Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Waliasisi Sawa kwa sababu ata mtu mjinga anaweza akaanzisha jambo ila kuliendeleza likamshinda,hivyo inampasa atafute mtu smart ili mambo yake yasonge mbele

Wale waswahili walianzisha TAA ila walikuwa na uelewa au elimu ndogo sana ndio maana waliona kabisa kuwa hawatoweza kufika popote,ikawabidi wamlazimishe Nyerere ajiunge kwenye harakati zao ili wafike sehemu waitakayo.........walitofautisha kati ya opinion na fact

Waislam ni vigumu sana kupiga hatua kama akijichanganya na Wakristo na hii sio Tanganyika pekee ake ata Nigeria wana Lia lia kama wewe unavyolia

huyo mzee mbishi tu. haya ni maneno ya Marehemu Bibi Titi Mohammed

 
Ni mfumo wa zamani sana tangu wakati wa Uhuru; Malima alikuwa anajua ku-sensionalize wafuasi wake sana hasa kwa vile alikuwa Profesa. ALikuwa waziri wa Elimu wakati mimi namaliza Chuo kikuu na miaka yote huko nilikopitia kuanzia Mock ya std7, STD7 kwenda Secondari, Mock ya Form 4, Form 4 na Form 6 tulikuwa tunatumia namba.
Ndicho nilichoambiwa, ila Mzee MS anasema muaisisi ni Malima. Hii ni hila kama hila nyingine kutugawa
 
kizee kimekimbia[emoji3][emoji3][emoji3]
Bwana Ngasera45,
Huwa sina kawaida ya kughadhibika kisha nikasema kuwa nimehamaki au nikarudisha tusi kama nilivyotukanwa.

Bwana Ngasera umeniudhi kwa kuwa umenitukana pasi na sababu kwa kuniita, ''kizee.''

Zingatia kuwa sikughadhibika kwa wewe kuniita mimi mzee.
Hakika mimi si kijana tena mimi ni mzee kwani nina miaka 71.

Namshukuru Mungu kwa umri mrefu na kunipitisha katika ujana uliokuw ana furaha na manufaa makubwa kwangu.

Leo niko London, Glasgow, kesho Paris, kesho kutwa Johannesburg, Dubai, Cairo kwingi.

Huu ndiyo ulikuwa ujana wangu.
Niheshimu.

Kilichonichoma ni kukuona kuwa unajribu kunidhalilisha kwa kuniita ''ki''
yaani ni ''kizee.''

NIngeweza nikakunyamazia lakini nitafanya kosa kwani utazoea kukosa adabu ukidhani kuwa unaweza kutukana wazee na isiwe lolote.

Hili mosi.
Pili wako watu hapa wananiheshimu sana.

Hawatafurahi kuona unanitukana nami nakaa kimya kama vile nimeridhia kutukanwa na napokea matusi yoko.

Inawezekana kama mama yako alikufunza adabu utajirudi na ukajua kuwa umekosea na hata kama hutonitaka radhi basi hutonitukana tena si mimi wala yeyote awaye yule.

Nini kimekuhamakisha?
Hupendi kusoma fikra zangu?

Ungeweza ukasema maneno yale yale ya mimi kukimbia na ujumbe ungefika tena kwa namna ambayo pengine hata mimi na wasomaji wengine wangenifurahi na kacheka.

Ungeweza kuandika, ''Mzee Mohamed kakimbia,'' au ''Mzee kakimbia.''

Hii ingependeza na naamini wengi ingewachekesha kuwa leo Mzee Mohamed kapatikana hadi anaukimbia ukumbi.

Hivi ndivyo tunavyonogesha mjadala unapendeza na kila mtu anaingia kuchangia kadri ya uwezo wake.

Mimi ni mzee lakini si ''ki'' si kizee.

Hata kama si baba yako lakini kwa umri wangu wa miaka 71 naamini naweza kuwa makamo ya baba yako.

Una wajibu wa kuniheshimu.

Sikukimbia ila nilikuwa na ugeni kutoka Ujerumani na Oman rafiki zangu wawili wamekuja kwenye kongamano wanaelekea Morogoro, MUM wamefika Dar es Salaam: Prof. Kai Kresse kutoka Zentrum Moderner Orient, Berlin na Prof. Ibrahim Noor kutoka Muscat.

Niliwafuata mjini kuwaleta nyumbani kwangu.
Hii ndiyo sababu nikapotea jukwaani kwa muda.

Sikukimbia.

Nakuombea Mungu akupe umri mrefu wenye manufaa kwako na kwa jamii inayokuzunguka.

1703954919669.jpeg

Kulia: Prof. Ibrahim Noor na kushoto ni Prof. Kai Kresse
naangalia baadhi ya vitabu walivyoniletea kama zawadi.​
 
Ndugu mwandishi tatizo la udini kwenye kazi yako ya sanaa ndio inafanya kazi zako zisifike mbali, nimekuwa nikikusoma sana, hebu sema ni lini wizara ya elimu inapofanya selection za watoto wanatumia kigezo cha dini? Ninavyojua kigezo cha ufaulu ndicho kinacho zingatiwa, sasa mtoto atafaulu vp kwenye hizo shule za kiislam zinazo kumbatia elimu ahela zaidi? Atafaulu vipi kwa kukaa na kobasi wenziwe na kukosa ushindani? Maana nani asie jua shule za kiislamu zimekumbatia ubaguzi wa dhahiri kwa kusomesha walio waislamu tu, tena uislamu upo zaidi kwenye jamii zilizo duni kielimu kama pwani. Tatu nani akasome chuo cha kiislamu moro chenye kila aina ya kukosa uhuru wa mtangamano na kuacha chuo kama st francis nk ambavyo watoto wanakuwa huru ku changamana na kushindana? Haya yote sidhani kama kwa usomi wako huyajui, shida ni ile elimu nyingine ya kimapokeo ambayo ina kinzana na mitizamo ya ki karne ya 21
DIY,
Nani kakuambia kuwa kazi zangu ni za udini.

Nani kakuambia kuwa kazi hazifiki mbali.

Hujanisoma sana.
Hapo hujasema kweli.

Ungenisoma sana ungefahamu na ungejua wapi nasimama.

Mimi nimefanya utafiti mkubwa katika historia ya Waislam wa Tanzania.

Kufanya hivi si udini.

Udini kwa lugha nyepesi ni kupendelea watu wa imani yako ukawabagua wa imani isiyokuwa yako.
 
Ndicho nilichoambiwa, ila Mzee MS anasema muaisisi ni Malima. Hii ni hila kama hila nyingine kutugawa
Plato...
Ikiwa sisi raia hatukubaliani na yale ambayo tunaona yana matatizo katika jamii inabidi serikali ndiyo ieleze ukweli.

Bahati mbaya hili swali la kubaguliwa Waislam katika elimu serikali wanaliogopa kulitolea tamko

Hili si tatizo la leo.

Warsha ilifikia kumwaga makaratasi ndani ya Bunge mwaka 1981 wakati Bunge liko Karimjee Hall ikieleza tatizo hili kwa takwimu.

Hiki ni kisa kirefu na nimepata kukiandika hapa.

Hatua ya serikali haikuwa kufanya uchunguzi kujua ukweli serikali ilishughulishwa kutaka kujua hawa Warsha ni nani na nani kiongozi wao.

Hii ikapelekea Sheikh Hussein Malik kufukuzwa Tanzania.
 
huyo mzee mbishi tu. haya ni maneno ya Marehemu Bibi Titi Mohammed

Mkata...
Nitashukuru kama utanifahamisha rejea ambayo Bibi Titi kasema maneno haya.

Nina mswada nimeandika wa maisha ya Bibi Titi katika utafiti wangu sikuona popote kauli hiyo.

Yawezekana ipo na wewe umeiona.
 
Hicho chuo kama sekondari...mashekhe wanapita na mijeledi waliwakuta tu mmekaa na wanawake mtatiwa mijeledi na kurukishwa kichura..yaani hakuna tofauti na primary jinsi wanavyochungwa.

Hovyo kabisa,bado wapo zama za ujima
 
Rava...
Hizi si hadithi.
Soma utatambua.

EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 ikapigwa marufuku na serikali na BAKWATA ikaundwa.

Hii si hadithi ni historia ya Waislam wa Tanzania.
Toka 1968 mpaka leo ni zaidi ya miaka 50! Mmeshindwa kujenga vyuo vikuu na kuvisimamia?

Je serikali ilifuta hiyo EAMWS kwa sababu inajenga chuo kikuu au kulikuwa na sababu zingine?
 
Kuna rafiki yangu sana kwao ni washika dini mno bimkubwa wake alimpeleka jamaa ubungo Islamic huko kulikua kusoma hakuna ni elimu akhera mwanzo mwisho plus kulishwa chuki dhidi ya nchi, na wazungu. akirudi kitaa jamaa mweupe kinoma bimdashi akaona sio poa akamuhamishia kirinjiko Islamic seminary huko ndio ilikua so watu wanaamshwa sana usiku kujifunza martial arts hakuna prepo huko usiku madarasa ni madojo akirudi kitaa mwamba anazid tu kua empty bimdashi akanyoosha mikono akamepeleka kijana wake jitegemee kumbe jamaa alikua kichwa bhana akamaliza form four na division two ya mwanzoni kabisa, bimkubwa wake angekaza fuvu angebaki na kilaza mwenye msimamo mkali alieiva kwenye sanaa za kimapigano
Hawa jamaa wanawaza karate tu.

Shule niliyosoma ilijengwa na wamissionari so ilikuwa na kanisa pale. Baadaye serikali ikazibinafsisha.

Wakati tunasoma, hawa jamaa wakalalamika hawana sehemu ya kufanyia ibada ilhali wakristu wana kanisa. Wakapewa eneo la swimming pool.

Ajabu wakaanza makarate huko ndani badala ya kufocus na ibada.
 
Kuokota sio lazima uokote vibaya...hongera Kwa uandishi...! Suala ni je,Leo hii Kuna kikwazo chochote Cha mtoto wa Kiislam kupata Elimu Bora kuanzia CHEKECHEA HADI CHUO KIKUU?!
Analikwepa hili swali. Analeta waraka wa enzi na enzi.
 
Toka 1968 mpaka leo ni zaidi ya miaka 50! Mmeshindwa kujenga vyuo vikuu na kuvisimamia?

Je serikali ilifuta hiyo EAMWS kwa sababu inajenga chuo kikuu au kulikuwa na sababu zingine?
City...
Miaka ya 1970 OIC walitaka kujenga Chuo Kikuu serikali ikakataa kutoa kibali.

Chuo kikajengwa Mbale, Uganda.
Sababu ya kupigwa marufuku EAMWS ni kutaka kujenga Chuo Kikuu.

Ikafutwa EAMWS na kuundwa BAKWATA.
 
Analikwepa hili swali. Analeta waraka wa enzi na enzi.
City...
Hapana hilo ndilo jibu lake sijakwepa.
Ikiwa wewe hukulipenda jibu hili mimi sina jibu lingine.

Ikiwa hukupendezewa na huo waraka ni bahati mbaya kwako.

Muhimu ni kuwa waraka huo ni sehemu ya historia ya Waislam wa Tanzania.
 
City...
Miaka ya 1970 OIC walitaka kujenga Chuo Kikuu serikali ikakataa kutoa kibali.

Chuo kikajengwa Mbale, Uganda.
Sababu ya kupigwa marufuku EAMWS ni kutaka kujenga Chuo Kikuu.

Ikafutwa EAMWS na kuundwa BAKWATA.
Sawa. Sasa mzee, kwanini Bakwata haijajenga chuo chochote?
Au la, kwanini hamjaanzisha taasisi mbadala wa EAMWS ili mtimize mpango uliokuwepo. Kama shida ilikuwa Nyerere na serikali yake, alikoma kuwa rais miaka takribani 40 iliyopita.
 
Back
Top Bottom