Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Rava...Sasa leo hii kwanini hamjengi shule na vyuo venu rais si muislamu ?,mtendaji mkuu wa necta si muislamu? mbona sioni shule zenu zikifanya vizuri ,mbona hamna vyuo
Majibu ya nini hapo?....haya mambo bado mmeyakumbatia tu ?Stux...
Wa kutoa majibu wamekuwa kimya hata pale tatizo hili lilipoletwa Bungeni.
Wewe unajibu kama nani?
Sisi tunasubiri majibu kutoka serikalini.
Rava...Hizo kesi za kuibiwa maksi kwa wanafunzi ziko kwa dini zote
Proved,Majibu ya nini hapo?....haya mambo bado mmeyakumbatia tu ?
Nan...Uzuri kwenye Islamic schools wanasoma historia yako.Wakijichanganya kwenye necta wanalambwa
Kama wanafahamika basi idadi yao ni ndogo sana.Wild...
Mdomo haumkatai bwana wake.
Wasomi Waislam wanafahamika.
mpaka mtendaji mkuu wa serikali ni muislamu haya majitu yana tabia ya kulalamika dunia nzimaSasa leo hii kwanini hamjengi shule na vyuo venu rais si muislamu ?,mtendaji mkuu wa necta si muislamu? mbona sioni shule zenu zikifanya vizuri ,mbona hamna vyuo
Rava,Naomba nikuulize,serikali iliwahi kutaifisha shule za kikristo na kuzifanya za umma ,hivi ingekua ni shule za kiislamu ndio zimetaifishwa hali ingekuaje?,nchi ingekalika kweli
Wewe unaweza kwenda kusoma chuo discussion lazima mkae kuanzia 3 kama jinsia ni tofauti au unachapwa kama mwanafunzi wa sekondari na msingi we uliona wapi karne hii ya technolojia chuo kinaendeshwa kama Kipindipi cha mashahid vile..Kipindi cha Ali Hassan Mwinyi, Aga Khan alikuja nchini kwa mara ya kwanza baada ya kutokanyaga ardhi ya Tanzania kwa miaka 20. Kwa maneno ya Mohamed Said Aga Khan aliitisha mkutano wa Waislamu ambao una mchanganyiko wa BAKWATA na wawakilishi wa iliyokuwa EAMWS. Na kwenye mkutano huo HAKUKUWA na MKRISTU hata mmoja. Yasemekana Songambele alisema Waislamu hawahitaji Chuo Kikuu.
Mwaka 2000 wakati wa B W Mkapa, akaamua kuwapa jamii ya Waislamu kilichokuwa Chuo cha TANESCO pale Morogoro.
Je ni Waislamu wangapi wenye passmark za juu za A- Level wanadahiliwa pale Morogoro dhidi ya Waislamu wanaochagua kwenda vyuo visivyo na itikadi ya dini kama UDSM, Mzumbe, SUA, SAUT na MUHAS?
Mumeshindwa kujua mnchotaka, bado Mohamed Said unawalaumu JK Nyerere na WAKRISTU kuhusu elimu.
Mfumo wa elimu ulipindishwa vipi wakati wakoloni ndio waliokuja na elimu yao na sharti ili upate elimu yao ilikulazimu ukubali imani yao sasa hapo mfumo ulipindishwa vipi..Mfumo wa elimu tangia ukoloni ulipindishwa kuwapa fursa wakiristo na kuwatenga waislamu. Huu ulikua ni mpango mmoja wa serikali ya kikoloni na kanisa katoliki. Hizi njama zilianza kutokea wajerumani na ukaendelezwa na waingereza na mpaka uhuru.
Kumbuka common factor ilikuwapo ni kanisa katika mipito yote serikali kuanzia wajerumani, waingereza na uhuru, kwa hiyo muendelezo wa hii njama haukuvurugwa katika mabadiliko yote ya serikali yaliotokea.
Taasisi za kiislamu hazikua na uhuru wa kutekeleza mipango yao hasa ya elimu wakati wa ukoloni. Baada ya uhuru wakaanzisha bidii kubwa kurekebisha mapungufu hayo ya elimu ndipo mwalimu Nyerere kuingilia na kudhoofisha taasisi za kiislamu na kuzima mipango yao yote ya kujiendeleza kielimu. Na hili limetia doa katika jina lake mwalimu sababu ni lazima alikua anajua kinachoendelea.
Muhimu sasa ihakikishwe kuwa fursa zinatolewa kwa haki na usawa. Na kanisa liwekwe mbali kabisa na shughuli za serikali.
Said Mohamed angeenda huko chuo kuwafunda uandishi. Muundo wa hii kitu kama ya wakaanfa chips na si ya wasomi wa chuo.Chuo kinatandika wachuo viboko??View attachment 2857330
Kwa mfumo wa shule za kanisa, huwezi kusoma kama sio the best upstairs na wana level ya ufaulu na usipoifikia, unaondolewa kwenye mfumo. Unadhani kwa system hiyo kuna mwanafunzi asiye smart au lazy atabaki shuleni??....Rava...
Sijasikia Wakristo wakilalamika kuwa NECTA inahujumu shule za Kanisa.
Hakika subra ni Iman...Mdukuzi,
Subra ni katika mambo ambayo Allah anasema katika Qur'an kuwa kila mwenye kusubiri yuko pamoja na Mwenyezi Mungu.
Naam tuko katika kusubiri.
Kuokota sio lazima uokote vibaya...hongera Kwa uandishi...! Suala ni je,Leo hii Kuna kikwazo chochote Cha mtoto wa Kiislam kupata Elimu Bora kuanzia CHEKECHEA HADI CHUO KIKUU?!Maku...
Siokotezi.
Ningekuwa wa kuokoteza nisingesikilizwa.
Nafanya utafiti:
PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
1.The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
2.The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
3.Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
4.Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
5.Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
6.Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
7.Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
8.Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
9.Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
10.Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
11.The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
12.Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
13.Sal Davis, An Autobiography, Readit/Amazon, 2023, Dar es Salaam
14.In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
15.Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
16.Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
17.The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
18.Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
19.The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
20.Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
21.Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
22.Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
23.Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
24.Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
25.Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
26.Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
27.Awards: Several Awards
28.Visiting Scholar: (2011)
29.University of Iowa, Iowa City, USA
30.Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
31.Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
32.OTHER COUNTRIES VISITED
33.Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
Ile ni haki au wanafanya muendelee kuwa wapumbavu?Himars,
Baada ya maandamano haki ikapatikana.
Shida ya waislamu nyie hamuangalii matatizo yenu kutokea kwenu ila huwa mnatafuta mbuzi wa kafara kwamba matatizo yenu anasababisha mtu mwingine ambae mmeshamtengeneza akili kuwa ni mkristo...... Angalia matajiri karibu wakubwa wote Tanzania ni waislamu kwanini wakristo wasiwahujumu kwa hilo wawahujumu kwenye elimu.... Waislamu nyie mnaamini kwenye kueneza uislamu bila kujifungamanisha na mazingira nje ya uislamu... Badilisheni kwanza mtazamo huu muone kama hali haitabadilikaTuanze hapa tulipo hivi sasa kisha nitaweka tulipotokea baada ya uhuru:
TUJIKUMBUSHE
Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.
Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.
Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.
Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.
Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.
Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.
Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?
Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.
Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.
Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.
Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.
Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.
Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.
Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.
Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.
Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.
Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.
Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.
Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.
Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.
Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.
Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.
Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.
Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.
Na hii ni kwa masomo yote.
Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.
Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.
Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.
Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:
1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.
Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.
3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.
Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.
Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.
Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.
Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.
Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.
Tunaomba kuwasilisha,
Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Sasa turudi nyuma wakati tumepata uhuru:
Ipyax,
Yametokea.
Serikali haiko tayari kutoa majibu.
Nina mengi naweza kukueleza muhimu ni wewe uwe tayari kusikiliza.
Marais Waislam hawakuchaguliwa kuchunguza watendaji Wakristo ndani ya serikali wana mchango gani katika matatizo haya yanayoelezwa na Waislam.
Endapo Rais Muislam ataingia madarakani na kuanza kuchunguza tatizo hili atakuwa anatengeneza tatizo kubwa zaidi linaloweza kuigawa nchi zaidi.
Hili la Waislam kuwekeza katika elimu hapa si mahali pake ila ningependa kukufahamisha kuwa baada ya kupatikana uhuru mwaka wa 1961 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alijiuzulu siasa na kuanzisha taasisi yake, "Daawat Islamiyya," yeye akiwa Mwenyekiti na Katibu wake Schneider Abdillah Plantan.
Sheikh Hassan bin Ameir akasema sababu ya yeye kujiuzulu siasa ni kuwaongoza Waislam katika kutafuta elimu kama alivyowaongoza katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
(Naamini inawezekana historia hii ninayokueleza ikakupa tabu kwani hujapata kuisoma popote kuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mwanachama wa TANU na kapigania uhuru.
Schneider Plantan yeye ndiye aliyesimama mwaka wa 1950 kuutoa uongozi wa wazee katika TAA Rais ambae ni kaka yake, Thomas Plantan na Katibu Clement Mohamed Mtamila na kuingiza uongozi wa vijana Dr. Vedasto Kyaruzi kama President na Abdul Sykes Katibu).
Mwaka wa 1962 Sheikh Hassan bin Ameir akishirikiana na EAMWS wakaitisha Muslim Congress agenda kuu ikiwa elimu.
Hii Muislam Congress ndiyo iliyoweka mpango wa kujenga shule Tanganyika nzima na Chuo Kikuu na kazi ilianza mara moja.
Mwaka wa 1968 Rais Julius Nyerere akaweka jiwe la msingi kujenga Chuo Kikuu.
Miezi miezi michache baadae Rais Nyerere akaivunja EAMWS na kuunda BAKWATA.
Uwekezaji wa Waislam katika elimu na ujenzi wa Chuo Kikuu na shule ukakoma hapo.
Historia hii ni ndefu lakini naamini nimekujibu swali lako na umeelewa matatizo yanayowakabili Waislam.