Mshahara wa huyo jambaz ni mishahara ya wachezaj 25 wa Simba ,na mishahara ya wachezaj 40 ya utopolo, mudi aache masihara kabisa awekeze kwenye mpira kama kwel yupo serious .
Yaan watu hapo simba wanakula m5 kwa mwez wengine had 2m huo ni utan ,ifike wakat mchezaj wa kiwango cha chini hapo simba angalau alipwe 15m
Tujaribu kujifunza biashara,uwekezaji unaenda sambamba na purchasing power ya nchi husika,uwekezaji unazingatia mahitaji ya soko.
nguvu ya watanzania kufanya manunuzi iko chini sana,wananchi wako hoi,kupata tu mlo wa siku ni changamoto,hivyo ni ngumu sana MO kufanya hayo mnayoyaitaji.
Tunaona watu wanaoingia uwanja wa taifa kwenye mechi za soka ni wachache sana,ukiondoa mechi ya derby angalau watu wanajaa uwanjani,sasa hizo gharama za kuendesha mradi mkubwa wa wachezaji hao utatoka wapi?!! Kumbuka hakuna mfanyabiashara anae taka kupata hasara.Wananchi wengi uwezo wa kununua vifaa vyenye nembo halisi ya club hawana,wanaishia kununua vitu feki vya bei za chini ambazo mara nyingi club haifaidiki chochote.
Mazingira ya viwanja vyetu sio rafiki kwa wachezaji wakubwa, mchezaji anaweza kupata injury kutokana na ubovu wa uwanja ikamuweka nje msimu mzima,inakuwa hasara kwa kubwa kwa club.
Tunampongeza MO kwa hiki anachofanya angalau kukusanya wachezaji wa kiwango cha kati- chini, wa ukanda wetu wa africa mashariki,taratibu jinsi nchi itakavyokuwa na uchumi imara na watu kuimarika kimapato,ndivyo sekta mbalimbali zitakuwa zinakua pia kwa kupata mapato mazuri na wadhamini wenye pesa nzuri.
Nchi za kiarabu zimefanikiwa kwasababu zina angalau Zina uchumi imara na watu wao Wana uchumi imara hivyo timu zinapata pesa hivyo zinakuwa na nguvu ya kushindana na kumudu wachezaji wazuri,hata South Africa wana uchumi angalau uko imara ndio maana unaona na timu zao zinamudu wachezaji wazuri.