Hatumfundishi kazi Rais bali tunamshauri kuhusu vitengo hivi viende wizara husika

Hatumfundishi kazi Rais bali tunamshauri kuhusu vitengo hivi viende wizara husika

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Umofia kwenu wana Great Thinkers.

Nilianzisha uzi huu uitwao Rais Samia hii wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ina ukakasi kidogo. ambapo pamoja na mambo mengine nimeona kutenganisha uzi huo na huu ninaouweka hapa hasa kuishauri serikali kwenye masuala ya kimuundo na siyo kisera.

Tunafahamu kuna thread inayotrend inayotutaka wanagenzi wa masuala ya siasa na maendeleo kuishauri serikali, lakini hapa ninaweza uzi unaohusu kuishauri serikali hasa kwenye maeneo ya kimuundo na utawala.

Tunafahamu pia kwamba, serikali hususani ofisi ya Rais wapo wataalam mbalimbali wabobezi katika masuala nyeti ya nchi mpaka eneo muhimu la utawala. Lakini haiwatoi kwenye ulingo kwamba wao si wanadamu kama sisi tunaosaka tonge kupitia umachinga na gombania goli.

Kuna vitengo vingi vya serikali vinahusika na masuala kadhaa ya kisekta lakini inawezekana idara hizo zipo kwenye eneo ambalo kimuundo linachangoa kuzorota kwake. hivyo kupitia uzi huu tuishauri serikali kuweka muundo wake kiutawala vizuri hasa kupeleka ama kuhamishia idara muhimu kwenye wizara sahihi kwa minajili ya kujenga tija.

Ninaanza na kuishauri serikali kuangalia mgawanyo wa majukumu yaliyopo ndani ya wizara ya TAMISEMI hususani usimamizi wa miundombinu ya shule. Ikumbukwe kuwa miundombinu ina wizara yake na hayo majengo ya shule na vyuo mbalimbali ni mali ya umma chini ya serikali, hivyo miundombinu ya shule zetu ikawekwa Wizara ya miundombinu chini ya wakala wa majengo ya serikali itasaidia ufanisi na kuokoa bajeti kwa sababu TAMISEMI eneo la miundombinu ni wazi lazima watoe kandarasi za wataaluma na wasanifu ili kufanikisha miradi wanayoisimamia. Kule Wizara ya Ujenzi na Miundombinu wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa

Serikali irejeshe jukumu la elimu na kupanga madaraja kwenye Wizara mama ya elimu, inachoweza kufanya ni kuimarisha eneo la upangaji wa madaraja na kuanzisha idara kamili ya Mitaala ambayo kazi yake kubwa itakuwa kufuatilia ufanisi, maoni na uandaaji wa mitaala na kupitia mitaala yote inayotumika nchini kwa kuifanyia verification ya ubora wake.

TAMISEMI
iongezewe jukumu la msingi la ustawishaji demokrasia kupitia idara za tawala za mikoa hususanani mgawanyo wa madaraka kuanzia mitaa, vijiji, vitongoji, Kata na tarafa. Umuhimu wa hili ni kurudisha madaraka kwa wananchi kivitendo zaidi. kusimamia ratiba za mikutano ya wananchi, kuhakiki masuala mazima ya O&OD kutoka kwenye ngazi za vihihi na mitaa.

Mambo ya Ndani
Kitengo cha Mgambo kiwekwe ndani ya wizara hii badala kuacha kusimamiwa na kamati za ulinzi na usalama pekee. Hii itawasaidia wananchi kuelewa uwajibikaji wa jeshi hili la mgambo ambalo kimsingi haijulikani lipo chini ya wizara gani

MAENDELEO YA JAMII
Hii idara ama kitengo kinahusu Wizara ya Fedha, itakuwa ni tija kubwa Wizara ya Fedha ikasimamia maendeleo ya jamii kwa sababu tunaposema maendeleo ni kugusa mianya ya uchumi kwa sehemu kubwa.

Tuendelee kuishauri serikali kimuundo
 
Hongera .
Washauri wa Rais kazi kwenu maoni mujarabu haya.
Lakini hapo kwenye maendeleo ya jamii kidogo si sawa
 
Umeandika mambo ya jumla jumla sana hata hayaeleweki.

Hebu jaribu kufafanua Kama ifuatavyo:

  • Muundo wa Sasa ukoje
  • Una mapungufu gani
  • Kwanini
  • Uboreshwe vipi, na kwa kufanya vipi?

======
Mfano, Mimi ukiniuliza Maboresho TAMISEMI nitapendekeza yafutayo:

- Vyeo vya DC, RC na ofisi zao vifutwe, badala yake Wakurugenzi wapewe nguvu. DED apewe Mamlaka ya ulinzi na Usalama.

- DED wapewe watu ambao ni veteran kiutumishi, siyo kimtu kinaokotwa tu Lumumba au chawa fulani Kwasababu anaonekana kwenye TV hajawahi kufanya kazi za utumishi wa umma anapelekwa kwenda kusimamia watumishi waliofanya kazi miaka 30.

- Wakuu wa idara wapewe nguvu ili kumsaidia DED kikamilifu.

- Kama ilivyo kwenye mashirika, Halmashauri zipewe nguvu ya maamuzi katika kistawisha maisha ya watumishi wake. Watumishi wanapambania kukusanya mapato, lakini yanaishia kulipa posho madiwani, DED na Wakuu wa idara na watumishi wengine hata nauli tu ya likizo iliyopo kisheria hawapati.

- Masuala ya kitaaluma yabaki kwa wahusika, mambo ya Wakuu wa shule Mara madaktari kusimamia Ujenzi ni upumbavu.
 
Ni maoni ya mleta uzi, lakini kwenye usimamizi wa miundombinu ya shule siafiki majengo hayo kupelekwa Wizara ya Miundombinu, inaonekana mtoa mada sio muumini wa ugatuaji wa madaraka kwenda Ngazi za chini, inangalie hiyo wizara ya miundombinu ina manpower kubwa kiasi gani kuweza kumudu majengo ya shule zote nchini
 
Umeandika mambo ya jumla jumla sana hata hayaeleweki.

Hebu jaribu kufafanua Kama ifuatavyo:

  • Muundo wa Sasa ukoje
  • Una mapungufu gani
  • Kwanini
  • Uboreshwe vipi, na kwa kufanya vipi?

======
Mfano, Mimi ukiniuliza Maboresho TAMISEMI nitapendekeza yafutayo:

- Vyeo vya DC, RC na ofisi zao vifutwe, badala yake Wakurugenzi wapewe nguvu. DED apewe Mamlaka ya ulinzi na Usalama.

- DED wapewe watu ambao ni veteran kiutumishi, siyo kimtu kinaokotwa tu Lumumba au chawa fulani Kwasababu anaonekana kwenye TV hajawahi kufanya kazi za utumishi wa umma anapelekwa kwenda kusimamia watumishi waliofanya kazi miaka 30.

- Wakuu wa idara wapewe nguvu ili kumsaidia DED kikamilifu.

- Kama ilivyo kwenye mashirika, Halmashauri zipewe nguvu ya maamuzi katika kistawisha maisha ya watumishi wake. Watumishi wanapambania kukusanya mapato, lakini yanaishia kulipa posho madiwani, DED na Wakuu wa idara na watumishi wengine hata nauli tu ya likizo iliyopo kisheria hawapati.

- Masuala ya kitaaluma yabaki kwa wahusika, mambo ya Wakuu wa shule Mara madaktari kusimamia Ujenzi ni upumbavu.
Uko sahihi sana japo kwenye DC, RC ni ngumu sana ccm kukubaliana na Hilo jambo.
Suala la DED ni kweli, hii position inahitaji mtu msomi na mzoefu lakini sio ilimradi kuokota mtu.
Hapo kwa madiwani umegonga penyewe kabisa. Watumishi waliopo front kabisa kwenye kukusanya mapato, DED yupo radhi kabisa kuchelewesha dokezo lao kuliko kuchelewesha dokezo la madiwani.
Suala la madaktari na walimu wakuu kusimamia ujenzi haliepukiki kwa hali nayoiona kwenye haashauri zetu. Manpower ni ndogo sana kwenye kitengo cha ujenzi kuweza kuratibu shughuli nzima ya ujenzi. Kikubwa kuwe na ukaribu kati ya wasimamizi na injinia
 
Back
Top Bottom