Hatukatai elimu ni muhimu ila kuwe na kipimo, Watoto shule za msingi masomo yamekuwa mengi, wakirudi home work, likizo tuition, Hii ni mbaya sana!!

Hatukatai elimu ni muhimu ila kuwe na kipimo, Watoto shule za msingi masomo yamekuwa mengi, wakirudi home work, likizo tuition, Hii ni mbaya sana!!

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Mtoto ni kama vile kazaliwa kwajili ya kusoma tu.

Tena siku hizi wameongezewa masomo na muda mwingi wapo shulenj, hawa ni watoto wenye umri mdogo kuliko hata sisi tulipokuwa shuleni, kumbuka siku hizi watoto wengi wanaanza la kwanza wana miaka mitano wanamaliza elimu ya msingi darasa la sita wakiwa na miaka 10

Mtoto hajui hata kufinyanga udongo, yani ni masomo kwa kwenda mbele ama games za computer / simu

Mtoto hapati hata muda wa kufanya chores zake kumfunza majukumu ya ziada kama kumwagilia bustani, kulisha kuku, kusafisha mazingira ya nyumbani, n.k. ni masomo kwa kwenda mbele
 
Likizo ni muda wa wanafunzi kupumzika. Pamoja na kujua stadi nyinginezo za maisha.

Mambo ya masomo ya ziada wakati wa likizo ni kiherehere cha wazazi.

Masomo si mengi. Kwa shule ya msingi ni masomo sita (nipo tayari kusahihishwa). Kwa Sekondari, wapo wanaosoma 7 au 9.

Hata hivyo, mfumo unabadilishwa. Huenda ikaleta ahueni.
 
Walimu hawawapi watoto maarifa, walimu wanawachosha watoto ili wafaulu, na mwalimu apate ujiko.

Ni aibu sana kuandika kwenye school 🚸 bus mshindi wa kwanza kimkoa.

Elimu imekuwa biashara, pumbavu kabisa
 
Ndo maana nawaambiaga kila siku hapa mpelekeni watoto wenu shule za Kayumba huko hakuna mambo hayo
 
Sema nini jamani, tukubali tukatae, hatukuja duniani kula bata, hao watoto inabidi wazoee msote toka wakiwa wadogo, wachoshe bongo zao, Elimu ya kuacha watoto wazunguke baada ya likizo na vitu kama hivyo imeonekana imeshindwa kulikomboa taifa letu, refer Viongozi wetu, uzembe makazini kwa wafanyakazi etc,

Heb tutengeneze taifa la watu waliozoeshwa kufanya kazi toka wadogo, watu wanaojua maisha ni mashindano kuwa you have to be number one, kufanya kazi masaa 18 kwa siku, hata kama tunalalamika ila mi nawaambia hii ni kitu kizuri, nendeni Asia muone jinsi watoto wanasoma sana, kutaka watoto waishi maisha soft ya kuamka saa 1 na kurudi home saa 10 bila homeworks wala nini ni kuendelea kuzalisha kizazi cha watu wazembe wasiojua kuhustle kabisa
 
Tanzania has one of the worst education systems in the world.
 
Back
Top Bottom