Hawa mabinti wawili watanitoa roho

Hawa mabinti wawili watanitoa roho

Hii hali inanikumba pia mm. Nina mahusiano na mabinti wawili (wote nna mwaka nao wa mahusiano) na wote nawapenda ktk kiwango ambacho nashindwa kumpiga chini mmoja. Hisingekua dini ningeoa wote wawili, bahati mbaya au nzuri wote wawili ni waiislamu na wapo tayari kubadili dini kunifuata,ila mm kubadili kuwafuata wao na kuoa wote wawili naona ni udhaifu mkubwa mnoo.

Eehh Mola nisaidie mja wako kuamua hili swala[emoji120]
Mm mkuu ingewezekana ningewaoa wote ila haiwezekan
 
Kukolea kwa wadada wawili hadi kufikia hatua ya wote kuwa tayari kuolewa nawewe ni kujiendekeza vibaya kunakokuja(ga) kuwatesa kwenye maamuzi ya kuoa yupi na maumivu kwa utakayemwacha!

Kwann usikomae na mtu mmoja toka mwanzo..?
Sasa mkuu imeshatokea, ndo maana maana natafuta solution
 
Chukua mrembo huyo mpambanaji achana nae ukimuoa akisha kuzoea atakua bze na upambanaji wake tu
 
Sasa mkuu imeshatokea, ndo maana maana natafuta solution
Ni ngumu kwetu kukuamulia wakuchagua. Labda ungekuja kuomba ushauri wakwamba umeamua kuwa na huyu flani then uombe ushauri wa jinsi ya kumjuza yule kuwa hutamuoa..
 
Nipe link ya huyo asiye kuwa na shobo/mpambanaji m nioe fasta
 
Narudia oa mwanamke mzuri utakuja kujuta

Unaoa jigsaw eti kisa mpambanaji acha ujinga wengine hatuna adabu ukitukaribisha tumuone mtoto kama ni mbaya kawaharibu lazima tukucheke

Halafu chura muhimu pia
 
Umeshajua kilicho bora Bado hutaki kufanya maamuzi.

Ni wazi huelewi nini unachihitaji mbele ya safari.

Ni muhimu kutooa maana Dunia ilivyoharibika, utakuwa kutesa tu watoto wako.
Kila Bata, ufe, tukuzike.
 
Oya andaa dinner halafu alika wote halafu Wachane ukweli mchungu Kwamba wote unawapenda baada ya hapo angalia watakapoteana either mmoja asepe atakayebaki Ndio sahihi kwako
Kama watabaki wote hapo kazi kwako!

Kwenu studio🎤🎤🎤
 
Hili swala limetugusa wangi Sana 😂😂😂😂😂.as days go . We all don’t know is who . Nahisi hata wenye we wana choices
 
Wana bodi, heshima kwenu.

Kadri muda unavyozidi kwendaa ndio nazidi kuchanganyikiwa, sielewi.. moja haikai, mbili haikai.

Niko kwenye mahusiano na mabinti wawili kwa muda miaka 3+ sasa.. Mmoja ni mzuri sana, mrembo, presentable na udambwiudabwi wa kila aina kwenye masula ya mapenzi na mambo ya show off. Kwenye suala la maisha huyu binti ni chenga, sio mpambanaji kivile.. Ila moyo wangu umelala kwake, kidume sipui kabisa pale.

Huyu mwingi ni binti wa kawaida sana, ana heshima zake tuu.. Kwenye uzur ni kawaida sana, sio mtundu sana.. Kwenye show off yeye hayupo kabisa, akisuka yebo fasta mwendo mdundo.. akibana yeye poa tuu, akibana kwa nyuma na raba bendi kama Jumong fresh tuu hana shida. Ila huyu binti ni mpambanaji bana, ni shujaa.. Linapokuwa swala la maisha huyu binti nampa GPA ya 5.0 ila moyo haupo kwake.

Wote wawili wapo tayar kuolewa muda wowote, hata kesho asubuh.

Nashindwa kabisa kuamua hii issue, nani nimchukue kama mke, nani nimpige chinini maana ni zaidi ya mwaka sasa na nikitazama muda unazidi kukimbia. Kwa upande wangu mm nataman vyote kwa pamoja tena kwa 100%.

Msaada wa mawazo yenye fact tafadhali.
Nini nafasi ya mwanaume katika familia?
 
Kwanza naomba nikushauri kitu ingawa ushauri wangu si sheria

huyo mwanamke mzuri ukishamweka ndani kitu gani utakipata kwake ukiachana na huo uzuri?KUMBUKA,mwanamke hata awe mzuri vp ukishakaa nae kwa mda flan utamuona wa kawaida tu ila wa nje ndo watakusifia kwamba una mke bomba lkn ww utaona kawaida tu,tena unaweza kuta unataman hd beki 3

Kumbuka,umri unaenda uzuri unapotea coz ya uzee,sasa jiulize uzuri ukishapotea utakuwa na nn cha kujivunia kwa huyo mwanamke?

Ushauri wangu..usione watu wanafunga ndoa ukadhan wanapendana sanaaaaa,no...asilimia kubwa ni kukubaliana kufichiana madhaifu lkn upendo unakuta upo kdg sana

Oa mwanamke atakaeweza kukusitiri pindi mambo yako yakikwama..kumbuka ukioa maana yake mnaanzisha familia..sasa oa uzuri wenye akili za kutafuta 0,utakuja kusimulia huku!!
 
Wana bodi, heshima kwenu.

Kadri muda unavyozidi kwendaa ndio nazidi kuchanganyikiwa, sielewi.. moja haikai, mbili haikai.

Niko kwenye mahusiano na mabinti wawili kwa muda miaka 3+ sasa.. Mmoja ni mzuri sana, mrembo, presentable na udambwiudabwi wa kila aina kwenye masula ya mapenzi na mambo ya show off. Kwenye suala la maisha huyu binti ni chenga, sio mpambanaji kivile.. Ila moyo wangu umelala kwake, kidume sipui kabisa pale.

Huyu mwingi ni binti wa kawaida sana, ana heshima zake tuu.. Kwenye uzur ni kawaida sana, sio mtundu sana.. Kwenye show off yeye hayupo kabisa, akisuka yebo fasta mwendo mdundo.. akibana yeye poa tuu, akibana kwa nyuma na raba bendi kama Jumong fresh tuu hana shida. Ila huyu binti ni mpambanaji bana, ni shujaa.. Linapokuwa swala la maisha huyu binti nampa GPA ya 5.0 ila moyo haupo kwake.

Wote wawili wapo tayar kuolewa muda wowote, hata kesho asubuh.

Nashindwa kabisa kuamua hii issue, nani nimchukue kama mke, nani nimpige chinini maana ni zaidi ya mwaka sasa na nikitazama muda unazidi kukimbia. Kwa upande wangu mm nataman vyote kwa pamoja tena kwa 100%.

Msaada wa mawazo yenye fact tafadhali.
Hahahahaaaaaaaa
 
Oa unayempenda

Hakikisha una kipato...si mmeambiwa wanaune watakula kwa jasho? Hakikisha una fedha za kushow off na udambwiudambwi mpaka uzeeni.

Unamtaka mpambanaji halafu baada ya miaka 10 uje mkeo hafui hapiki kutwa kufukuzia pesa?????
 
Ila waomba ushauri wanashangaza sana.
Yaani anakuja kuomba ushauro ilhali ana maamuzi yake tayari yasiyoyumbishwa.

Wewe ushasema unamkubali huyo slayqueen na hapo umempa sifa kibao kuliko huyo mwingine uliemdisi kabisa kua yeye ni kama jumong!! Halafu eti unaomba ushauri wa kuoa umuoe nani.

Mkuu wewe huombi ushauri ila unatafuta wataokusupport kuoa huyo slayqueen.
Halafu sasa mbaya zaidi unaonekana huna doo, we mwanaume upambanaji wa mwanamke unahusika vipi ilhali wewe ni mpambanaji au unataka kulelewa.

Na huyo slayqueen anavokuendesha mtaachana kesho tu mkioana. Akili kumkichwa, kalaghabaho.
 
Uyu wapili kuna jambo alinteka ambalo sikuwahi kutana nalo toka nianze mahusiano ya mapenzi. Kupitia hilo hilo jambo, nikaona wacha nijilipue nisongeshe wawili kibingwa.
Jambo gani? hebu liseme tukuelimisha ipasavyo
 
Back
Top Bottom