Hatoi matumizi ya mtoto, kaomba nimkopeshe pesa

Makubwa!!!
 
Thank you
Asante mkuu. Ila huwezi mlazimisha mtu mzima kufanya majukumu yake.Mwenyewe babangu alikua na blabla kibao wakati wa kutoa matumizi na sijui anaendeleaje huko. Ila nikipata chochote siwezi msahau mamangu.

Watoto wanakua na wanaona. Huo muda wa kukimbizana nae Bora nikae nisimamie biashara. Ila nitamkomesha tu ,nitamkomeshaga tu.
 
Si rahisi mtoto wa Kike kwa baba. Unless aendelee kuwa mpuuzi baada ya mtoto kuvunja ungo. Nakueleza akiwa baba yake ni mjanja kama sie kwa watoto, humbandui kwa baba. Akiwa wa kiume hapo sawa. Nina mifano lukuki
 
Pole mkuu, kila jaribu huwa na mlango wa kuingia na kutokea. Hilo nalo litapita, just concentrate na mwanao huku ukisimamia ndoto zako.
 
Hii mada ilivyoanza nilifikiri naongelewa mimi! [emoji2363][emoji2363][emoji2363][emoji2305][emoji2305][emoji2305]
 
Ndio maa a wengine huwaambia watoto wait baba walishakufa kuepuka masumbufu kama hayo,.
 
Mungu baba awabariki sana kina mama wote wanaolea watoto wao bila usaidizi wa baba zao..!!
Ni ushauri wangu kuwa suala la kuanzisha familia liwe mmekubaliana, vinginevyo hutokea misuguano kama hii hasa mwanaume asiyejua thamani ya ubinadamu na asiyethubutu kuvaa kiatu cha mzazi mwenzie.
 
Huwaga napata wakati mgumu kuhukumu story za upande mmoja......kila mmoja ana play victim......tunataka tusikie na upande wa pili......

Niliwahi kuletewa kesi kama hii na binti mmoja na nikawa mkali mpaka nikampeleka yule kijana police na ustawi wa jamii.....mpaka siku nilipooneshwa picha na video chafu za huyo mwanamke akifanya mapenzi na kijana mwingine.......tangu hapo nikawa makini na vilio vya wakina mama mpaka nisikie upande wa pili.......

NB;
Panapo fuka moshi, kuna moto chini.......
 
Ila huyo jamaa ni mjinga sana asee. Hata kama angekuwa hajaajiriwa mtoto wake anashindwa jichanga hata vi buku tano tano vya hapa na pale yani anapita neutral karibu miaka miwili?


Huyo kama hatumii bange basi yake ina loose connection, maana angekuwa timamu kwanza ujasiri wa kupiga simu na kuomba hela asingekuwa nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…