Hawa ndio vijana wamenivutia katika miongo miwili hii tuliyonayo

Kama hawa hawapo
Bambo
Onyango
Sugu
Lema
Natoa shilingi
Sugu- na makeke yake bungeni lakini baada ya kushindwa ubungu hakutia neon ameahisi yeye na dada yake Tulia watashirikiana kuleta maendeleo jimboni kwao amenifurahisha sana
 
Mkuu lazima tukubali kuna wengine wana bahati ya kuvuma
Sina uhakika kama swali lililenga kwenye mada au mvuto gani,manake huchelewagi wewe!
No yuko sahihi maana ninyi mko bize kuwafagilia wenzenu huku mkisahau vipaji vyenu wenyewe, ambalo ni jambo la kipuuzi. Unakuta mko kwenye kikao mnaambiwa pendekezeni majina 10 ya vijana wa kuingia kwenye kamati fulani, badala ya mtu kusimama na kusema najipendekeza mwenyewe wote wanaishia kupendekeza wengine, huu ni ulofa.
 
Mkuu upo sahihi kwa upande fulani,lakini nimetumia neno 'kuvutiwa' .Inazewezekana na mimi nimefanya vizuri katika sekta yangu lakini hainizuii kuona ubora wa wengine.
MIMI mwandishi mzuri habari naachaje kuvutiwa na Mexence Melo au Millardayo?
AU mimi John Boko nashindwaje ku appriciate juhudi za Samata? AU Konde boy anaanzaje kujitaja yeye kabla ya diamond? Lazima tukubali ku appriciate wengine kama wanafanya vizuri zaidi yetu,kufanya hivyo hakuondoi ubora/ufanisi wako
 
1.Sugu..kutoka kuonekana muhuni wa muziki wa kufoka hadi kuisimamisha bongo fleva kwenye ramani na vijana sasa wanapiga hela kama ajira rasmi inayotambulika.Pia kutoka ktk bongo fleva huku zile elements za uhuni zikiwa bado hazijaisha na kuuvaa ujasiri wa kugombea ubunge na kuhamasisha vijana wengine hasa wasanii kama yeye kuingia mjengoni..yaan huyu kwangu mm ni mpambanaji anaejiamini bila kujali mtazamo wa watu wengine kuhusu yeye..
2.Diamond Platnams..huyu kijana ni fighter haswa na ni ROLUMODO kwa sisi vijana wengi mana mwanzo wake unafahamika,upambanaji wake unaonekana, na mafanikio yake yana reflect kile anachokifanya..ameubadili mziki wa bongo fleva kutoka kwenye umaarufu bila kipato hadi biashara kubwa inayolipa..
3.January Makamba..huyu kwangu ni Presidential Material..Hekima,Busara,Maarifa,Utulivu,Heshima,Nidhamu pamoja na Ustaarabu hizi ni miongoni mwa sifa chache alizonazo mwanasiasa huyu kijana ndani ya CCM japo mm sio mwanachama wala mpenzi wa CCM..kama taifa jukumu letu kuvilea vipaji hivi ili vije kuwa msaada mbeleni...
4.Zitto Zuberi Kabwe..hiki kichwa kina Talanta ya Siasa,huyu ni mwanasiasa hasa..hakuna mtanzania makini asiejua mchango wake ktk maendeleo ya nchi yetu hasa ktk ujengaji wa hoja za mashiko na ukosoaji wa kistaarabu..ni Kielelezo cha uhamasishaji vijana kuvutiwa ktk siasa...
5.Mbwana Ally Samatta..Miongoni mwa Vipaji tulivyojivunia watanzania ni kuwa na kijana huyu ktk taifa letu,Juhudi zake,Njaa zake za mafanikio,pamoja na nidhamu ni mfano bora kwa vijana wengine wa kitanzania ktk medani za ulimwengu wa soka,yeye na mwenzake Simon Msuva mwenyeziMungu awabariki wafike ndoto zao ili wazidi kujenga hamasa zaidi kwa vijana wengine waongeze juhudi wawe kama wao..
6.Millard Ayo...Very appreciate you brother.....
7.MwanaFA...Very appreciate you brother....
8.Ali Kiba..I appreciate you brother, but you're not like that..you can do more than that,jicho langu LA tatu nikikuangalia nakuona unatumia asilimia nusu ya ubora wako japo mafanikio yako pia si ya kubeza...
9.Konde boy..Keep keep keep fighting brother...
10.Mimi mwenyewe Binafsi...Kiukweli najikubali sana mwenyewe..Nakubali harakati zangu binafsi ktk kujitafutia kipato ili niweze kuwa MTU bora zaidi ya sasa japo nimekuwa nikikumbana na vikwazo vingi vya wazi vya makusudi kabisa ktk juhudi zangu za kunifikisha kule ninakotaka kwenda..ila pamoja na hayo bado nimekuwa MTU imara nisiekubali kurudishwa nyuma kirahisi na kunifanya niendelee kupambana bila kuchoka wala kukata tamaa.naamini nitafika kule nitakako kufika hata kama itachukua muda..
Huo ni mtazamo wangu binafsi
Asante
 
Asante mkuu kwa hiyo list iko vizuri.
ILA bwana sugu wakati mwingine anakuwa mgomvimgomvi
 
Umewasahau vijana wafuatao kwa kukubalika na vijana wa kike na kisha kuungana nao:
1. Kapuya
2. Pius Ng'wandu
3. Mengi
nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…