Hatuoni tatizo kwa miradi ya Serikali kutokana na mawazo ya wawekezaji wa kigeni?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ngoja na mimi leo nibwabwaje. Hili jambo nimeanza kuligundua zamani sana. Unakuta mwekezaji au serikali ya nje inakuja na kusema fanyeni hivi na vile tutawapa pesa za huo mradi. Motive ya hao wawekezaji ni ROI yao kwanza, wanazo pesa zimezagaazagaa wanazunguka dunia nzima kutafuta pa kuzizungusha ili zisikae bure. Hatuzingatii hilo.

Unakuta sisi hatukuwa hata na mpango na project ya namna hiyo ila kwa kuwa tunaona kuna pesa za bure, tunavuruga mipango yetu tunadakia mawazo hayo. Inaonyesha serikali yetu haiwezi kusema NO pale mtu anapokuja na pesa. Hili ni tatizo kubwa.

Sasa hivi hili tatizo tumelivika joho la PPP, ndiyo mvurugano mwenda mbele.

Kuna mtu aliwahi kuuliza inakuwaje miaka ya hivi karibuni tu tulitumia pesa nyingi saana kupanua bandari halafu ghafla tunamkabidhi mwekezaji bandari yote? Ile pesa ya upanuzi ingeweza kufanya mangapi mengine?

Tunaona pale Jangwani panaenda kujengwa daraja, jambo ambalo limekuwa linaongelewa miaka nenda rudi ila miaka ya karibuni kuna shughuli nyingi za upanuzi ikiwemo kujenga mwendokasi zimefanyika pale bila kuleta matokeo yenye tija. Huu upotevu wa pesa hauwaumi wananchi?

Tunaambiwa Mchina ameshauri kujenga barabara za kulipia ndani ya Dar na tumemkabidhi mradi ila ni miradi kiasi gani ya upanuzi wa barabara imefanyika miaka ya karibuni hapo Dar bila kutatua tatizo la foleni? Nini kinakwamisha hii miradi?

Tumetumia mapesa mengi sana kwenye mradi wa Bwawa la Nyerere, tukaambiwa tatizo la umeme sasa baaasi. Ghafla tunaambiwa tuko mbioni kuruhusu wawekezaji binafsi kwenye sekta ya umeme? Kwa nini hatukuwaruhusu hao wawekezaji kabla ili tuokoe pesa iliyotumia kwenye ujenzi wa bwawa ili wao ndiyo wafanye huo upanuzi wa vyanzo vya umeme? Unamuita mwekezaji wakati tatizo umeshalitatua?

Je miradi ya Serikali inatekelezwa bila kuwa na mipango ya muda mrefu na bila kufanya upembuzi yakunifu au ndiyo tunachukua mipango iliyo katika makabati toka enzi za Nyerere ndiyo tunaitekeleza bila kujali mabadiliko ambayo yameshatokea, matokeo yake inashindwa kuleta matokeo tarajiwa?
 
Kwa hiyo hii mada hamjaiona au ni dharau tu?
 
Ni afadhali jiji la Dar es Salaam lipangwe na Wachina kuliko kupangwa na Wabongo. Hivi unategemea mtu ambaye amezaliwa kwenye nyumba ya tembe aweze kupanga mji? Ukienda China utashangaa kule Shangai au Schenzen, ni kama miji hiyo imeumbwa na Mungu! Lakini angalia hapo Magomeni Mapipa na Buguruni Malapa ndio utajua kwanini tuwape wageni watupangie miji yetu. Kwani sisi ni mji gani tunaweza kujivunia kwamba tumeupanga? Nitajie mmoja tu.
 
Sahihi kabisa, tunatoa watu vijijini waje walete maendeleo na kuwasimamia watu wa mjini.

Ila kama tunaamua kuwakabidhi wageni basi twende all the way, siyo tunazungukazunguka halafu baada ya kupoteza saana pesa na muda kwa miradi uchwara ndiyo tunawakabidhi wageni tena kutatua sehemu tu ya tatizo.
 
Back
Top Bottom