Hatoi matumizi ya mtoto, kaomba nimkopeshe pesa

Me siamini vipimo vya DNA bongo, hata kama mtoto sio wako watakuambia ni wako ili mtoto asikose malezi
 
lady Jay unaona wenye uzoefu! Mtoto wa Kike na baba yake, we acha tu. Mimi Nina mtoto wa kiume ambaye tangu alipozaliwa nilimweleza mama yake kuwa kazi yako imeisha. Nikasema hata akimnunulia pipi anidai nitarejesha. Sasa yupo form six lakini naona uhusiano wangu naye si mzuri kihivyo sababu ya sumu ya mama pamoja na kumsomesha Feza boys. Siku moja alinitamkia kuwa sikutenda haki kutoishi na mama yake! Imagine (usisahau mama yake alikuwa mchepuko). Maisha haya yaone tu
 
Me siamini vipimo vya DNA bongo, hata kama mtoto sio wako watakuambia ni wako ili mtoto asikose malezi
Ushawahi kupima DNA? Eti mtoto asikose matumizi, kwa hiyo unadhani kila DNA ni positive ili watu wabambikiziwe watoto wasiyo wao.?..Anyway huyu mwenyewe ilitoka positive na matumizi hatoi.Na mtoto kamfanana kuanzia yeye(baba) ,mamake(bibi),na dadake(shangazi)
 
Mkuu, nilishafanya juhudi zote..Ila mambo yanabadilika.Mtoto kadri anavyokua anaona mamake anavyo hustle kwa ajili yake halafu leo hii mtu anajileta in the name of father daughter bond..No way, Mbona mimi hiyo father daughter bond sina na babangu cuz niliona my mum alivyokuwa anahustle.

Nakuelewa mkuu, nilihangaika na mimba alone, nikazaa kwa uchungu nikamtaarifu jamaa hakusema pole wala hongera, nikamlea mtoto mpaka 3 months ndo tukafanya DNA , matumizi katoa kdgo as if siyo jukumu lake baadae akasitisha, Imagine yeye hapo maisha yake yanamwendea tu halafu leo hii eti kuna father daughter bond.From where?

Hapa naomba Mungu nipate mtu anaejielewa tutengeneze familia ili mtoto wangu apate familia kamilifu na father figure .Hiyo father daughter bond itatengenezwa hapohapo cuz mtoto bado mdgo..Yule asiyejitambua atakua anahangaika na laana zake
 
Pole mkuu ila mtoto akikua atajitambua cuz ulifanya jukumu lako
 
Pole mkuu ila mtoto akikua atajitambua cuz ulifanya jukumu lako
Not at all, mtoto wa kiume ni wa mama na mama akimlisha sumu haitoki hata kwa maziwa ya ngamia. Nishaona matendo na msimamo wa kijana. Alikweleza kaka yake kuwa hanipendi kwa vile sisaidii mdogo wake (mtoto wa mama mdogo wake) imagine na kuwa siishi na mama yake. Huyo kaka yake ni wa mke wangu wa ndoa.

Tunawajibika kwa watoto wa kiume kwa vile ni sisi tuliowaleta duniani kwa raha zetu maana wao hawakuomba tuwalete. Lakini kujitambua mpaka aanze kula k na ayaone yenu ndipo atajua ukweli. Wakati huo hatupo duniani.
 
I believe in jasho la mtu haliendi bure mkuu.Just be accountable kuhusu reward mwachie Mungu atajirudi. Kama ni kumlisha sumu tu basi wangu nitamlisha sumu pia dhidi ya babake japo siyo busara.Ila I always believe in being a good person and the world will adjust .
 
nakpongeza sana...ila muwafundishe na wadogo zenu wa KIKE...hakuna mimba ya bahati mbaya....mnajua mnachokifanya.....sio kila mwanaume yuko tayari kulea mimba mpaka mtoto.....mnapaswa kujadiliana....KINGA si zipo.....
 
Huenda mimba ilipatikana kwa bahati mbaya, hamkupanga kupata mtoto japo mlikuwa kwenye mahusiano.

Kitendo cha kupima DNA kinamaanisha kulikuwa na shida mahala.

Hapo uliposema hutaki mazoea na mtu asiejielewa panazidi kuongeza utata kwenye maandishi yako.

Ila hongera kwa kusimamia malezi ya mwanao kwa ujasiri mkubwa, maana kuzaa na mwanamke wa aina yako mpaka mtoto akafikisha miaka miwili bila kupelekwa ustawi wa jamii kwa issue ya malezi ni jambo la bahati sana, ukizingatia Mzee baba anafanyakazi taasisi nyeti.
 
Chai tupu hii.
 
Mungu baba awabariki sana kina mama wote wanaolea watoto wao bila usaidizi wa baba zao..!!
Wakina baba wanaolea watoto bila usaidizi wa mama zao wao hawahitaji hizo baraka za Mungu!!??
 
Huyo asikupe stress mimi natunza watoto kwa kila kitu,mama zao wapambabe n hali zao
 
Akipatikana baba wa mtoto atakuwa na story yake pia
 
Akipatikana baba wa mtoto atakuwa na story yake pia
Of course hakuna baba anamsusa mtoto bila kuwa na hasira za masahibu ya mama yake na mtoto. Kwa bahati mbaya wanaume wengi hususa watoto kutokana na masahibu wanayoyapata toka kwa mama . Ingawa kwa mwanaume anayejitammbua lazima utofautishe mahusiano yako na mtoto au yako na mama yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…