Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Mama's boys endeleeni kukaa nyumbani tu.
Ukifatilia wanaokomaa home kwa wazazi ni watoto type za mikocheni,masaki,obey yani jibaba ,limama zima linashinda sebureni kungombania remote na watoto ,wa huku uswazi 18 to 21 ushalianzisha
 
Sasa wewe kama familia yenu mnakaa kwenye nyumba ya kupanga mpaka leo utakaeje hapo?acha kuwaonea wivu watoto wa wenzio Wazazi wao waliojipanga na kujenga nyumba ili kuwasitiri watoto wao mpaka pale watakapofanikiwa kimaisha,wewe mlaumu Baba yako wakati wenzie wanasoma yeye alijifanya mjanja kuwa chimbo na kuvuta bangi na kunywa mataputapu.
Wewe watoto wako watajengewa na nani?
 
Hii mada ni nzuli sana lakini kusema ukweli kuna umri na mazingira unafikia inakubidi mtu kuhama nyumbani na kutafuta maisha sehemu nyingine.
 
Kuna wakati unafika ukiwa kama kijana ni lazima ubadilike kiakili na kuanza kujitegemea kwa sababu maisha ya sasa yana leo na kesho.

Hebu fikiria tuu upo kwenu unasikia nyumba yenu imepigwa x ibomolewe.

Pili hebu fikiria siku uko home unasikia nyumba yenu inapigwa mnada na benki inauzwa hapo unakuta mzee wako alikopa benki.

Sasa jiulize hapo utaanzia wapi
 
Siyo kweli.
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
 
Umesema kweli mkuu! Waafrika tuna utamaduni wa kulelewa na kutojitegemea. Wenzetu wazungu mtoto akifika miaka ata 18 anawashwa kuindoka nyumbani ili aanze kujitegemea na atafanya hivyo kwa kufanya kazi ata za uhudumu mahotelini... Na hii sio kwa waliosoma tu.
Tatizo letu tunachagua sana kazi za kufanya. Mtu anajiona ana degree ko anataka kazi za maofisini tu na za kulipwa malaki. Yaani elimu ndo imetuharibu sana akili ndo mana wale ambao hawajasoma ndo wanatajirika zaidi.
Well said brother,.... Yan Elimu ndo imetuletea haya majanga
 
Back
Top Bottom