Hawa madereva wa serikali waangaliwe kwa umakini sana watawaua viongozi wetu wote

Hawa madereva wa serikali waangaliwe kwa umakini sana watawaua viongozi wetu wote

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Hawa watu wanakabidhiwa LC 300 gari ya gharama kubwa na kuwabeba viongozi wetu, hili jambo litazamwe upya

ili uwe dereva unahitaji kufanya mafunzo ya mchongo na pengine yenye usimamizi hafifu na kuachiwa uingie barabarani ukalete madahara kwa watu wengine

Darasa la saba B atapewaje gari ya thamani kubwa ikiwa imembeba mtu ambaye upatikanaji wake unachukua miaka mingi ya kielimu na kiuzoefu?

Uwezo wao wa kufanya maamuzi hata yale binafsi ni mdogo, inakuaje aachiwe akafanye maamuzi mazito huko barabarani?

Wakati umefika, viongozi wajiendeshe wenyewe au wasafiri kwa vyombo vingine ambavyo wanaondesha wanatumia muda mwingi darasani na hawaku-fail darasa la saba

Nawasilisha kwa hasira

PIA SOMA
- TANZIA - Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari
 
Mkuu lakini kwa ajali ya leo huko Kilimnjaro inayomhusisha Katibu Tawala wa Mkoa, kulingana na Mkuu wa Mkoa Mohammed Babu, mwenye makosa si dereva wa serikali bali dereva wa lori lililokuwa lina ovateki wakati magari mengine yaliyosimamishwa yamesimama.

Hivyo ikawa uso kwa uso.
 
My friend you lack seriousness. Waliomo kwenye hayo magari ndo hao hao viongozi na watunga sera. Kama wanashindwa kuwaambia madereva wao wapunguze mwendo au wafuate sheria za barabarani, si unaona hata umakini wa hao viongozi ni wa kutiliwa Shaka?

Wakati mwingine nadhani hawa viongozi wanaotumia magari ya kodi zetu, wanajiaminisha kwamba ajali zinawahusu walipa kodi pekee.

Inasikitisha, lakini ajali zitapungua endapo magari ya serikali yataanza kufuata sheria na kuwajibishwa kama raia wengine.
 
Mkuu lakini kwa ajali ya leo huko Kilimnjaro inayomhusisha Katibu Tawala wa Mkoa, kulingana na Mkuu wa Mkoa Mohammed Babu, mwenye makosa si dereva wa serikali bali dereva wa lori lililokuwa lina ovateki wakati magarai mengine yaliyosimamishwa yamesimama.
Hivyo ikawa uso kwa uso.
Endelea kutetea upuuzi, hao watu hawana akili kabisa, wengi wanavunja sheria za barabarani na ku-overtake kwenye milima na kona kali bila kujali
 
Mkuu lakini kwa ajali ya leo huko Kilimnjaro inayomhusisha Katibu Tawala wa Mkoa, kulingana na Mkuu wa Mkoa Mohammed Babu, mwenye makosa si dereva wa serikali bali dereva wa lori lililokuwa lina ovateki wakati magarai mengine yaliyosimamishwa yamesimama.
Hivyo ikawa uso kwa uso.
Ajali nyingi zinazohusisha magari na viongozi wa serikali. Mara nyingi chanzo ni uzembe!
 
My friend you lack seriousness. Waliomo kwenye hayo magari ndo hao hao viongozi na watunga sera. Kama wanashindwa kuwaambia madereva wao wapunguze mwendo au wafuate sheria za barabarani, si unaona hata umakini wa hao viongozi ni wa kutiliwa Shaka...
Mkuu, viongozi wengi wanakua exhausted, wanalala tu njiani, ukiona dereva katulia barabarani manake kiongozi yuko macho
 
Wakati umefika, viongozi wajiendeshe wenyewe au wasafiri kwa vyombo vingine
Viongozi kama Samia, Majaliwa na Mpango wajiendeshe wenyewe, au wapande mwendokasi? Nawaza tu.


Darasa la saba B atapewaje gari ya thamani kubwa ikiwa imembeba mtu ambaye upatikanaji wake unachukua miaka mingi ya kielimu na kiuzoefu?
Kwahiyo unataka dereva awe na PhD, amuendeshe mbunge darasa la saba kama Msukuma, Maganga na Babu Tale?

Au unataka dereva awe profesa aendeshe wabunge f4 na f6 failures kama Biteko, Jenista, mama Salma, Margret Sitta, n.k?
 
Viongozi kama Samia, Majaliwa na Mango wajiendeshe wenyewe, au wapande mwendokasi? Nawaza tu...
Nimetoa options ya kujiendesha au watumie vyombo vingine ata kama wakipanda punda au farasi, ajali zitapungua
 
Back
Top Bottom