Hatua nzuri kwao tecno phantom v fold & galaxy z fold 4 wanachuana vikali samsung wapunguze bei tu

Infinix wanahusikajeee hapa?
 
Shida ipo hapo kwenye chipset,wachane na hizo mediarek zao warasonga
 
Mediatek Dimensity ni Chip bora sana sio kama mediatek za nyuma
Dimensity ni Bora ila Tecno hupenda vitonga, wakitoa vitu vyao lazima uone kasoro kama hizo Dimensity 9000 ni Flagship soc ya Mwaka jana wao wanatoa simu 2023 tena ina bei Milioni 3 kwanini utumie Processor ambayo ishapitwa na wakati?

Fananisha hii simu na michina wengine utaona inapitwa Bei, specs etc, Hata simu kama Oppo ambazo zinauza vitu bei ghali Fold zao zina value kushinda hii.
 
Infinix wanahusikajeee hapa?
Infinix, Tecno na itel ni brand tatu tofauti za simu zinazomilikiwa na kampuni moja ya Kichina "Transsion"
Kwa hiyo hapo jamaa amezilist brand zote tatu zinazomilikiwa na kampuni ya Transsion so hawezi kununua simu kutoka kampuni hiyo including Infinix
 
Ikibadilishwa jina itauzwa na kuwa branded kuliko Samsung au kwenda sawa

Ila kwa jina hilo la Tecno haitoboi, hata ziwekwe features za time travelling bado raia wataikataa
Hivyo ilivyo ikipewa jina la samsung fold v itauza kama chips kuku 🤣🤣🤣
 
Naamini na hii Tecno itaweza kutumika kuchemsha maji...

Maana Tecno za kawaida sio kwa kuchemsha betri vile kama pasi
 
Huwezi kulinganisha sumsung na hicho kitu dunia ya leo bado unatumia prosesa za mediatek tena kwa dolla 1000 hawapo siliazi kabisa
 
Zimefanana specs kweli ila kwenye duarability ndio tatizo ukija baada ya mwaka hiyo samsung kama mtu ni mtunzaji utaikuta kama ilivyo ila nenda kwa tekno sasa utakuta ishachoka vitu kibao.
Uwongo. Kila kitu matunzo. Sio automatic!
 
Uwongo. Kila kitu matunzo. Sio automatic!
Mtu mwenye simu A ameangusha simu yake kwa bahati mbaya kutoka kwenye jengo lake lenye urefu wa mita sita
Mtu mwenye simu B ameangusha simu yake kwa bahati mbaya kutoka kwenye jengo lake lenye urefu wa mita sita pia
Simu A ilipasuka kioo vibaya na ikagoma kuwaka tena pia ilitengeneza ufa kwenye kamera
Simu B ilitengeneza ufa kwenye kioo lakini kamera haikupata madhara na simu iliendelea kufanya kazi kama kawaida.
Kwa mfano huo, je shida ni matunzo?
 
Hapo kuna factors nyingi pia zinahusika. Simu iliyoangukia mgongo haiwezi kuumia kama iliyoangukia uso
 
Kioo chake wameweka nits kidogo ndo maama ni ngumu kutumia kwenye direct sunlight
 
Hapo kuna factors nyingi pia zinahusika. Simu iliyoangukia mgongo haiwezi kuumia kama iliyoangukia uso
Unaposhindanisha durability ya devices tofauti, then all factors should remain constant then utapata fair results
Anyway, you can complicate it the way you want but the point is "durability ni muhimu katika simu na unajua kabisa durability ya devices hutofautiana"
We're gonna choose the more durable product over the less durable ones. End of story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…