Hawa mbuzi wanaozagaa maeneo ya Mbezi Tangibovu ni wa Serikali?

Hawa mbuzi wanaozagaa maeneo ya Mbezi Tangibovu ni wa Serikali?

Bamping

New Member
Joined
Sep 29, 2021
Posts
1
Reaction score
51
JF,

Kwa kweli nimekuwa nikipata shida sana kuona mbuzi Hawa wanazagaa barabarani hovyo wakati Sheria za kutunza wanyama zipo wazi.

Je wale ni wa Serikali au? Kwasababu najua kabisa wangekuwa wa mtu binafsi wangeshakamatwa zamani na kutozwa faini.

Nani au Mamlaka gani ya Serikali inawajibika kusimamia wanyama wale inaleta mawazo mabaya kuichafua Serikali kwa vitu vidogo kama vile eti vimeshindikana na vimeachwa holela tu.

Naomba wahusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo kwa sababu mbuzi Hawa wanaishi barabarani zaidi ya miaka mitano na ushee.

Pia, soma=> Mbuzi wanaozurura mijini ni wa nani? Inakuwaje hawaibwi na vibaka na hurudi nyumbani hata km 10 wenyewe?
 
Hao mbuzi wanapanda mpaka juu ya bati bila ngazi

Screenshot_20220505-221123.png
 
Kuendekeza ushirikina tu haifai!

Halmashauri kitengo cha mifugo watoe tangazo la kila mtu afungie mifugo yake la sivyo ikiachwa na kutembea hovyo mtaani/barabarani ikamatwe na kwenda kutelekezwa porini!

Wanakwaza sana

Wanasababisha ajali
 
Hata mbwa ambao wenyewe hawataki kuwafungia wanawaacha mtaani ni hatari kubwa,

Mbwa wakati wowote hubadilika na kuuma watu,

Halmashauri watoe tangazo la watu kufungia
Mbwa wao la sivyo wawakamate na kuwaua!

Kuweni pro-active badala ya kuwa reactive!
 
Hawa mbuzi wanashangaza sana..yaani hata jeshini Lugalo huwa wanatimba fresh tu. Wanajeshi wenyewe huwa hawathubutu kuwachinja.

Hawa mbuzi 🐐 hapo mjini wanavuka barabara kama watu yaani.

Siku moja natoka karume nakutana nao abiria wakawa wanapiga story kuwa hata wakifa huwa wanaenda kuzikwa mikoani huko.

Swali langu ni hawa panya road au vibaka huwa hawawaoni au?

1651778536281.jpg
 
JF
Kwa kweli nimekuwa nikipata shida sana kuona mbuzi Hawa wanazagaa barabarani hovyo wakati Sheria za kutunza wanyama zipo wazi..Je wale ni wa Serikali au ?? Kwa sababu najua kabisa wangekuwa wa mtu binafsi wangeshakamatwa zamani na kutozwa faini..Nani au Mamlaka gani ya Serikali inawajibika kusimamia wanyama wale..inaleta mawazo mabaya kuichafua Serikali kwa vitu vidogo kama vile eti vimeshindikana na vimeachwa holela tu..Naomba wahusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo kwa sababu mbuzi Hawa wanaishi barabarani zaidi ya miaka mitano na ushehe..
Wale Mbuzi hawana Mwenye nao, Jichangamye uone Sasa Moto wake
Kuna Mwanangu Mmoja aligonga Mmoja, alishinda Parokiani akisali wiki nzima kujikabishi chini ya Ulinzi wa Mungu
Ndio ilikuwa pona yake
 
Nadhania ipo thread humu kuhusu hao mbuzi..hao mbuzi Huwa hawaguswi miaka Mingi Sasa na kumekuwa na story nyingi zikihusishwa na ushirikina ..kutokana na hizo story hakuna mtu ameweza wakamata.

Hata wanajeshi hapo lugalo wanaaaangalia tu na hakuna kitu watawafanya eneo lao pendwa kutembea ni kuanzia mwenge Hadi tegeta kama wanazaliana pia it's another problem. Serikali ichukue hatua au inawaogopa?
 
Wale Mbuzi hawana Mwenye nao, Jichangamye uone Sasa Moto wake
Kuna Mwanangu Mmoja aligonga Mmoja, alishinda Parokiani akisali wiki nzima kujikabishi chini ya Ulinzi wa Mungu
Ndio ilikuwa pona yake
Imani za kishirikina watz wanazipenda sana
 
Imani za kishirikina watz wanazipenda sana
Mimi nimemshudia kijana bodaboda amegonga hao mbuzi hakwenda kwa mwenyewe kuomba msamaha kesho yake hakuamka tumezika, ni true story.

Hao mbuzi wapo wa mpemba mmoja maeneo ya kwa Gude jet kiwalani anajurikana nao wanazurura tu.

Ukigonga hao mbuzi inabidi uende kujisalimisha kwake kinyume chake lazima parapanda litaimbwa nyumbani kwenu, hili ni jambo nimelishuhudia sijahadisiwa na mtu.
 
Serikali imshughulilie huyo mpemba au serikali inamwogopa?
 
Serikali imshughulilie huyo mpemba au serikali inamwogopa?
Wapemba unawajuwa au unawasikia?

Kuna ndugu yao kafa mwezi wa pili na wao wakajibu mapigo mwezi uliofuata tarehe ileile aliyokufa ndugu yao.
 
JF
Kwa kweli nimekuwa nikipata shida sana kuona mbuzi Hawa wanazagaa barabarani hovyo wakati Sheria za kutunza wanyama zipo wazi..Je wale ni wa Serikali au ?? Kwa sababu najua kabisa wangekuwa wa mtu binafsi wangeshakamatwa zamani na kutozwa faini..Nani au Mamlaka gani ya Serikali inawajibika kusimamia wanyama wale..inaleta mawazo mabaya kuichafua Serikali kwa vitu vidogo kama vile eti vimeshindikana na vimeachwa holela tu..Naomba wahusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo kwa sababu mbuzi Hawa wanaishi barabarani zaidi ya miaka mitano na ushehe..
Kuna Threads nyingi sana hapa JamiiForums za Kuwazungumzia hao Mbuzi nasikitika hujazifungua ili uzisome na upate Undani wake zaidi.

Hao Mbuzi unaowana hapo 50% ni Mbuzi kweli ila 50% ni Wenzetu na hapo wapo Kazini. Sheria yao Ukimgonga Mmoja na Kumuua usikimbie au usimchukue Ukamle bali jisalimishe kwa Mmiliki wake kisha ondoka zako kinyume cha hapo Ndugu zako watakuwekea Maturubai ya Msiba Nyumbani Kwako tayari kabisa kwenda Kukuzika mazima.
 
Hawa mbuzi wanashangaza sana..yaani hata jeshini Lugalo huwa wanatimba fresh tu. Wanajeshi wenyewe huwa hawathubutu kuwachinja.

Hawa mbuzi [emoji238] hapo mjini wanavuka barabara kama watu yaani.
Siku moja natoka karume nakutana nao abiria wakawa wanapiga story kuwa hata wakifa huwa wanaenda kuzikwa mikoani huko.

Swali langu ni hawa panya road au vibaka huwa hawawaoni au?

View attachment 2213112
[emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom