Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao

Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao

Hata hao ulioonana nao sidhani kama walidai wana hivyo vitu vyote.

Ni uongo na uzushi wako tu.

Mtu ataanzaje kusema ana hivyo vitu vyote?

Na wewe ulikuwa unaandika kwenye daftari hayo yote waliyokuwa wanayasema?

Wewe ni muongo na mzushi tu!
Naona sasa umekuwa nabii, popote nilipo upo, na unayasikiliza maongezi yetu. Vyema sana ndugu nabii
 
Hiyo ilikua JF ya zamani, watu wakakutana, wengine walikimbia makutano kwa vile walivyokuwa wanajimwambafai, wengine walikua omba omba pm lakini nje wanajinadi wana mapesa na wanafanya mambo makubwa, wengine walidhalilishwa kwa picha zao halisi wakajulikana kumbe ni wale wale pangu pakavu tia mchuzi. Baada ya kujuana uhalisia hayo mambo yakapungua kama sio kuisha hapa jukwaani.

Sasa hivi kuna vijana wa hovyo wanaojisifia kuchakata mbususu, wanajua kuhonga, wana mihogo mikubwa, hao nao wana muda wao kabla hawajalipuana humu wambea tukatafuta popcorn na pepsi.
 
Kama hujawahi kukutana na mimi na huu uzi si wako
Wewe ni muongo tu hahahaaaa.

Unataka kujipatia vi brownie points kwa kuwasema hao uliokutana ili sijui uonekane uko ‘real’.

FOH with that bullshit.

Mtu anaanzaje kukuambia wewe ana hivyo vitu vyote?

‘Aisee Bujibuji, mimi nina gari, nina madigrii, nina ma akaunti Uswisi, nina mashamba, nina matrekta’…

Wewe ni mzushi tu. You don’t sound believable at all.
 
Niliokutana nao mimi wote wana wake zao wanne na wote wamewajengea, hakuna hata mmoja anaefanya kazi kati yao wote anawahudumia yeye kwenye majumba yao🤣 wote hawapendi wanawake wafanya kazi. Jf raha sana sasa sijui hawa marioo tunaowaona huku mitaani ni zao la wapi
 
1. Wote wana magari
2. Wote wana majumba yenye majina ya kizungu ie contemporary house, bungalow, crib, mansion na kadhalika.
3. Magari waliyo nayo ni ya gharama kubwa, hamna mwenye vits wala IST.
4. Elimu zao ni kubwa kama nyumba zao na magari yao.
5. Wote ni maboss
6. Wote ni wafanyabiashara wakubwa.
7. Wote ni watu wa safari sana, zile safari za nje ya bara letu.
8. Wote walizipeleka familia zao vacation
9. Wote wamesoma shule nzuri za kimataifa
10. Wote walikuwa wakali sana darasani.
11. Wote wana wenza wenye hela nyingi na wazuri sana.
12. Wote familia zao ni bora sana na zina upendo wa hali ya juu sana.
13. Wote wanatumia simu kali na za juu. Techno na infinix wanawapa walinzi wao
Wote wana access na mkuu wa nchi muda wowote watakao.

Usiwaamini mtu hapa jukwaani, watu wamechoka balaa.
Watu hawana ajira, wanapost kuwa wao ndio wana uwezo wa kuajiri.

Watu hawana mitaji lakini hapa wanajiita wafanyabiashara wakubwa.

Hawana pesa ya kulipa pango la nyumba, wanaishi kama digidigi kwa kuwakimbia wenye nyumba walizopanga, lakini wakiwa hapa jukwaani wanajiita Land lord.

Kuwa macho ndugu yako
Vyote hivyo nnavyo kwani ni dhambi
 
Ni uongo tu.

Hakuna sehemu yoyote hapa ambapo watu wote huwa wanasema hivyo.

Halafu, kama ni wote huwa wanasema hivyo, ina maana na yeye huwa anasema hivyo, si ndiyo?

Au yeye anajitoa katika hao ‘wote’?

Mimi naona yeye ana project vile ajionavyo humu.
Nyani unamkumbuka mwalimu Sharifu huyu kuna siku alinifanyia kitu siwezi msahau
 
1. Wote wana magari
2. Wote wana majumba yenye majina ya kizungu ie contemporary house, bungalow, crib, mansion na kadhalika.
3. Magari waliyo nayo ni ya gharama kubwa, hamna mwenye vits wala IST.
4. Elimu zao ni kubwa kama nyumba zao na magari yao.
5. Wote ni maboss
6. Wote ni wafanyabiashara wakubwa.
7. Wote ni watu wa safari sana, zile safari za nje ya bara letu.
8. Wote walizipeleka familia zao vacation
9. Wote wamesoma shule nzuri za kimataifa
10. Wote walikuwa wakali sana darasani.
11. Wote wana wenza wenye hela nyingi na wazuri sana.
12. Wote familia zao ni bora sana na zina upendo wa hali ya juu sana.
13. Wote wanatumia simu kali na za juu. Techno na infinix wanawapa walinzi wao
Wote wana access na mkuu wa nchi muda wowote watakao.

Usiwaamini mtu hapa jukwaani, watu wamechoka balaa.
Watu hawana ajira, wanapost kuwa wao ndio wana uwezo wa kuajiri.

Watu hawana mitaji lakini hapa wanajiita wafanyabiashara wakubwa.

Hawana pesa ya kulipa pango la nyumba, wanaishi kama digidigi kwa kuwakimbia wenye nyumba walizopanga, lakini wakiwa hapa jukwaani wanajiita Land lord.

Kuwa macho ndugu yako
Afadhali kama iko hivyo.
Angalau wote sio chawa wa wanasiasa na watu maarufu
 
Back
Top Bottom