Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kupitia falsafa ya 4Rs,
Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ana lenga na anakusudia kuiponya Tanzania kwa majeraha mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kitaifa na kimataifa, na kujenga hali na mazingira ya kuaminiana na kurejesha imana za wanachi zilizotoweka katika kuamini taasisi za Umma.
Na kwahivyo, jitihada za makusudi, dhamira ya dhati na nia yake njema ni kutibu kabisa majeraha yote ya kisiasa, kuliunganisha taifa na waTanzania wote, na zaidi sana kufungua nchi miongni mwa mataifa ya ulimwengu.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA
Katika kipindi kifupi sana cha uongozi wake wa awamu ya sita na kwakupitia serikali sikivu ya CCM, Rais, Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno kuwaleta waTanzania wote pamoja mathalani katika suala la maridhiano limechochea kwa kiasi kikubwa kidemokrasia nchini kuimarika sana, mikutano ya hadhara rukhsa, maandamano rukhsa, ukosowaji kwa Serikali rukhsa, uhuru wa maoni, habari, haki na usawa wa habari na kuabudu, chaguzi huru, sawa na haki n.k
Lakini pia, uwazi na uwajibikaji serikalini ni mkubwa sana, kwamfano sheria za uchaguzi na Tume Huru ya Uchaguzi vimefanyiwa marekebisho mukubwa sana muhimu kwa uwazi sana na kufanya mazingira bora zaidi na ya kuaminika kwa wananchi, kwamba chaguzi zetu hasa zinazokuja.
zinafanyika katika mazingira ya uwazi, usawa na uhuru ili kuondoa manung"uniko na sintifahamu na hujuma za wasiolitakia mema Taifa letu.
sasa katika hali hiyo, anatokea kiongozi muandamizi tena mteule wa Rais eti ng"we ng"we ng"we kuhusu uchaguzi? wateule wa aina hii ni sharti wabanduliwe kwenye nafasi zao maramoja bila maelezo wala ufafanuzi wa kina.
Soma Pia: Kama taifa, zawadi pekee ya kumpa Rais Samia kwa kazi nzuri ya maendeleo ni ushindi wa kishindo uchaguzi mkuu 2025 ikiwa atagombea
Huko ni kumuhujumu Mwenyekiti wa CCM taifa na kuhujumu kwa makusudi dhamira njema na jitihada kubwa sana za Rais Samia Suluhu Hassan kuliunganisha Taifa na kufungua nchi na zaidi sana kuimarisha umoja, amani, utulivu na mshikamano wa waTanzania wote.
Natoa rai kwa watumishi wa Umma kote nchini, kutunza ndimi zao na kuheshimu mamlaka hasa za uteuzi..🐒
Mungu Ibariki Tanzania