Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Achana naye mapema. Huko mbeleni sio kwema kabisa. Angalia watoto watalelewa vipi pindi mtakapokuwa mmeachana.
 
Sababu halali ya kuvunja ndoa in uzinifu tu. soma Mat 5:31, 32

31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;

32lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Pia soma Mat 19:3-12
3: Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

4Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

7Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

8Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

9Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
 
MKUU,UKIANGALIA SIGNATURE YANGU HUTAPATA SHIDA NA HILO.

HEBU CHUNGULIA HALAFU UJE TENA HAPA USEME CHOCHOTE.

AHSANTE.
 
Mie huwa nashangaa sana kuona watu wanataka kuvunja ndoa kwa tofauti ya dini hasa ukitilia maanani mke hana tatizo kwa watoto kufuata dini ya Baba yao.

Sioni shida mkeo kuabudu anapopaamini kwa sababu Mungu ni mmoja.
Cha muhimu mkae chini mkubaliane watoto hawatahusika kwenye dini yake aliyoirudia ili msiwachanganye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa na mimi huku wanamshauri mtu avunje ndoa kisa dini. Aiseee. Kwani mke kuwa imani tofauti na mumewe kitapungua nini kwenye ndoa yao?
Kama ni waroman Catholic ndoa mseto zipo
Mie huwa nashangaa sana kuona watu wanataka kuvunja ndoa kwa tofauti ya dini hasa ukitilia maanani mke hana tatizo kwa watoto kufuata dini ya Baba yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thread ya nyuma ulisema watoto wanne, leo umesema wawili.

Kinachosikitisha hapo ni yeye kusema alipretend kukuridhisha wewe na familia yako, maana hata hapo bado hujajua ni vingine vingapi anapretend.

Maamuzi ya busara yanahitajika.
 
Kuna watu dini tumezifanya kama ndo maisha, at the same time matendo yetu hayaakisi jinsi dini husika zinachofundisha na kuhitaji.

Kama wewe ni mtu wa dini kwa matendo haya yasingefika huku, at first place usingeishi na mtu kabla ya ndoa. The same person asingefanya aliyoyafanya.

Hapo unajaribiwa bosi, na mpaka dakika hii inaonekana mtihani unaenda kuwa mgumu kwako.

Omba Mungu akuongoze kwenye maamuzi yako.
 
Uko tayari kuona watoto wako wanalelewa na mama wa kambo? Je, unampenda mkeo? Katika hii miaka 11 ya kuwa pamoja purukushani za hapa na pale hazikosi, katika muda huo wa kuwa pamoja bado unaweza kutamka ni mke mwema ni mama mwema kwa watoto wenu?

Ukiweza kuyajibu maswali hayo kwa ufasaha bila kigugumizi basi unajua maamuzi yako yataegemea upande upi.

Kila la heri kwenye kufanya maamuzi magumu na mrejesho ukiweza muhimu.
Nikiri kweli nampenda na sijawahi penda wanangu walelewe na mama Wa kambo ila sasa hapa nafanyaje
 
Nakuambia amehudhuria kanisani miaka kumi na kubatizwa kabatizwa sasa nashindwa elewa na nimemwuliza uko serious akaniambia hawazi kurudi nyuma coz amepretendi mda mrefu dini ya kweli in uislam pekee hakuna nyinginee
Huyo umezaa nae,kuzaa ni mkataba kama mkataba unavyojua kuna sehemu lazima mukae mujue kulea watoto.Kua nae lakini asije akakubadilisha na imani. Ukimwambia unamuacha kwa imani yake akakubali ujue ana mchumba huko shuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
1. Ndugu yangu ni lazima kabisa ukubali kuwa ulikosea kwa kuoa mtu asiyekuwa wa imani yako. Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa maana kuna ushirika gani kati ya wasioamini na walioamini.

2. Kuishi wilaya tofauti nayo ni issue iliyochangia kwa asilimia 100% kwasababu kama mngekuwa mnaishi wote mnalala wote na mnaamka wote na mnasali wote usiku na asubuhi sidhani kama yangefikia hapo.

3. Inaonekana pia unashida katika imani, si mtu aliyemlingana Yesu kisiawasawa. Ni wale wa tia maji tia maji yaani bora mkristo tu jina. (Kumbadili mtu kutoka uislam kwenda roman huyo asilimia 99.9 atarudi tu dini yake, most of roman hawako serious na kuabudu, sorry kwa kauli hii. Lakini ndio ukweli wenyewe). Ukristo ni maisha halisi ya kila siku na kama wewe ungekuwa mtu uliyezama kwenye imani kwa Kuishi maisha ya msimamo wa kristo kwa maombi, kusoma neno kila siku na familia yako, na kuwa mfano kwa matendo mema , haya singetokea)

4. Kama ni mkristo halisi anayeishi maisha ya wokovu haswa, basi kuna mambo mawili, mosi-ni jaribu lako na unajua pa kulipeleka na si kulileta hapa jf maana hapa utapata stress tu, pili-kuna sehemu hukutimiza majukumu yako ya kiimani hadi mkeo akaona kuna gap and so hakuna haja ya kuendelea huku wakati kuna mambo anapungukiwa kiimani.

Ushauri:
Hakunq haja ya kuumiza kichwa kuhusu mkeo, zidisha mapenzi juu yake. Kama hujaamini haswa haswa, for the sake of your children tafta mchungaji aanze kukulea kwa kukufundisha jinsi ya kuomba. Baada ya hapo funga na kuomba kwa ajili ya mkeo bila hata yeye kujua maana hiyo ni vita ya kiroho kwa hiyo unatakiwa upigane kiroho. Ukifanya kwa uaminifu, matokeo utayaona baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA KWELI UMEIVA KIIMANI/KIROHO HAPO NI PA KUFANYIA MAAMUZI MAGUMU.

MFANO:

SAMSONI NA DELILA KUFIKIA CHANZO HADI SAMSONI ALIMSALITI MUNGU NI HUKO HUKO KUTOFAUTIANA KIIMANI.

DELILA ALIKUWA AKIABUDU MIUNGU WATU HUKU KWAO SAMSONI WALIKUWA WAKIMUABUDU MUNGU MUUMBA MBINGU NA ARDHI.

WAZAZI WAKE SAMSONI WALIMKATAZA SANA SAMSONI ASIJIHUSISHE NA DELILA KIMAHUSIANO SABABU HAWAKO SAWA KIIMANI, LAKINI SAMSONI ALISHUPAZA SHINGO HATIMAYE YALIMKUTA MATOKEO MABAYA AMBAYO HAKUYATEGEMEA KABISA KWA KUGUNDULIKA KWA SIRI YA NGUVU ZAKE NA KUTOBOLEWA MACHO.

NB:

"MSIFUNGIWE NIRA NA WASIOAMINI, HIZI IMANI ZINA SIRI NZITO SANA MPENDWA, NI WAKATI WAKO KUONESHA MSIMAMO KATI YA MKEO NA MUNGU YUPI NI BORA HASA KWAKO."

MUHIMU KATIKA VYOTE, JITAHIDI KUMSHIRIKISHA SANA MUNGU KTK HII CHANGAMOTO YAKO AKUPE HEKIMA KABLA HUJAFANYA MAAMUZI SAHIHI.

KILA LA HERI KAKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom