UWOGA=UMASKINI
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 2,399
- 1,014
Labda kwa kuanza tu niwasalim wote na nawaomba muwe miongoni mwa mtakaookoa nafsi yangu iliyojaa maumivu yasiyo na kifani
Nilianza kuishi na mke wangu huyu 2008 kabla ya ndoa na tukabahatika kupata watoto wawili na mwaka 2018 january tukaamua kubariki ndoa
Na kilichokuwa kinachelewesha ndoa ilikuwa dini tofauti mimi ni mkristo yeye ni mwislam ila mwisho aliamua kubadili dini mwanzoni mwa mwaka 2009 na tukawa tunahudhuria ibada pamoja na wanetu mpaka january hii na tupo mkoa mmoja lakini wilaya tofauti
Point ya ushauri hii hapa naohitaji kwenu waungwana
Leo usiku huu kaniambia anarudia imani yake kwa kina na anahudhuria ibada na maadili yote ya imani yake (islamic) na hakuna wa kumrudisha nyuma tena
Ila pia anakiri kurudi kwenye imani yake hana maana kwamba hanipendi ananipenda na ataendelea kuniheshimu kama mume wake na pia hataachana na mimi labda mimi nitakapoamua kumuacha
Na pia naendelea kuniambia ameshaomba toba kwa mwenyezi mungu amsamehe madhambi yake yote aliyotenda kwa kipindi chote alichimchangana nabii issa na mungu
Hakuchoka wala kuishia hapo aliendelea kuniambia nimsamehe kwa maamuzi hayo na maisha yaendelea kama kawaida na pia alifanya ndoa kuweza kuturidhisha mimi na ndugu zangu
Japo anasema jambo hilo anaamini haliwezi vunja uhusiano wetu na hata akibaki katika imani hii ataendelea kupretend ambavyo yeye hataki kupritend na niliogopa kukuambia mda ila leo nimeamua kukuambia tu
Na haya yote yanatokea baada ya kumpeleka kwenye shule kurisit mtihani wake wa kidato 4 katika shule za kislam
Sasa naomba mnishauri nifanye nini kwa kuwa naona kama moyo unatoboka sijapata usingizi toka nilivyojaribu kulala saa 2 ya leo
Pili kiimani ikoje tena hii ndoa baada ya mwenzangu kuamua hivyo
Je kuna umuhimu wa kuendelea na mipango ya maisha ya pamoja mfano tulikuwa tumenunua viwanja vitatu na kimoja nimeandika jina langu viwili majina ya watoto na pia kiwanja kimojawapo tumeshaanza ujenzi na nilipanga kumalizia nyumba yetu mwezi wa nne je kuna umuhimu wa kufanya hivyo ?
Nb sikuweza kuamini yaliyotokea kwa kuwa yeye alibadili na kuwa mkisto bila kushawishiwa na mtu yeyote na kwa kweli tulipendana na nawapenda sana yeye na wanangu
Na kabla hajafanya maamuzi ya kuhamia ukristo 2009 alikuwa anateswa sana sana na mapepo na alipohamia tu ukristo toka kipindi hicho hajawahi kuangushwa na mapepo.