kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Wakazi wa Kijiji cha Ilela, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe waliokuwa wanakabiliwa na kero ya maji safi na salama wameondokana na adha hiyo baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu kuwapelekea mradi wa maji ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani.
Mradi huo umekamilika kwa 100% utawanufaisha wakazi 980 wa kijiji hicho ambao hawajawahi kupata maji ya bomba tangu uhuru walikua wanatumia maji ya ziwa Nyasa ambayo wanayafata kilometa moja. Diwani wa kata ya Ruhuhu, Athanas Haule alisema mradi huo wa maji ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji hicho hasa wakati wa kiangazi kwa kuwa wakati wa masika wananchi wanatumia maji yanayotiririka kutoka milimani.