kichakaa man
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 5,500
- 5,164
Muungano lazima udumu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa maana hiyo ile january 12/1964 ilikuwa uhuru upi tena! Tanganyika wapeni Wazanzibari uhuru wao.
Muungano hauwez kuvunjika kamwe Mungu anaulinda umoja Ni nguvu
Ukweli mchungu ambao Mzee Nyerere aliona lakini alikataa kuukiri ni kwamba siku ambayo Zanzibar inatoka kwenye huu Muungano kutakuwa na machafuko makubwa sana huko Zanzibar. Lakini baada ya muda Zanzibar itatulia na kuwa taifa moja tajiri sana Afrika ya Mashariki, siyo tajiri kwa kubahatisha bali tajiri haswaaa na kitakuwa ndicho kitovu kikubwa cha dini ya Uislamu kusini mwa jangwa la sahara. Itafika kipindi hata kama tunaweza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi wao wanaweza kuishi vizuri kabisa bila bughudha ya Tanganyika.
Kardinali Pengo na baadhi ya viongozi wa dini wanaujua sana huu ukweli,
Mzee Nyerere alilijua hili ndiyo maana "akasema ukiwaacha Wazanzibari watapewa mapesa mengi kutoa kwa waarabu"
Ukikaa na Wazanzibari utakuja kugundua mbali na tofuati zao, wana kitu cha ziada ambacho sisi Watanganyika hatuna kabisa: Kwenya maslahi mapana ya Zanzibar CUF na CCM visiwani wote huwa na sauti moja.
NB: Kimkakati Zanzibar kutoka kwenye Muungano kunaweza kuwanufaisha sana kwasababu eno lao limekaa vizuri sana kijographia. Hasa hasa ukiangalia Maritime Silk Road inapita hapo baada ya Kutoka The Strait of Malacca kwa upande wa Bahari ya Pasifiki na Suez Canal ukiwa umetoka Ulaya. Kama wataamua kutanua bandari yao basi wanaweza kujihakikishia kuwa na soko kubwa sana la biashara za kimataifa kama ilivyo Dubai. Pia inaweza kuwapunguzia sana kutegemea Tanganyika kwasababu bidhaa zao wanaweza kuzipata kutoka Asia, Ulaya, Uarabuni na Mombasa (Haya yatafanyika kama watapata viongozi wenye akili na upeo mkubwa wa kufikiri bila kutumiwa kama vibaraka wa Tanganyika ili kuwagawanya Wazanzibar kama ilivyo sasa hivi)
Tanganyika wakiacha siasa za kidini na kibaguzi basi wanaweza kuitumia Zanzibar kama moja ya kitega uchumi kikubwa,
Pia Zanzibar inaweza ikaongezewa uhuru (Commercial Autonomy) kwenya masuala ya kibiashara kama Bandari na Kodi ili kuutenga mfumo wa kodi wa Muungano ili kuweza kutengeneza soko la kimtaifa ambapo wafanya biashara wa Tanganyika na Zanzibar wanaweza kupata bidhaa nyingi kwa bei ndogo kutoka Ulaya, Asia ya Mbali na Ghuba ya Uajemi. Haya yanawezekana kama tu, tutaamua kukaa kama Taifa na kuweka siasa na udini pembeni......ZANZIBAR INAWEZA KUUINGIZIA MUUNGANO PESA NYINGI SANA....
LONG LIVE THE UNION.............
THE FUTURE IS VERY BRIGHT FOR TANGANYIKA AND ZANZIBAR!
Mtafuteni mwandishi wa makala ndugu Joseph Mihangwa anaijua Zanzibar kuliko hata kina shen na Maalim Seif.
Huu muungano wetu kwa mujibu wa viongozi wa ccm ni "Muungano wa kipekee"
Matatizo ya Zanzibar hupikwa kutoka Tanganyika
soma hapa wavuti: Jisomee online: Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia
Ni ruhksa sheikh..., kasikilize kesi hii kwa uhuru wooote mzee...!hivi inaruhusiwa mwananchi wa kawaida kwenda kusikiliza kesi kama zifanyazo Mahakama nyingine?
Nakubaliana na wewe kidogo,
Matatizo mengi lakini siyo yote hasahasa ya kimfumo na kiutawala yanapikwa Tanganyika.
Lakini kuna mengine kama matabaka ya kijamii yamekutwa na yalikuwepo tangia enzi za Usultani.
Nijuavyo mimi, hakuna kesi yoyote hapo, kwa sababu hatuna mahakama yenye jurisdiction kusikiliza kesi ya kikatiba. Muungano ni suala la kikatiba, mahakama yenye uwezo huo ni mahakama ya katiba, ambayo haijawahi kuwa constituted Tanzania, labda sasa ndio tui constitute.
P
Sultani hakuwa na mamlaka yoyote. Mwenye mamlaka alikuwa ni mkoloni muingereza . Na ndio ukatafutwa uhuru wa Disemba 1963 . Ukisoma kitabu hichi utajua mengi wavuti: Jisomee online: Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia
Nijuavyo mimi, hakuna kesi yoyote hapo, kwa sababu hatuna mahakama yenye jurisdiction kusikiliza kesi ya kikatiba. Muungano ni suala la kikatiba, mahakama yenye uwezo huo ni mahakama ya katiba, ambayo haijawahi kuwa constituted Tanzania, labda sasa ndio tui constitute.
P
Tusitegemee nakala moja tu ya kihistoria,
Uingereza alikuja kuitawala Zanzibar baadae sana.
Eneo kubwa la Pwani ya Afrika Mashariki ilikuwa inatawaliwa na Sultani ambaye nyaraka za wazungu zinasema alikuwa tajiri sana. Haya basi tukubali kwamba mwenye mamlaka Zanzibar alikuwa ni Muingereza, lakini tusisahau mbinu-mkakati wa Utawala wa Uingereza ulikuwa siyo wa moja kwa moja (Indirect Rule); Hivyo basi hata kama Sultani alikuwa ni mtu wa pili alikuwa bado ana sehemu kubwa sana kiushawishi huko visiwani, kwasababu tofauti na sehemu nyingine alizotawala Muingereza, Zanzibar ilikuwa na idadi kubwa sana ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Kutawala nchi ya namna hii huwezi kufanikiwa bila kufanya makubaliano (Concessions) fulani na muhusika mkuu (Sultani).