Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Somo kuhusu kuchagua njia za kutengeneza fedha kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo ni somo muhimu sana kwa yeyote anayewekeza kwenye uwekezaji huu.
Rafiki yangu ukianza vibaya kuwekeza kwenye ardhi na majengo utashindwa kukuza uwekezaji wako kwa haraka kwa kutumia viwanja na majengo uliyowekeza.
Ili uweze kutumia uwekezaji wako wa mwanzo kukuza zaidi uwekezaji wako unatakiwa kuzingatia maelekezo ya somo hili.
Somo hili ni kwa watu ambao wamechagua uwekezaji kwenye ardhi na majengo kama njia yao kuu ya kujenga utajiri wao.
Kwa watu ambao wanatafuta uwekezaji na biashara inayowafaa kwa ajili kujenga utajiri wao, somo hili linaweza lisipe mwanga wa kutosha.
Somo hili linamlenga mtu ambaye ameamua kujenga utajiri wake kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Njia zote za kutengeneza fedha kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili (2). Sehemu hizo ni kama ifuatavyo;-
✓ Njia za kuwekeza moja kwa moja kwenye ardhi na majengo.
✓ Njia za kuwekeza kwenye huduma zinazohusiana na uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Njia zote mbili (2) unaweza kuanza kuwekeza kwa kutumia kiasi kidogo cha mtaji fedha.
Njia Nne (4) Za Kufahamu Njia Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo.
Kuna zaidi ya njia 100 za kutengeneza fedha kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo. Njia hizo zina faida na chanagamoto zake kwa kila njia.
Moja.
Makala Za Brandon Turner.
Mwandishi na mshauri mbobezi kwenye ardhi na majengo ambaye ameeleza njia nyingi za kutengeneza fedha kupitia uwekezaji huu.
Kupitia mtandao wake na timu yake uitwao BIGGERPOCKETS unaweza kujifunza njia tofauti tofauti za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.
Mbili.
Vitabu Vya Lugha Ya Kiingereza.
Kitabu ambacho kimeeleza njia nyingi za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo ni kama ifuatavyo;-
✓ How to buy and sell real estate for financial freedom (Jinsi ya kununua na kuuza ardhi na majengo kwa uhuru wa kifedha na James Dicks na JW Dicks. Kitabu hiki nitakutumia bure ukikihitaji.
✓ 5 Magic paths to making a fortune in real estate by James E.A Lumley (Njia 5 za kimaajabu za kupata bahati kwenye ardhi na majengo na James Lumley). Kitabu hiki unaweza kukipata kutoka kwangu bila malipo yoyote.
Tatu.
Kitabu cha kiswahili cha ardhi na majengo.
Kitabu changu kiitwacho NJIA 120 ZA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE ARDHI NA MAJENGO kimeeleza njia zaidi ya 100 za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo. Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa nakala tete kinauzwa tshs 6,000/= (elfu sita tu).
Nne.
Kuwa Mwanachama Wa Kundi La UWEKEZAJI MAJENGO.
Hili ni kundi ambalo kila siku utajifunza kuhusu mbinu za uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Kupitia kundi hili unaweza kuuliza maswali kuhusu njia nyingi za kutengeneza fedha kwa kuwekeza kwenye ardhi na majengo.
Kwenye kundi hili unaweza kunishirikisha chochote na nikakushirikisha njia zote zilizoandikwa kwenye kitabu changu.
Poa, wanachama wa kundi hili ndio wana sifa za kupata ushauri moja kwa moja kutoka kwangu kupitia njia mbalimbali isipokuwa njia ya kukutana ana kwa ana.
Ada ya ushauri wa kukutana ana kwa ana sio sehemu ya ada ya uanachama wa kundi la UWEKEZAJI MAJENGO.
Hatua Tano (5) Za Kuchagua Njia Sahihi Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo.
Moja.
Andika Orodha Ya Kila Ulichonacho.
Hapa unatakiwa kuandika orodha ya vitu vifuatavyo;-
✓ Uaminifu wako. Huu hupimwa kwa idadi ya watu ambao wanakuamini mpaka kukupatia mtaji fedha. Pia, idadi ya watu wanaoweza kukudhamimi mbele za wengine.
✓ Akiba ya mtaji fedha ulionao. Kiasi cha akiba ulinacho kinaweza kuamua njia sahihi kwako ya kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.
✓ Uzoefu na ujuzi wako. Ufundi nyumba, ufundi wa kukarabati nyumba, maarifa sahihi ya sheria za umiliki wa ardhi na nyumba, maarifa sahihi ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo, na kadhalika.
✓ Mtandao wa watu ulionao. Hapa ni lile kundi linalokuamini na linaweza kuamini mipango yao. Kundi hili linaweza kugeuka kuwa wawekezaji wenza kwenye ardhi na majengo.
Mtandao wako unaweza kutumika kupata mtaji fedha kwa njia tofauti tofauti kulingana na ukubwa wa mtandao wa watu wako na uwezo wao wa kifedha na uwezo wao wa ushawishi.
✓ Muda ulionao. Kama una muda wa kutosha, kuna njia ambazo zinaweza kukufaa sana ikiwa ni pamoja na kutoa huduma zinazohusiana na uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Mfano; kama umeajiriwa au umejiajiri na hauna muda wa zaidi ya masaa mawili kila siku, nyumba za kupangisha zinakufaa sana.
✓ Taaluma yako. Je una shahada yoyote unayoweza kuitumia kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo?.
Kama una vyeti vya taaluma yoyote unayoweza kuitumia kuwekeza kwenye ardhi na majengo hakikisha unachagua njia ya kuanza kutengeneza fedha kulingana na taaluma yako.
✓ Vifaa na vyombo vya uwezeshaji. Hapa hujumuisha simu janja (smartphone) au kompyuta. Vifaa hivi vinaweza kutumika kuchagua njia ya kuanza kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.
Hii ni kwa sababu vifaa hivi vitakuwa ni nyenzo muhimu kwa ajili ya njia utakayoamua kuwekeza kwayo.
Mbili.
Jifunze Njia Zote Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo.
Rejea vyanzo vinne (4) unavyoweza kupata maarifa sahihi kuhusu njia sahihi za kutengeneza fedha kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Njia hizo ni vitabu vya kiingereza, kitabu changu cha kiswahili, makala za Brandon Turner (kupitia mtandao wake wa BIGGERPOCKETS na kupitia kundi langu la UWEKEZAJI MAJENGO.
Tatu.
Chagua Njia Tano (5) Tu.
Chagua njia tano tu ambazo umezielewa na unaamini unaweza kujenga mafanikio makubwa kupitia njia hizo kulingana na hali ulinayo.
Njia unayoipenda lakini huna uwezo nayo kwa sasa kulingana na orodha yako ya hapo juu achana nayo. Iandike pembeni njia hiyo kwa ajili ya kuitumia miaka ijayo ya uwekezaji wako.
Nne.
Chagua Njia Tatu (3) Tu.
Chagua njia tatu kutoka kwenye orodha ya njia tano za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo ulizo orodhesha hapo kwenye hatua ya tatu.
Katika njia hizi tatu, anza na njia moja tu mpaka njia hiyo iweze kuanza kuingiza kipato endelevu au faida kwa ajili ya kukuza uwekezaji wako.
Unatakiwa kuendelea kujifunza kwa undani zaidi kuhusu njia hizi siku hadi siku. Hii itaongeza imani kubwa kwenye akili yako. Kwa kuwa imani huja kwa kusikia, huwezi kuwa na imani na kitu ambacho hukifahamu vizuri.
Ili imani iwe imara zaidi kwenye njia ulizochagua ni lazima uendelee kujifunza kuhusu njia hizo za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.
Mfano wa njia nilizochagua mimi ni kama ifuatavyo;-
✓ Kutoa mikopo ya ukarabati na maboresho ya majengo.
✓ Kununua ekari za ardhi, kuendeleza na kuuza vipande vidogovidogo.
✓ Kumiliki nyumba za kupangisha zenye kuingiza kipato endelevu na kipato chanya.
Kutoka kwenye mfano huu, sitakiwi kuanza kutamani njia nyingine wakati ninaanza au ninaendelea kuwekeza. Kwa njia hizi tatu (3) inawezekana kabisa kujenga utajiri mkubwa sana bila kuhangaika na njia nyingi zaidi ya 100 zinazobaki.
Tano.
Rudia Hatua Ya Kwanza Hadi Ya Nne.
Baada ya kukamilisha mradi fulani na unaendelea kuingiza faida au kipato endelevu ni kuwekeza tena faida niliyopata kwa kuzingatia hatua hizi.
Kwenye hatua zote hizi, ni muhimu sana kuwa na menta au kocha mbobezi kwenye ardhi na majengo.
Mimi nipo kwa ajili yako rafiki yangu. Nipigie simu kupitia 0752 413 711 ili tuzungumze chanagamoto ulinayo inayohusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mawasiliano; +255 752 413 711