The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Siku chache baada ya kutoa ushahidi wake mbele ya Kitengo cha Uhalifu Dhidi ya Binadamu katika Mahakama Kuu ya Paris, familia ya Bongo inaendelea kusisitisha madhila na mateso waliyoyapata kutoka serikali ya Gabon. Katika taarifa ndefu iliyotolewa siku ya Alhamisi, Julai 3, Sylvia na Noureddin Bongo wanasisitiza mateso walioyapata kutoka kwa mamlaka ya Gabon kwa. Wanasema kuwa walijumuisha kwenye faili la malalamiko yao yaliyowasilishwa nchini Ufaransa mnamo Mei 2024 na familia nzima (Rais wa zamani Ali na watoto wawili wa kiume wa mwisho, Jalil na Bilal) kwa "utekaji nyara, kuwekwa kizuizini kiholela, vitendo vya utesaji na ukatili," video zinazothibitisha unyanyasaji waliopata, pamoja na shinikizo la jeshi kuwatia hatiani.
Wakati mamlaka ya Gabon ilikuwa na matumaini kwamba kuiondoa familia ya Bongo na kuipeleka nchini Angola katikati ya mwezi Mei, ingesalia kimya na kutoeleza kilichotokea, lazima wakubali mamlaka hiyo inaona kwamba familia ya rais wa zamani imeamua kutoweka kutokaa kimya. "Hatutanyamaza," wanaandika Sylvia na Noureddin Bongo, kuhusiana na unyanyasaji dhidi yao katika gereza kuu la Libreville na kisha katika sehemu ya chini ya ikulu ya rais, "ghorofa sita chini ya vyumba vya rais," kwa kipindi chote cha miezi 20 wakizuiliwa.
Katika kuunga mkono hili, wanaambatanisha na malalamiko yao video iliyorekodiwa kwa siri mnamo Februari 28, 2025, na Noureddin Bongo katika chumba cha jaji wa uchunguzi wa Gabon aliyesimamia kesi hiyo. Video inaonyesha jaji, mtoto wa rais wa zamani, na wakili wake, Eyue Bekale, wakiwa na mazungumzo yasiyo rasmi kuhusu kesi hiyo. Mtu mwingine, anayeketi kwenye kompyuta, yaelekea ni msaidizi au karani wa mahakama, anakaa kimya. Noureddin Bongo analalamikia kutendewa vibaya na hatua za kiholela dhidi yake, na kuonyesha kuwa kesi hiyo inahusishwa na msuala ya siasa. "Ulitakiwa mzingatiye hili," jaji anasema. Anasema alishinikizwa: "Lazima wahukumiwe," askari walimwambia. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, video nyingine pia zilijumuishwa kwenye jalada la kesi hiyo zinazodaiwa kuwaonyesha wanachama wa CTRI wakikiri vitendo vya utesaji.
Siku chache baada ya kutoa ushahidi mbele ya majaji wawili wa Ufaransa, familia ya Bongo ilishukuru "jumuiya ya kimataifa, hasa Umoja wa Afrika," kwa "kuokoa maisha yao." Wanaishutumu serikali ya Gabon kwa kuandaa "kesi nyingine" hivi karibuni ili kuhalalisha unyakuzi wa mali zao. "Kuchapwa viboko, kupigwa na umeme, kuzamishwa majini, kupigwa na mateso mengi mabaya zaidi. Kati ya vipigo, tulilazimishwa kutia sahihi," wanaandika. "Siku moja kabla ya kuondoka, tulilazimika kutia saini hati zinazotulazimisha kukaa kimya kuhusu mateso tuliyopata. Lakini hatutakaa kimya kutokana na dhuluma hizi."
Baada ya kufukuzwa na kupelekwa Angola katikati ya mwezi wa Mei na kufikia kwenye makazi yao London, mwendesha mashtaka alihakikisha kwamba mashtaka dhidi ya Sylvia na Noureddin Bongo, pamoja na mambo mengine, rushwa, ubadhirifu na kughushi saini ya Rais, bado yako halali, na kwamba kesi itafanyika hata kama hawapo. Rais wa zamani Ali Bongo alikuwa bado hajafunguliwa mashtaka.
Kulingana na vyanzo vya kuaminika, uchunguzi wa Gabon ulihitimisha kuwa Ali Bongo alipokea faranga za CFA bilioni 266 (takriban euro milioni 406) katika uhamisho usio wa kawaida kwenye akaunti yake ya benki kwa muda wa miaka kumi. Ofisi ya mwendesha mashitaka inabaini kwamba majengo ya kifahari na ghorofa kadhaa vilinunuliwa kwa kutumia vifaa vya kijeshi. Pia inachunguza uuzaji haramu wa mafuta na bidhaa zingine, zilizokubaliwa na mamlaka za zamani katikati ya ufisadi.
Ili kukashifu ushuhuda wa Ali Bongo wa "kutengwa" na "kufungiwa" katika makazi yake huko La Sablière baada ya kupinduliwa, maafisa wa Gabon wanaelezea kuwa video zinaonyesha kwamba alisherehekea siku yake ya kuzaliwa huko na wanafamilia, na kwamba alipokea wakuu wa nchi na wageni wengine, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari. Hata hivyo, alikataa mara kwa mara kuondoka nchini.
Kuhusu tuhuma za utesaji, mara zote zimefutiliwa mbali na mamlaka ya Gabon.