Hatoi matumizi ya mtoto, kaomba nimkopeshe pesa

Huyo hana mapenzi na wewe,na anayafahamu madhaifu yako anatumia kama silaha kukufanya anavyotaka! Fanya maamuzi songa mbele,la sivyo utajikuta hauna kitu at the end.
 
Yaani dada ni dharau kubwa sana,uo ujasiri huyo mwanaume anaupataje kama siyo dharau ni nini
 
ahaha,,we kauzu bibie
 
there's is thin line between love and hate

huyu huyu jamaa akitaka kupasha kiporo anapata
 
Pia nilimblock na katumia namba ngeni .Na kama kosa ni kukopesha,ningemkopesha kwa maandishi na angerudisha kwa riba.
Uondo mwanzo wa kurudisha penz upya mtakopeshana we mwisho atakwambia muish pamoja mlee mtoto ata kudanganya hana mtu na haja pata mtu sahii kama wewe, atakuita uende kichukua pesaza mtoto na muongee Zaid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huendaa jamaa hakuwa tayari kulea mtoto ....

Muwe mnashirikishana kwenye hatua za kubeba ujauzito, sio mnaanza kulialia badae bila sababu ....
Hakuwa tayari alipoiweka pekupeku alikuwa anatarajia nn?halafu Inaonyesha hana shida ni child support kutoa nayo ni shida...Dada usimpe hata 100 ila usiache kudai matumizi ya MTT ni wake
 
Ni kweli, lakini nikukumbushe tu kuwa ukiona mpaka mtu ana kila kitu kisha anakataa mimba hadi anakuja kudai DNA ya mtoto ili apate uhakika ujue hapo kuna tatizo sio bure, hapo Kuna kila dalili ya kutokuwepo kwa uaminifu kati yao ( ujue kila mtu anamfahamu vema mwenza wake) Kama mtu anaona Kuna kila dalili ya kusalitiwa au mabye umeona kwa macho yako then mtu anakuja kukwambia anamimba yako unadhani ni rahisi namna hiyo kukubali?

Sio kila anaye kataa mimba basi ni kwa ujinga, kukimbia majukumu au roho mbaya no wakati mwingine Kuna vitu vinatokea kwenye mahusiano vinashawishi mtu kukataa mimba ila havisemwi wazi badala yake point inayo onekana ni ile tu ya kukataa basi ila vyanzo haviangaliwi kabisa.

Mfano Kama huyu ana kila kitu kwa mujibu wa maelezo hufikirii kwanini kakataa hadi anadai vipimo vya DNA unayajua maumivu ya kabambikiwa mimba unalea mtoto si wako miaka kibao bila kujua then unakuja kustuka badae ushagharamika vya kutosha?

Okay, baada ya vipimo akakubali mwanae na akaanza kutoa matunzo ila ghafla akaacha hadi kafikia hatua ya kuja kukukopa pesa unadhani Kuna nini hapo kilimpata huyu jamaa?
Unadhani alikuwa anamkopa pesa kwa kumdhihahi au kumtapeli?

Best narudia kusema maisha yetu haya yana mambo mengi mno, katika mada kama hizi Kuna vitu haviwekwi wazi kisha anashambuliwa mtu mmoja.
Sawa lakini yote ni maisha na hakuna asiye kosea.
 
Ushauri wangu

Fanya vyoyote utakavyofanya uhakikishe huyo baba anatoa matunzo yote ya mtoto hata ikibidi kumpeleka ustawi wa jamii au mahakamani mpeleke! Mathalan imethibitika mtoto ni wake, hana budi kumlea tena na hiyo miezi ambayo hajalipa andika kama deni na lazima alipe!

Kwanini nasema hivi?

Wewe na jamaa inawezekana mmegombana, lakini mtoto na baba yake hawajagombana. Utapambana mwenyewe apo kujidai kumlea mtoto, baadae mtoto akiwa mkubwa atakusumbua sana umpeleke kwa baba yake! Usipompeleka utajenga uhasama mkubwa na mtoto ambae umemtesekea wewe mwenyewe na atakuona mbaya! Ukija kumpeleka kwa baba yake baadae, na akagundua baba ana hela, atakulaumu sana kwa kumkosesha fursa katika maisha!! And trust me, huwezi kumtenganisha mtoto wa kike na baba yake, bora ata angekua wa kiume.

Ishu kama hii ilimtokea dada yangu, kapambana na mtoto saizi yuko chuo. Mtoto kamtafuta baba yake mpaka kampata na sasa hivi mtoto na baba lao moja, mama ndio anaonekana kituko!


Sina "uduazi" huo
 
Dr. umeua [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1544]
 
Asante mkuu.Nilishafanya yote hayo hadi mahakamani but niliambulia patupu. Nikaona napoteza pesa kwa mwanasheria na muda.Thats why nikaachana nayo.

For now, ngoja niwekee mambo yangu kwenye mstari kuliko kumfikiria mtu mzima mwenye meno 32 asiyejua majukumu yake.

All in all, najua sehemu ya kumkomesha
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna vitu vingine vinachekesha na kusikitisha walah!!
 
lady Jay sasa nimejua ni binti. Maskini huyo mwanaume bado hajielewi! Mtoto wa Kike ndiye mkombozi wa mwanaume uzeeni. Ni kosa kubwa kwa mwanaume kumtupa mtoto wa Kike. Unapoinvest kwa mtoto wa kike unajiwekea security, hata akiwa na shilling mbili lazima atakupa moja abakie na moja. Mtoto wa kiume akikua atahangaika na mama yake na girlfriend wake. Wewe hata kukupigia simu inakuwa ni mtihani.

Jitahidi mama kuhakikisha baba yake anawajibika maana sie tumeyaona, baba hakumtunza mtoto ila akikua lazima ahangaike na baba yake. Mtoto wa Kike kwa baba ni Chanda na pete. Watoto wa kiume tunawazalia mama zao tu.

kwa upande wangu kila wakati najitahidi mtoto wa Kike afike mbali kielimu. Wakiume including me tunaboa kwa kusahau baba zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…