa turudi nyuma wakati tumepata uhuru:
Ipyax,
Yametokea.
Serikali haiko tayari kutoa majibu.
Nina mengi naweza kukueleza muhimu ni wewe uwe tayari kusikiliza.
Marais Waislam hawakuchaguliwa kuchunguza watendaji Wakristo ndani ya serikali wana mchango gani katika matatizo haya yanayoelezwa na Waislam.
Endapo Rais Muislam ataingia madarakani na kuanza kuchunguza tatizo hili atakuwa anatengeneza tatizo kubwa zaidi linaloweza kuigawa nchi zaidi.
Hili la Waislam kuwekeza katika elimu hapa si mahali pake ila ningependa kukufahamisha kuwa baada ya kupatikana uhuru mwaka wa 1961 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alijiuzulu siasa na kuanzisha taasisi yake, "Daawat Islamiyya," yeye akiwa Mwenyekiti na Katibu wake Schneider Abdillah Plantan.
Sheikh Hassan bin Ameir akasema sababu ya yeye kujiuzulu siasa ni kuwaongoza Waislam katika kutafuta elimu kama alivyowaongoza katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
(Naamini inawezekana historia hii ninayokueleza ikakupa tabu kwani hujapata kuisoma popote kuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mwanachama wa TANU na kapigania uhuru.
Schneider Plantan yeye ndiye aliyesimama mwaka wa 1950 kuutoa uongozi wa wazee katika TAA Rais ambae ni kaka yake, Thomas Plantan na Katibu Clement Mohamed Mtamila na kuingiza uongozi wa vijana Dr. Vedasto Kyaruzi kama President na Abdul Sykes Katibu).
Mwaka wa 1962 Sheikh Hassan bin Ameir akishirikiana na EAMWS wakaitisha Muslim Congress agenda kuu ikiwa elimu.
Hii Muislam Congress ndiyo iliyoweka mpango wa kujenga shule Tanganyika nzima na Chuo Kikuu na kazi ilianza mara moja.
Mwaka wa 1968 Rais Julius Nyerere akaweka jiwe la msingi kujenga Chuo Kikuu.
Miezi miezi michache baadae Rais Nyerere akaivunja EAMWS na kuunda BAKWATA.
Uwekezaji wa Waislam katika elimu na ujenzi wa Chuo Kikuu na shule ukakoma hapo.
Historia hii ni ndefu lakini naamini nimekujibu swali lako na umeelewa matatizo yanayowakabili Waislam.
Himars,Hawaishi lalamika hata matokeo ya CSEE 2012 waliandamana kuwa wanaonewa
Rava...Hadithi nyiiingi haya sasa mkurugenzi wa Necta sasa ni muislamu ,acheni visingizio nyanyueni watoto wenu kielimu we hujiulizi kwanini mikoa yenye waislamu wengi ndio yenye dropout kubwa ya wanafunzi je ni hujuma pia?,waislamu mna taasisi gani imara za kielimu? hakuna ,elimu sio lelemama
Tatizo ni kwamba unachukua mtazamo wa mtu binafsi au kikundi cha watu ndio unafanya kuwa Uislamu.
Uislamu mtu ukiusoma kwa watu ambao hawajui dini kwa haki yake kwa hakija lazima mtu atapotea na kujazwa fikra potufu. Swala kuwa elimu tofauti na dini kuona sawa na ukafiri hilo kimaandiko na kihistoria inakataaa kwani Uislamu umehimiza sana mwanadamu some chochote kike chenye manufaa katika dini yake na dunia yake kwa kuchunga mipaka ila dini lazima iwe kipaumbele cha kwanza kwa maana mtu akijua vyote akiwa mtupu katika dini ni hasara kubwa sana hivyo lazima awe na basic knowledge ya dini kwanza kisha afanye nyingine na wala haimaanishi kwamba mtu kuithamini dini ni kuitupa Dunia hapana kwani hata Allah amesisitiza mja kuwa "asisahau fungi lake katika dunia"
Kihistoria enzi ya Dola ya Uislamu Abbasid Caliphate Baghdad hata Dola ya Uislamu iliyokuwepo Andulasia (Spain) huko ndiko kulikuwa center ya science ,arts na innovation Duniani na gunduzi nyingi ambazo nyingine zinasaidia na zimeweka msingi wa sayansi ya sasa zilitoka huko...
Hizo kesi za kuibiwa maksi kwa wanafunzi ziko kwa dini zoteNga...
Soma makala hiyo hapo chini na nifahamishe wapi ulipo udini na nani wa kubadilika:
Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.
Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.
Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.
Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.
Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.
Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?
Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.
Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.
Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.
Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.
Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.
Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.
Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.
Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.
Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.
Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.
Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.
Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.
Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.
Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.
Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.
Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.
Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.
Na hii ni kwa masomo yote.
Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.
Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.
Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.
Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:
1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.
Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.
3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.
Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.
Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.
Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.
Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.
Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.
Tunaomba kuwasilisha,
Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Quote Reply
Uzuri kwenye Islamic schools wanasoma historia yako.Wakijichanganya kwenye necta wanalambwaKinj...
Huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mimi nimeandika kitabu kilichobadili kabisa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuieleza historia ya kweli na kuwaleta mashujaa ambao walifutwa.
Historia iliyokuwapo iliwafuta mashujaa wengi wake kwa waume na wengi katika hao Waislam na masheikh.
Kitabu cha Abdul Sykes si tu kimebadilisha historia ya Julius Nyerere bali imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.
Huu ndiyo umuhimu wa kitabu changu.
Na baada ya kuchapwa 1998 kiliingia katika Cambridge Journal of African History na mimi kama mwandishi nikatiwa katika mradi wa kuandika Dictionary of African Biography kamusi la volume 6 (Oxford University Press, New York 2011).
Haya nimeeleza mara nyingi.
Ukweli ni kuwa elimu yako ni ndogo katika ufahamu wa historia ya uhuru.
Jitulize acha kudhani unajua na niulize maswali kwa adabu utanufaika.
Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora wa Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
Waislam wamenipa nishani mbili kwa kuandika historia ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nimealikwa Vyuo Vikuu kadhaa ndani na nje ya mipaka yetu.
Mimi siko hapa kufanya utani.
Ninalo jina katika uandishi wa historia ya kweli ya Tanzania.
Rava...
Hizi si hadithi.
Soma utatambua.
EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 ikapigwa marufuku na serikali na BAKWATA ikaundwa.
Hii si hadithi ni historia ya Waislam wa Tanzania.
Sasa leo hii kwanini hamjengi shule na vyuo venu rais si muislamu ?,mtendaji mkuu wa necta si muislamu? mbona sioni shule zenu zikifanya vizuri ,mbona hamna vyuoMfumo wa elimu tangia ukoloni ulipindishwa kuwapa fursa wakiristo na kuwatenga waislamu. Huu ulikua ni mpango mmoja wa serikali ya kikoloni na kanisa katoliki. Hizi njama zilianza kutokea wajerumani na ukaendelezwa na waingereza na mpaka uhuru.
Kumbuka common factor ilikuwapo ni kanisa katika mipito yote serikali kuanzia wajerumani, waingereza na uhuru, kwa hiyo muendelezo wa hii njama haukuvurugwa katika mabadiliko yote ya serikali yaliotokea.
Taasisi za kiislamu hazikua na uhuru wa kutekeleza mipango yao hasa ya elimu wakati wa ukoloni. Baada ya uhuru wakaanzisha bidii kubwa kurekebisha mapungufu hayo ya elimu ndipo mwalimu Nyerere kuingilia na kudhoofisha taasisi za kiislamu na kuzima mipango yao yote ya kujiendeleza kielimu. Na hili limetia doa katika jina lake mwalimu sababu ni lazima alikua anajua kinachoendelea.
Muhimu sasa ihakikishwe kuwa fursa zinatolewa kwa haki na usawa. Na kanisa liwekwe mbali kabisa na shughuli za serikali.
Naomba nikuulize,serikali iliwahi kutaifisha shule za kikristo na kuzifanya za umma ,hivi ingekua ni shule za kiislamu ndio zimetaifishwa hali ingekuaje?,nchi ingekalika kweliMaku...
Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.
Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.
Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.
Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.
Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.
Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?
Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.
Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.
Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.
Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.
Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.
Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.
Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.
Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.
Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.
Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.
Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.
Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.
Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.
Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.
Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.
Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.
Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.
Na hii ni kwa masomo yote.
Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.
Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.
Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.
Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:
1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.
Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.
3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.
Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.
Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.
Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.
Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.
Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.
Tunaomba kuwasilisha,
Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Maku...Yaani unaokoteza Historia ya miaka 50 unajibu maswali ya Sasa! Najiuliza Leo hii Kuna mtoto au kijana wa Kiislam anakosa Elimu kwa vikeazo ya kimfumo?! Mbona wamejaa kwenye Shule na Vyuo vya Kanisa! Acha kuwatia upofu Waislam wachache ambao bado wamelala! Inawezekana changamoto zilkuwepo huko nyuma lakini Sasa watu wameamka wanasoma bila hofu...Nina Imani hata wewe ukiambiwa uchague Kati ya St Augustine ,Tumaini au St.Joseph University dhidi ya Muslm University pale Msamvu utachagua chaguo la kwanza!