Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Waislam tuna matatizo yetu ya ndani, makubwa kuliko hayo ya nje. Na hatuwezi kamwe kuyatatua ya nje, sababu ya ndani hatujayatatua. Siku tukikubali tuna matatizo ya ndani, na tukayatatua, basi tutamaliza matatizo yetu ya nje siku moja tu.

Wild...
Mdomo haumkatai bwana wake.
Wasomi Waislam wanafahamika.
 
Mfumo wa elimu tangia ukoloni ulipindishwa kuwapa fursa wakiristo na kuwatenga waislamu. Huu ulikua ni mpango mmoja wa serikali ya kikoloni na kanisa katoliki. Hizi njama zilianza kutokea wajerumani na ukaendelezwa na waingereza na mpaka uhuru.
Kumbuka common factor ilikuwapo ni kanisa katika mipito yote serikali kuanzia wajerumani, waingereza na uhuru, kwa hiyo muendelezo wa hii njama haukuvurugwa katika mabadiliko yote ya serikali yaliotokea.

Taasisi za kiislamu hazikua na uhuru wa kutekeleza mipango yao hasa ya elimu wakati wa ukoloni. Baada ya uhuru wakaanzisha bidii kubwa kurekebisha mapungufu hayo ya elimu ndipo mwalimu Nyerere kuingilia na kudhoofisha taasisi za kiislamu na kuzima mipango yao yote ya kujiendeleza kielimu. Na hili limetia doa katika jina lake mwalimu sababu ni lazima alikua anajua kinachoendelea.

Muhimu sasa ihakikishwe kuwa fursa zinatolewa kwa haki na usawa. Na kanisa liwekwe mbali kabisa na shughuli za serikali.
 
Msikiti tu wa mtambani pale kinondoni,lilikuwa eneo la posta
Ben mkapa huyo huyo aliwaachia
Mjenge pale
Hebu tupunguze kulalamika

Ova
Nilisikia tetesi wengine wanasema Ben anawanyamazisha ila mpango wa kukinukisha uko palepela
 
Kinj...
Unajua kiwango cha elimu ya waasisi wa African Association?
Huijui historia hii.

TAA haukuasisiwa iliyoasisiwa ni African Association mwaka wa 1929 na mwaka wa 1948 ikabadili jina kuwa Tanganyika African Association.

Waasisi wa African Assocation: President Cecil Matola, Secretary Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Viongozi wa TAA 1950 walikuwa hawa: President Dr. Vedsto Kyaruzi, Secretary Abdul Sykes na wakaunda Political Sub Committee: Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.

Viongozi wa TAA 1953: J. K. Nyerere, President, Abdulwahid Sykes, Vice President, J. P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Minutes Secretary; Committee Members: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.

Nyerere hakulazimishwa na yeyote kujiunga na TAA.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kuna historia yote hii kwa ushahidi wa Nyaraka.
Hao viongozi wote uliowataja Kuna yoyote aliweza kumzidi Nyerere kielimu au ata kimtazamo?? Mzee wakati mwingine Sema tu ukweli kuwa Uislam hauna nguvu ya kupambana pamoja na Uikristo,hivyo kilichobaki ni kulia Lia eti tunaonewa lakini ukweli sisi ndio tunaonea watoto wetu wenyewe
 
John...
Waislam vipi wawe na uwezo mdogo wa kufikiri ilhali wao ndiyo walioasisi African Association 1929 na wakaunda TANU kupigaia uhuru wa Tanganyika tena wake kwa waume?

Au hujasoma historia ya Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Suleiman Takadir kwa kuwataja wachache au Shariffa bin Mzee, Tatu bint Mzee, Halima Selengia na Titi Mohamed?

Kawadanganye wajinga wenzio,hicho chama kilipewa ruzuku na mkoloni.
 
Hao viongozi wote uliowataja Kuna yoyote aliweza kumzidi Nyerere kielimu au ata kimtazamo?? Mzee wakati mwingine Sema tu ukweli kuwa Uislam hauna nguvu ya kupambana pamoja na Uikristo,hivyo kilichobaki ni kulia Lia eti tunaonewa lakini ukweli sisi ndio tunaonea watoto wetu wenyewe
Kinj...
Huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi nimeandika kitabu kilichobadili kabisa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuieleza historia ya kweli na kuwaleta mashujaa ambao walifutwa.

Historia iliyokuwapo iliwafuta mashujaa wengi wake kwa waume na wengi katika hao Waislam na masheikh.

Kitabu cha Abdul Sykes si tu kimebadilisha historia ya Julius Nyerere bali imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huu ndiyo umuhimu wa kitabu changu.

Na baada ya kuchapwa 1998 kiliingia katika Cambridge Journal of African History na mimi kama mwandishi nikatiwa katika mradi wa kuandika Dictionary of African Biography kamusi la volume 6 (Oxford University Press, New York 2011).

Haya nimeeleza mara nyingi.

Ukweli ni kuwa elimu yako ni ndogo katika ufahamu wa historia ya uhuru.

Jitulize acha kudhani unajua na niulize maswali kwa adabu utanufaika.

Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora wa Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Waislam wamenipa nishani mbili kwa kuandika historia ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimealikwa Vyuo Vikuu kadhaa ndani na nje ya mipaka yetu.

Mimi siko hapa kufanya utani.

Ninalo jina katika uandishi wa historia ya kweli ya Tanzania.
 
Mfumo wa elimu tangia ukoloni ulipindishwa kuwapa fursa wakiristo na kuwatenga waislamu. Huu ulikua ni mpango mmoja wa serikali ya kikoloni na kanisa katoliki. Hizi njama zilianza kutokea wajerumani na ukaendelezwa na waingereza na mpaka uhuru.
Kumbuka common factor ilikuwapo ni kanisa katika mipito yote serikali kuanzia wajerumani, waingereza na uhuru, kwa hiyo muendelezo wa hii njama haukuvurugwa katika mabadiliko yote ya serikali yaliotokea.

Taasisi za kiislamu hazikua na uhuru wa kutekeleza mipango yao hasa ya elimu wakati wa ukoloni. Baada ya uhuru wakaanzisha bidii kubwa kurekebisha mapungufu hayo ya elimu ndipo mwalimu Nyerere kuingilia na kudhoofisha taasisi za kiislamu na kuzima mipango yao yote ya kujiendeleza kielimu. Na hili limetia doa katika jina lake mwalimu sababu ni lazima alikua anajua kinachoendelea.

Muhimu sasa ihakikishwe kuwa fursa zinatolewa kwa haki na usawa. Na kanisa liwekwe mbali kabisa na shughuli za serikali.
Hivi ktk Dunia ya Leo mtoto ww Kiislam anapata changamoto gani kwenye mchajato wa Elimu?
 
Kinj...
Huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi nimeandika kitabu kilichobadili kabisa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuieleza historia ya kweli na kuwaleta mashujaa ambao walifutwa.

Historia iliyokuwapo iliwafuta mashujaa wengi wake kwa waume na wengi katika hao Waislam na masheikh.

Kitabu cha Abdul Sykes si tu kimebadilisha historia ya Julius Nyerere bali imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huu ndiyo umuhimu wa kitabu changu.

Na baada ya kuchapwa 1998 kiliingia katika Cambridge Journal of African History na mimi kama mwandishi nikatiwa katika mradi wa kuandika Dictionary of African Biography kamusi la volume 6 (Oxford University Press, New York 2011).

Haya nimeeleza mara nyingi.

Ukweli ni kuwa elimu yako ni ndogo katika ufahamu wa historia ya uhuru.

Jitulize acha kudhani unajua na niulize maswali kwa adabu utanufaika.

Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora wa Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Waislam wamenipa nishani mbili kwa kuandika historia ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimealikwa Vyuo Vikuu kadhaa ndani na nje ya mipaka yetu.

Mimi siko hapa kufanya utani.

Ninalo jina katika uandishi wa historia ya kweli ya Tanzania.
Ni sawa ila hebu tuambie ,hali ilivyo Sasa Kuna kikwazo chochote Cha mtoto wa Kiislam kupati ilimu kadri ya uwezo wake?!
 
Msikiti tu wa mtambani pale kinondoni,lilikuwa eneo la posta
Ben mkapa huyo huyo aliwaachia
Mjenge pale
Hebu tupunguze kulalamika

Ova
Hawa watu Nyerer amewaanzishia BAKWATA ili wawe na chombo Cha kuwaunganisha, haikuishia hapo, akawapa prime area kule karibu na Taifa , KWASABABU hawana maoni, wakauza lile eneo wapate pesa ya ulevi. Bado mwendazake akahangaika huku na kule ili wapate mskiti mzuri pale kino.
Ben kawapa chuo Moro. Waulize AHM, JK na mpendwa wamewafanyia Nini?
 
Kipindi Cha Ali Hassan Mwinyi Aga Khan alikuja nchini kwa mara ya kwanza baada ya kutokanyaga ardhi ya Tanzania kwa miaka 20. Kwa maneno ya Mohamed Said Aga Khan aliitisha mkutano wa Waislamu ambao una mchanganyiko wa BAKWATA na wawakilishi wa iliyokuwa EAMWS. Na kwenye mkutano huo HAKUKUWA na MKRISTU hata mmoja. Yasemekana Songambele alisema Waislamu hawahitaji Chuo Kikuu.

Mwaka 2000 wakati wa B W Mkapa, akaamua kuwapa jamii ya Waislamu kilichokuwa Chio cha TANESCO pale Morogoro. Je ni Waislamu wangapi wenye passmark za juu za A- Level wanadahiliwa pale Morogoro dhidi ya Waislamu wanaochagua kwenda vyuo visivyo na itikadi ya dini kama UDSM, Mzumbe, SUA, SAUT na MUHAS?

Mumeshindwa kujua mnchotaka, bado Mohamed Said unawalaumu JK Nyerere na WAKRISTU kuhsu elimu.
Nyerere alitaifisha shule nyingi sana za kikiristu na kuzifanya za umma ili watu wote wasome bila kujali dini zao. Elimu ya Msingi hadi Chuo kikuu ilikuwa bure kwa wote, lakini watu waliofundishwa kulaumu watatafuta kila sababu kuwa waislamau walionewa wakati hali halisi ilikuwa kwamba mitihani yote kuanzia ule wa darsa la saba hadi wa Form 6 ulikuwa unatolewa kwa namba ili kuepuka bias ya majina, lakini bado watu walilalamika kuonewa tu. Nadhani watu wengine mafunzo ya dini wanayopata ni ya kuamini kuwa wanaonewa tu.
 
Kinj...
Huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi nimeandika kitabu kilichobadili kabisa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuieleza historia ya kweli na kuwaleta mashujaa ambao walifutwa.

Historia iliyokuwapo iliwafuta mashujaa wengi wake kwa waume na wengi katika hao Waislam na masheikh.

Kitabu cha Abdul Sykes si tu kimebadilisha historia ya Julius Nyerere bali imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.

Huu ndiyo umuhimu wa kitabu changu.

Na baada ya kuchapwa 1998 kiliingia katika Cambridge Journal of African History na mimi kama mwandishi nikatiwa katika mradi wa kuandika Dictionary of African Biography kamusi la volume 6 (Oxford University Press, New York 2011).

Haya nimeeleza mara nyingi.

Ukweli ni kuwa elimu yako ni ndogo katika ufahamu wa historia ya uhuru.

Jitulize acha kudhani unajua na niulize maswali kwa adabu utanufaika.

Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora wa Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Waislam wamenipa nishani mbili kwa kuandika historia ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimealikwa Vyuo Vikuu kadhaa ndani na nje ya mipaka yetu.

Mimi siko hapa kufanya utani.

Ninalo jina katika uandishi wa historia ya kweli ya Tanzania.
Mzee wangu unazunguka sana na hutaki kuukubali ukweli........hakuna ambae hajui kuwa waasisi wa harakati za kudai uhuru wa nchi walikuwa ni Waislamu tena walikuwa hawana DNA za utanganyika

Swali langu ni kuwa je,kwenye hao masheikh na Waislamu wote uliowataja nani alikuwa na uwezo Sawa na Nyerere kielimu au ata kimtazamo?? Ukinijibu hili swali nitajua kweli unachozungumza ni sahihi

Ata Zanzibar penyewe waasisi wa Mapinduzi ni Waislamu tena wengi wao masheikh ila bado Muikristo mmoja aliyeongoza Mapinduzi yale tukufu........kwahyo hii ni kusema kwamba Waislamu wapo vizuri kwenye kupiga mdomo ila inapotakiwa kuweka vitendo uwa inawashinda

Äta dola pindi inaposhikwa na Waislamu uwa haifanyi vyema na ufisadi uwa mwingi na akiingia Muikristo ndo huanza kusafisha machafu yote yale yaliyo achwa na Waislamu
 
Hivi ktk Dunia ya Leo mtoto ww Kiislam anapata changamoto gani kwenye mchajato wa Elimu?
Maku...

Waislam wa Tanzania na Tatizo la Udini Katika Wizara ya Elimu.

Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu.

Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.

Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo.

Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.

Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili?

Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.

Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.

Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza.

Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.

Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili.

Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari.

Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote.

Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah.

Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.

Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.

Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.

Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.

Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu.

Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.

Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli.

Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu.

Na hii ni kwa masomo yote.

Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.

Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.

Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi.

Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.

Mheshimiwa Waziri,
Ili kupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:

1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani.

Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.

3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.

4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.

Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote.

Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.

Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.

Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa.

Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.

Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.

Tunaomba kuwasilisha,

Mwenyekiti,
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
 
Katika kusoma kwangu Shule ya Msingi/Socondary/Chuo nimeona ni asilimia chache sana ya wanafunzi wa kiislamu wanao jibidisha sana katika elimu.

Wengi wao nilioona wanafanya vizuri. Yaani top 5 wa kiislamu nao walikua na akili sana kiasi kwamba walikua hawajitumi ukilinganisha na wengine.
hiyo shule umesoma ya wajinga mno. tangu lini mtu asiyejibidisha akawa anafaulu.
 
Ukweli usemwe;
Mimi nilikuwa Muislam ila baadae niliamua kuokoka,kwahiyo nitazungumza vyema sana kuhusu Uislam na Elimu kama ifuatavyo;

Uislam unaichukulia Elimu Dunia kama elimu ya kikaffir bali wanawekeza nguvu kubwa sana kwenye elimu akhera.......Nakumbuka Baba yangu alikuwa akitoka kazini swali la kwanza ni kuwa "Ulienda chuo (Madrasa)?" Na kama sikwenda basi atanichapa sana ila kama sikwenda skuli basi huchukulia kawaida tu..........na wazazi wengi wa kiislam wanataka wana wao wakalili Alif,Bee,Tee badala ya A,B,C.......wakati huo watoto wa kikristo wanapoteza muda wao mwingi kwenye Tuition na ata kama ni dini hujifunza Sunday school,tofauti kabisa na uislam ambao kila siku ni Kuhudhuria madras

Waislamu wao kwa wao mtu akisoma sana wanaanza kumuonea wivu kuwa kakengeuka na anataka kuwa kaffir.......Mimi Kuna dada yangu alisoma mpaka chuo sasa ule mtaa mzima hakuna binti wa Rika lake ambaye aliwahi kusoma vile na wengi wao waliposwa mapema sana kwa kisingizio cha dini......walianza kumuandama eti kwanini haolewi na umri amefikisha wa kuolewa,Kuna imaam wa msikiti akataka amuowe kama mke mdogo,dada akagoma aiseeh!!! Kilinuka ikabidi atoke zenj aje bara na mpaka anamaliza chuo hakuwahi kurudi........Aliolewa na Muikristo.

Waislamu hawataki kutoa nguvu zao kwenye mambo ya elimu kama wafanyavyo kwenye Dini pamoja na ndoa.........Unaweza ukafaulu kwenda vidato vya juu kielimu lakini watakao kuunga mkono kimawazo au kiuchumi ni wachache lakini ukitaka kuoa au kuolewa utaungwa mkono na Jamii nzima..........Waislamu wenyewe hawataki kujenga Skuli au Hospitali zao wenyewe kama wafanyavyo Wakristo,lakini ukipitishwa mchango wa kujenga Msikiti au kumlipa mwalimu wa madras pesa uwa yapatikana muda huo huo

Elimu ndio kila kitu ndugu zangu Waislamu .....Jamii ya wajinga ni rahisi sana kuwadanganya na kuwatawala, ndio maana tulishindwa kumtoa Sultan wenyewe mpaka tukasaidiwa na John Okello(Muikristo mmoja anawaongoza wazenj milioni 3 kudai kupigana vita)..... .....leo hii mikoa maskini ya Waislam ndio maskini sana kuliko ata ya Wakristo
Tatizo ni kwamba unachukua mtazamo wa mtu binafsi au kikundi cha watu ndio unafanya kuwa Uislamu.

Uislamu mtu ukiusoma kwa watu ambao hawajui dini kwa haki yake kwa hakija lazima mtu atapotea na kujazwa fikra potufu. Swala kuwa elimu tofauti na dini kuona sawa na ukafiri hilo kimaandiko na kihistoria inakataaa kwani Uislamu umehimiza sana mwanadamu some chochote kike chenye manufaa katika dini yake na dunia yake kwa kuchunga mipaka ila dini lazima iwe kipaumbele cha kwanza kwa maana mtu akijua vyote akiwa mtupu katika dini ni hasara kubwa sana hivyo lazima awe na basic knowledge ya dini kwanza kisha afanye nyingine na wala haimaanishi kwamba mtu kuithamini dini ni kuitupa Dunia hapana kwani hata Allah amesisitiza mja kuwa "asisahau fungi lake katika dunia"

Kihistoria enzi ya Dola ya Uislamu Abbasid Caliphate Baghdad hata Dola ya Uislamu iliyokuwepo Andulasia (Spain) huko ndiko kulikuwa center ya science ,arts na innovation Duniani na gunduzi nyingi ambazo nyingine zinasaidia na zimeweka msingi wa sayansi ya sasa zilitoka huko...
 
Mzee wangu unazunguka sana na hutaki kuukubali ukweli........hakuna ambae hajui kuwa waasisi wa harakati za kudai uhuru wa nchi walikuwa ni Waislamu tena walikuwa hawana DNA za utanganyika

Swali langu ni kuwa je,kwenye hao masheikh na Waislamu wote uliowataja nani alikuwa na uwezo Sawa na Nyerere kielimu au ata kimtazamo?? Ukinijibu hili swali nitajua kweli unachozungumza ni sahihi

Ata Zanzibar penyewe waasisi wa Mapinduzi ni Waislamu tena wengi wao masheikh ila bado Muikristo mmoja aliyeongoza Mapinduzi yale tukufu........kwahyo hii ni kusema kwamba Waislamu wapo vizuri kwenye kupiga mdomo ila inapotakiwa kuweka vitendo uwa inawashinda

Äta dola pindi inaposhikwa na Waislamu uwa haifanyi vyema na ufisadi uwa mwingi na akiingia Muikristo ndo huanza kusafisha machafu yote yale yaliyo achwa na Waislamu
Kinj...
Wewe ni mgeni katika somo hili.

Nilichoandika katika historia ya uhuru ni kufutwa kwa historia ya kweli ikapachikwa historia ya uongo.

Kitabu changu kikasahihisha historia hii.

Kilichompa uongozi Mwalimu Nyerere katika TAA mwaka 1953 haikuwa elimu yake peke yake.

Nafasi ile ilitakiwa ishikwe na Mkristo ili kujenga umoja TANU isiingie katika kudai uhuru chama kikiwa kimejaa Waislamu na wengine wako nje.

Hii ndiyo ilikuwa fikra ya Hamza Mwapachu aliyowaeleza Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) walipomfuata Nansio, Ukerewe kutaka ushauri kuhusu kumwingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953.

Haya ninayokueleza si mageni katika Jukwaa la Historia.

Nina wanafunzi wengi hapa na wengi wamenufaika.

Njoo hapa kwa nia ya kusoma.

Hujafika makamo ya kujadili historia hii kwa kuwa huna ulijualo.

Sasa nataka nikufunze kanuni za uandishi.

Nukta zinakuwa tatu tu ...
Usizidishe.

Ingia hapo chini usome historia ya John Okello:

View: https://youtu.be/xlhYXGyQ2qI?si=z5Z4tXB_DH7wNyPK
 
Bado hutoi jibu la kueleweka unajikanyaga mwenyewe,inaonesha ni jinsi gani usivyokuwa na msimamo wa kueleweka mzee wangu

Nijibu swali langu kuwa kwenye wale waasisi wote wa TANU wa Kiislamu,Kuna yoyote alikuwa anamzidi Muikristo Nyerere elimu?

Kuhusu ushujaa wa Okello na Mapinduzi ya Zanzibar hilo halipingiki na liko wazi kabisa japo nyie Waislamu mnafanya kazi kubwa sana ili mfinye historia yake kuwa yeye sio Shujaa kwa sababu tu hakuwa Muislam

John Okello,field Marshall,Che Guevara of Africa and father of Zanzibar revolution.......Mungu awe naye siku zote
 
Back
Top Bottom