Sikupingi, haya mambo yapo. Huku kwetu Kuna siku Niko stationary wakawa wanapita mbuzi na kondoo barabarani. Nikasema loooh Hawa mbuzi vipi mbona hawana mchungaji, si wataibiwa na vibaka?. Yule mwenye stationary alicheka akasema, "dada kamata mbuzi ata 1 apo halafu uone kimbembe chake, hutaamka mzima ww. Hao mbuzi wanatembea popote na wanarudi Kwa mwenyewe wakiwa idadi sawa kabisa. Sasa ww jichanganye. Mie mdomo ukaachia Kwa mshangao.
Nilivyomaliza nikaondoka, nafika nyumbani nikaanza muelezea bi Mkubwa. Bi Mkubwa akasema, heee hao si wa Mzee Fulani, anasifika kwa uchawi, na gusa uone kama utapona. Watu wote wanamuogopa, na akitaka kuchinja mbuz mojawapo anasimama Nyumbani kwake anaita tuu [emoji3][emoji3] basi mbuzi kokote walipo wanarudi Kwa kasi Sana, anachagua amtakaye then wengine wanaendelea kutawanyika.
Duniani Kuna mambo aisee [emoji28][emoji28]. Nilichoka Kwa taarifa.