kizee kimekimbia[emoji3][emoji3][emoji3]
Bwana Ngasera45,
Huwa sina kawaida ya kughadhibika kisha nikasema kuwa nimehamaki au nikarudisha tusi kama nilivyotukanwa.
Bwana Ngasera umeniudhi kwa kuwa umenitukana pasi na sababu kwa kuniita, ''kizee.''
Zingatia kuwa sikughadhibika kwa wewe kuniita mimi mzee.
Hakika mimi si kijana tena mimi ni mzee kwani nina miaka 71.
Namshukuru Mungu kwa umri mrefu na kunipitisha katika ujana uliokuw ana furaha na manufaa makubwa kwangu.
Leo niko London, Glasgow, kesho Paris, kesho kutwa Johannesburg, Dubai, Cairo kwingi.
Huu ndiyo ulikuwa ujana wangu.
Niheshimu.
Kilichonichoma ni kukuona kuwa unajribu kunidhalilisha kwa kuniita ''ki''
yaani ni ''kizee.''
NIngeweza nikakunyamazia lakini nitafanya kosa kwani utazoea kukosa adabu ukidhani kuwa unaweza kutukana wazee na isiwe lolote.
Hili mosi.
Pili wako watu hapa wananiheshimu sana.
Hawatafurahi kuona unanitukana nami nakaa kimya kama vile nimeridhia kutukanwa na napokea matusi yoko.
Inawezekana kama mama yako alikufunza adabu utajirudi na ukajua kuwa umekosea na hata kama hutonitaka radhi basi hutonitukana tena si mimi wala yeyote awaye yule.
Nini kimekuhamakisha?
Hupendi kusoma fikra zangu?
Ungeweza ukasema maneno yale yale ya mimi kukimbia na ujumbe ungefika tena kwa namna ambayo pengine hata mimi na wasomaji wengine wangenifurahi na kacheka.
Ungeweza kuandika, ''Mzee Mohamed kakimbia,'' au ''Mzee kakimbia.''
Hii ingependeza na naamini wengi ingewachekesha kuwa leo Mzee Mohamed kapatikana hadi anaukimbia ukumbi.
Hivi ndivyo tunavyonogesha mjadala unapendeza na kila mtu anaingia kuchangia kadri ya uwezo wake.
Mimi ni mzee lakini si ''ki'' si kizee.
Hata kama si baba yako lakini kwa umri wangu wa miaka 71 naamini naweza kuwa makamo ya baba yako.
Una wajibu wa kuniheshimu.
Sikukimbia ila nilikuwa na ugeni kutoka Ujerumani na Oman rafiki zangu wawili wamekuja kwenye kongamano wanaelekea Morogoro, MUM wamefika Dar es Salaam: Prof. Kai Kresse kutoka Zentrum Moderner Orient, Berlin na Prof. Ibrahim Noor kutoka Muscat.
Niliwafuata mjini kuwaleta nyumbani kwangu.
Hii ndiyo sababu nikapotea jukwaani kwa muda.
Sikukimbia.
Nakuombea Mungu akupe umri mrefu wenye manufaa kwako na kwa jamii inayokuzunguka.
Kulia: Prof. Ibrahim Noor na kushoto ni Prof. Kai Kresse
naangalia baadhi ya vitabu walivyoniletea kama zawadi.