Hatuhitaji vita vya kikanda na Iran-Waziri Mkuu wa zamani wa Israel

Hatuhitaji vita vya kikanda na Iran-Waziri Mkuu wa zamani wa Israel

Mateso chakubanga

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2021
Posts
587
Reaction score
800
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak amesema Israel ilifanya makosa ya kimahesabu kwa adui zake ,hivyo haoni kuna haja ya kufanya vita na Iran,

na anajua tayari kuna upinzani kutoka Hamas, Hezbolla,Houthis na sasa Iran na itachukua muda mrefu sana katika operesheni zake katika miji ya Rafah, Gaza na West bank,makosa yalifanyika tangu oktoba 7 na April 1 ,hivyo anaona vipaumbele vya serikali viwe:
1.kuachiwa mateka wa israel
2.kusitisha vita.
Chanzo: Channel4news Israel
 
Iran anaweza akapata kiburi endapo watamuacha hivihivi, ni hatari sana kwa mataifa ya magharibi kuangalia tu maslahi yao ya kiuchumi kuliko usalama wa taifa la Israel.
Kwhyo wafanyaje sasa...maslahi ya uchumi yapi??...kuiba mafuta middle east au....Wampe silaha Israel halafu aingie kati wqdundane na hao waajemi tuone nani ni nani....inatakiwa ifikie wakati kila mtu ajue mipaka yqke ni wapi na aishie wapi....dhulma haiwezi kutawala milele maana unaowadhulumu bdo wataendelea kutafuta namna ya kutokudhulumiwa na kuonewa na hapo maugomvi na mavita hayatakaa yaishe
 
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak amesema Israel ilifanya makosa ya kimahesabu kwa adui zake ,hivyo haoni kuna haja ya kufanya vita na Iran,
View attachment 2966459
na anajua tayari kuna upinzani kutoka Hamas, Hezbolla,Houthis na sasa Iran na itachukua muda mrefu sana katika operesheni zake katika miji ya Rafah, Gaza na West bank,makosa yalifanyika tangu oktoba 7 na April 1 ,hivyo anaona vipaumbele vya serikali viwe:
1.kuachiwa mateka wa israel
2.kusitisha vita.
Chanzo: Channel4news Israel
Sisi wayahudi wa Nandagala tunapinga. Hiyo video ni ya mchongo kutoka Iran.
 
Iran anaweza akapata kiburi endapo watamuacha hivihivi, ni hatari sana kwa mataifa ya magharibi kuangalia tu maslahi yao ya kiuchumi kuliko usalama wa taifa la Israel.
Usalama wa Taifa la Israel upo mikononi mwa Israel na sio nchi zingine, akili zao na maamuzi yao ndio yatafanya aidha nchi yao iwe salama ama wapigike
 
Iran anaweza akapata kiburi endapo watamuacha hivihivi, ni hatari sana kwa mataifa ya magharibi kuangalia tu maslahi yao ya kiuchumi kuliko usalama wa taifa la Israel.
Huyo ni waziri mkuu mstaafu, hivyo anafaham vizuri weakness ya taifa lake dhidi ya mwenye nguvu Iran. Kama nchi zaidi ya 7 zimeshindwa kuzuia shambulio la Iran lisifike Israel kwa shambulio 1 tu ambalo tayari Iran ilikuwa ishawapa taarifa ili wajipange kulizuia na wakashindwa, je ikitokea majibizano yakawa ya kuendelea kwa week nzima huku nchi zinazoilinda Israel kuchoka kuilinda hali itakuaje kwa nchi hiyo.

Wewe myahudi wa bonyokwa unataka kujifanya una uchungu na uwezo wa kulipiza kisasi kuliko waziri mkuu mstaafu anaeiona hatari ya nchi hiyo kuangamizwa na makombora mabaya zaidi ya Iran.

Fikiria hata Mmarekani mwenyewe ameonekana kuogopa na kumshauri Netanyahu asithubutu kujibu, nchi yake inaweza kugeuzwa kifusi.
 
Kwa hiyo wanasubiri nini kukafuta?
Iran hakufanya shambulizi la uoga la kushtukiza kama afanyavyo Israel huko Lebanon, Syria nk.

Kwanza kwa kujiamini walitoa taarifa mapema huku wakijua fika taarifa hizo zitawapa nafasi Israel na washirika wake wajipange kulizuia.

Pili baada ya kuona Israel na washirika wake wameshajipanga kuzuia akafungulia bomba ili aone panapovuja. Na kweli ikabainika kuwa vifaa vyao vyote vya kuzuia vinavuja. Maana Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujeruman, Jordan, Saudi Arabia na Israel yenyewe walianza kuzuia kuanzia Iraq, Saudi Arabia, Syria, Jordan nk, lakini mzigo umepita kilometres zaidi ya elf 2000 hadi katika nchi husika.

Sasa jiulize kama Iran isingetoa taarifa au Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Jordan wasingeisaidia kuzuia hali ingekuaje.
 
Kwenda zako! Ndo maana aliondolewa kama sio photo edit basi ni propaganda! Kitu ambacho Israel hawezi kufanya ni kuchokozwa na akakaa kimya! Israel ni taifa la vita miaka yoote! Lilianzishwa kwa vita na linaishi kwa vita! Huwezi kuchokoza Israel ikanyamaza kimya! Israel ni kama Marekani! Mchokoze marekani huone kama atakunyamazia! Kwenye uringo wa kijeshi kuchokozwa ukakaa kimya kunaitwa "coward" yahani "mwoga"

Back
Top Bottom