lady Jay sasa nimejua ni binti. Maskini huyo mwanaume bado hajielewi! Mtoto wa Kike ndiye mkombozi wa mwanaume uzeeni. Ni kosa kubwa kwa mwanaume kumtupa mtoto wa Kike. Unapoinvest kwa mtoto wa kike unajiwekea security, hata akiwa na shilling mbili lazima atakupa moja abakie na moja. Mtoto wa kiume akikua atahangaika na mama yake na girlfriend wake. Wewe hata kukupigia simu inakuwa ni mtihani.
Jitahidi mama kuhakikisha baba yake anawajibika maana sie tumeyaona, baba hakumtunza mtoto ila akikua lazima ahangaike na baba yake. Mtoto wa Kike kwa baba ni Chanda na pete. Watoto wa kiume tunawazalia mama zao tu.
kwa upande wangu kila wakati najitahidi mtoto wa Kike afike mbali kielimu. Wakiume including me tunaboa kwa kusahau baba zetu