Sema nini jamani, tukubali tukatae, hatukuja duniani kula bata, hao watoto inabidi wazoee msote toka wakiwa wadogo, wachoshe bongo zao, Elimu ya kuacha watoto wazunguke baada ya likizo na vitu kama hivyo imeonekana imeshindwa kulikomboa taifa letu, refer Viongozi wetu, uzembe makazini kwa wafanyakazi etc,
Heb tutengeneze taifa la watu waliozoeshwa kufanya kazi toka wadogo, watu wanaojua maisha ni mashindano kuwa you have to be number one, kufanya kazi masaa 18 kwa siku, hata kama tunalalamika ila mi nawaambia hii ni kitu kizuri, nendeni Asia muone jinsi watoto wanasoma sana, kutaka watoto waishi maisha soft ya kuamka saa 1 na kurudi home saa 10 bila homeworks wala nini ni kuendelea kuzalisha kizazi cha watu wazembe wasiojua kuhustle kabisa