Hatua na maandalizi muhimu ya kujenga nyumba

Kuweka tiles ukutani ni big no kwangu.
Halafu mkuu mimi kitu nachopenda kiwe quality ni tiles za sakafuni na ukutani. Kitchen iwe na kabati quality ambazo ni flat zísiwe na maurembo. Gypsum iwe ya kawaida isiwe na urembo mwingi. Mimi napenda vitu vyenye flat surface.
 
Gypsum tumia ya Thailand nadhani ndio ya bei. Hizi nyingine za bei chee huwa zinatoa unga ambao lazima mna uvuta na unaingia kwenye mapafu. Which is very bad for health. .

Pia kuna mtu alinambia aliweka tiles za wapi basi mke wake akawa anapasi nguo na tandiko kwa sakafu. Zile tiles zilifumuka kama kichuguu halafu zikawa zinalia kama bomb nyumba nzima halafu walivyo wajinga wanafikiri wamelogwa kwa sababu ya kujenga🤣 kumbe tiles sizo.

Remba kidogo tena hapo juu nyumba ivutie 😀
 
Eti wamerogwa... Nyumba ya kwanza nilizingua ramani alikuja nayo fundi ina makosa kibao.
Mimi napenda vitu kama hivi.
 
See through bathroom ili ukioga uonekane🤣😀

Ila mazingira ya geti nimeyaelewa sana yanavutia ila kiswahili swhili watachungulia sana ndani 😀

bedroom imetulia sana napenda hii system ya kuweka kitanda kati. Haya maisha ya mwafrica yan unalala na vitu kibao kila siku vinaongezeka. .
 
Aisee vitu vitam hivi,
Unataka kunambia Ni lazima viwepo tangu wakati wa kuchora ramani au unaweza fanya muda wa finishing tu?
Vingine tunaibuka mavyo mbeleni... Ila vyumba vya watoto nmevizingatia mapema
 
We imekugharimu kiasi gani Hadi kuisha
Haijaisha mkuu ndo kwanza nmeianza mwishoni mwa feb halafu naijenga bila stress. Nilianza nikamwaga tofali 1200 na mchanga trip 2 na kokoto trip moja na nondo 34 na cement 30. Hivyo nlikuwa nanunua kimoja kimoja tu maana sitak jenga kwa stress sina haraka ila lengo kufika mwez wa 8 niwe nimeezeka. Fundi akaja akachimba msingi akaanza jenga msingi akafunga mkanda. Nikamwaga tena tofali 1400 fundi anainua ila mpaka kukamilisha pagala bado tofali 1400 nyingine. Nmeandika ila sijapga hesabu kamili
 
Ujenzi unategemea namna kiwanja kilivyo, ukubwa wa nyumba na ramani. Mfano kiwanja kilocho sehemu yenye mwinuko au yenye udongo unaotuamisha maji itakugharimu zaidi kuliko sehemu tambarare na yenye udongo usiohifadhi maji.

Pia kona kona za nyumba zinakula material. Idadi ya partition za ndani pia ina gharama zake tofauti na ukiweka open space au joined space kwa sebule, kitchen na dining room.

Self contained bedrooms pia zitacost more kuliko shared washroom na master moja. Aina ya paa na urefu wake pia utaleta additional costs. Ramani ya nyumba ni lazima uwe nayo ili ipitishwe na mamlaka husika.
 
Kwani mkuu unataka kujenga nyumba inayofanana na wazee wetu zamani?
 

Mambo mazuri sana haya mkuu Nafaka . Huo muonekano master ya kwanza ni very attractive, space ya kutosha kabisa. Hivi kutengeneza master bedroom ya taswira hiyo ni too expensive? ama inawezekana tu na kwasie wa kipato cha kati? Napenda Sana master bedroom yenye space kubwa na mpangilio wa kisasa, na sebule kubwa.
 
Kokoto na mchanga vinapatikana wapi kwa hapa dar?
 
Naomba kufahamu utofauti wa hizi sehemu kwenye nyumba:

  • Lounge
  • Living room
  • Sitting room

au ni the same thing?

Nafaka , Gily
 
Naomba kufahamu utofauti wa hizi sehemu kwenye nyumba:

  • Lounge
  • Living room
  • Sitting room

au ni the same thing?

Nafaka , Gily
Nyumba chache sana zina Lounge hapa bongo😀

living room nadhani ni sehemu ya sebule but unaweza weka vitanda watu wakalala. Mfano ukaweka zile sofa zinageuka kitanda

sitting room no sebule tu ya kawaida ina TV watu wanakaa kujumuika pamoja

Lounge nadhani ni sehemu ya nyumba haina mkusanyiko wa watu wala kelele
unakuta mtu amekaa Lounge ametulia anatafakari maisha😀
 

Shukrani mkuu
 
View attachment 2547359
View attachment 2547360
Nahitaji nyumba Kama hii
Ramani nimeitoa tu sehemu Ila kitu Kama hiki ndo kipo kichwani mwangu

Vyumba 3 masters,library,jiko, dining,sebule,choo,store
yaani gharama ya nyumba inategemea ukubwa wa eneo unalojenga: mfano jumla ya square meter ngapi ndiyo zitahusisha ujenzi wenyewe.

Nikupe mfano: nyumba yangu ina vyumba vitatu tu lakini eneo jumla ni square meter 220 (living room kubwa, jiko kubwa, dining na MB vyote vikubwa, plus vile vyumba viwili kila kimoja ni ni 4.5 x 4.5 sq meters.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…