Nikukumbushe tu; Tanzania imeanza kuonja mgao wa umeme mwaka 1992, wakati huo rais akiwa ni Ali Hassan Mwinyi, think tank ya wakati huo ikaona iingie mkataba na IPTL, nadhani unajua IPTL ndio iliokuja kuzaa escrow account scandal. Ni miaka hiyo hiyo ndio tulipowauzia Waarabu mbuga ya Loliondo, hadi leo mie binafsi sijawahi kuelewa why tuliuza mbuga ile na baadae watu wakaigeuza kua nchi ndani ya nchi, tabia hiyo hiyo imerudia tena awamu hi. Sina hakika kama walau unaweza kunambia taifa linapata faida gani kwa hatua hizo.
Mashirika mengi ya umma yalianza kuporomoka kibiashara, wizi, ufisadi kwenye mashirika hayo ulikua mkubwa mno, nyakati zile wafanyakazi wa umma na wafanyabiashara walikua na pesa kuliko serikali, nikukumbushe tu, ilifika hatua IMF, world bank, Paris club wakakataa kutoa misaada na mikopo kwa Tanzania wakidai, sie tunasamehe wafanyabiashara KODI, waziri wa fedha wa wakati huo alikua ni professional wa uchumi bwana Kighoma Ali Malima, alifukuzwa barazani kwa shinikizo kutoka nje na hapa sasa ndio umaarufu wa J. Kikwete ulipopanda. Yapo mengi, now mzee wa Lupaso akaaingia madarakani (RIP ) huyu sasa ndio aliyeanza kuleta heshima makazini, watu wapande vyeo kwa elimu; walimu wa UPE walitakiwa kujiendeleza ili walau wapate vyeti vya form 4, elimu ikaanza kua na maana (that's future) akaanza kujenga misingi ua utawala bora, taasisi nyingi unazo zijua leo zimetengenezwa na BWM, tukaanza kuona hata ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege nk. Enzi zake mwamba yule, mgao wa umeme yes ulikiwepo but sio kila mwaka kama ilivokua kwa mtangulizi wake na aliyemfuata. Mgao mkali (kama nitakua nakumbuka vizuri ) ulikua mwaka 1998, aliyemfuata sasa ndio khaa, mgao hadi masaa 16 kwa siku halafu kila mwaka, tukaingia kwenye mikataba ambayo sio ya utatuzi wa umeme kwa maana ya future, ni temporary tu, ndio ikaja Richmond/Dowans, baadae sijui Symbio nk, mwishoni mwa utawala wake ndio ikapigwa pesa ya maana hasa, Escrow account. Magufuli alipokuja akaanza kurekebisha mambo, umeme huo hapo, katanua gati za bandari ya Dar, mikataba ya madini hasa dhahabu I think umeona, nchi ikaanza kua na heshima, baadhi ya mataifa ya Africa yakaanza ku copy from us. Hatimae mwamba yule akafariki.
Vipi, niendelee?