Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao

Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao

Wewe ni muongo tu hahahaaaa.

Unataka kujipatia vi brownie points kwa kuwa seam hao uliokutana ili sijui uonekane uko ‘real’.

FOH with that bullshit.

Mtu anaanzaje kukuambia wewe ana hivyo vitu vyote?

‘Aisee Bujibuji, mimi nina gari, nina madigrii, nina ma akaunti Uswisi, nina mashamba, nina matrekta’…

Wewe ni mzushi tu. You don’t sound believable at all.
Mkuu,uko serious Sana. Umemkalia Bujibuji kooni ila Mimi naona Kama jamaa ni mtu wa utani mwingi. Don't take it seriously.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mbona me sina gari, sina nyumba, sina biashara, sina elimu, sio boss, ssiendagi vacation na ni mwana JF? Au ni mimi peke angu?
Huendi vacation[emoji23][emoji23]kuna uzi nimeona unatupata utaratibu wa kuvisit Lushoto
 
1. Sio wote Wana magar
Nenda jukwaa la magari utaupata uhalisia nyuzi kibao Watu wanawaza wajichange vipi kutoka kwenye adha ya daladala, bodaboda na miguu

2. Sio wote Wana majumba,
Nenda jukwaa la ujenzi uone nyuzi kibao Watu wanauogopa ujenzi, hawajui watatokaje nyumba za kupanga
Jukwaa la hoja mchanganyiko Watu wanatafuta hata pa kuegesha kichwa TU.

3. Sio wote Wana biashara au ajira kubwa Nenda jukwaa la biashara, Kuna Watu Wanahangaika hata biashara ya mtaji wa elfu 30

Jukwaa la kazi na ajira, majobless kibao wengine Hadi jukwaa la Siasa wanalalamikia ukosefu wa ajira na maslahi kiduchu

4...... Mengine naona wameshatiririka sana wakuu

NNACHOONA
JF Ni jukwaa mtambuka Sana
Kuna Watu wa kila Aina, maskini, matajiri, wakawaida, wanasiasa, madaktar n.k

Pia sio kila kinachoandikwa humu uchukulie serious Sana, ukiamini 100%

Kwa mwingiliano ulioko humu tegemea kila Aina takataka, suala Ni wewe kuchuja kutumia akili zako mbivu na mbichi.
 
Hata hao ulioonana nao sidhani kama walidai wana hivyo vitu vyote.
Kiswahili kigumu amesema

Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao JF sio nilioonana nao nje ya JF.

Anamaanisha kwamba ni amewakuta humu amewajua humu na wapo humu km sio wewe basi kaa ukijua wapo wenye wameandikwa kwenye hio orodha usibishe, humu kuna kila aina ya watu na unakutana nao na kupishana nao kwenye cordor za JF kila leo kwa hio kiswahili cha mtoa mada kisikuorofishe ubongo mkuu, mimi binafsi nimekuelewa ukitaka kuelewa anazungumzia nini tafuta uzi za Bill Lugano uone anavyojieleza leo yupo Thailand kesho anaenda kutembelea Malaysia, wewe upo wapi?

Huo ni mfano mmoja wapo tu nimemzungumzia wengine wapo, je kweli Bill Lugano ana ukwasi kiasi hicho cha kuzurula kila majiji ya hii dunia au yupo Tandale kwa mfuga Mbwa tu hapo? Sorry mkuu Bill Lugano kwa kukutolea mfano Ila kuna watu bila kuonyeshwa mifano hawawezi kuelewa

Ukiniondoa huyo wapo wengi wengine ambao kweli yaliyoandikwa ndio maisha yao na wapo humu JF, sasa kuna ubaya gani mtoa mada anaposema amekutana nao humu JF? Sio kwamba amekutana nao Bar au nyumbani kwake
 
Mtoa mada kaleta Uzi wake kikejeli flan hivi
Ila niseme TU kua tusikatishane tamaa
Jf pia Kuna Watu wema na wazur sana

Kuna Watu wengi humu wametatua changamoto zao mbalimbali kupitia wanajf

Ukiona huiamini jf Basi unakiogopa Hadi kivuli chako mwnyw (yaan fake I'd)

Nmekutana na watu zaidi 20 nje ya jf na sijawai kujutia hasa, juz juz nilileta Uzi flan wa malalamiko kule HHM.

Kuna mwanajf kauona na kunifata pm,
Nmeonana nae kumbe ni mtu mkubwa mwenye mamlaka Sema id Yake kichekesho, kanitatulia changamoto yangu tumekua marafiki mpk Sasa na tunaheshimiana Sana.

DAIMA SIJUTII KUIFAHAMU JF[emoji4][emoji1431]
 
Kudai kwamba wote wako hivi au wote wako vile ni uongo. Ni uzushi.

Je, kati ya hao wanaJF ‘wote’ nawe umo?

Sijawahi kuona popote pale hapa JF ambapo kila mtu alisema ana gari au yeye ni bosi au sijui kasoma shule bora.

Hiyo ‘wote’ ni projection yako tu.

Acheni uzushi na uongo.
Msome mpaka mwisho utamwelewa
 
Back
Top Bottom