Hawa ndio wasanii wa Tanzania wenye hali nzuri za kiuchumi baada ya maisha ya muziki. Nani kasahaulika?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
wasanii wenye Hali nzuri nje ya Sanaa ta mziki, Kwa Sasa hawajishughulishi sana na mziki kama kazi zao kuu, ni wastaafu

Si jambo la kuficha kwamba ni wasanii wachache huwa wana hali nzuri za kiuchumi baada ya maisha ya muziki

Orodha ya hawa wasanii hatuwezi kusema kwamba ni matajiri wa kutisha sana ila itoshe kusema kwamba angalau kiuchumi wapo freshi,

Alafu cha kushangaza hata katika hao wachache orodha imejaa kundi kubwa la wasanii wa hiphop,

Sugu



Ashakuwa mbunge mara 2 wa mbeya, Ana dili zake toka kitambo enzi hizo 2002 anaitoa sugu moto chini aliwachana mapromota (Laki 1 na nusu kitu gani dili zangu milioni 1 , 2, 3 4, mpaka 5), Ukifika Mbeya maeneo ya ushuani mitaa ya Uzunguni, Taita huyu ana hoteli yake inaitwa Desderia


-Proffesor Jay

Nae ashakuwa mbunge wa Mikumi, Kibunda cha milioni 250 kiinua mgongo kinahusika

- AY

Yeye pamoja na mwenzake Mwana Fa walikunja kibunda cha bilioni 2 baada ya tigo kuwalipa kama fidia ya kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ridhaa yao)

-Mwana FA


Ukiachana na mzigo mzito walioutwika yeye na mwenzake kutoka Tigo, kwa sasa huyu ni naibu waziri wa michezo

Bonta


Huyu ni daktari wa serikalini.

- Roho saba

Ni afsa wa jeshi mwenye cheo si haba,

Niki wa pili


Napendaga kumuita John kisomo wa hiphop yetu hapa Tz, Mwamba kabukua sio kitoto, ana PHD ya darasani, kwa sasa kalamba Teuzi ni Mkuu wa wilaya.
 
Sijui ni Mimi tu nimeelewa tofauti? sky soldier ameweka bayana wasanii wenye hali nzuri nje ya Sanaa ya mziki. Nafikiri alilenga wale ambao kwa sasa hawajishughulishi sana na mziki kama kazi zao kuu za kujiingizia kipato.

Sasa watu wanataka waingizwe kwenye orodha akina Diamond au Lady Jaydee wakati wao bado wanafanya mziki.

Tujitahidi kidogo kuongeza umakini Kwa kusoma na kuelewa kabla ya kuuliza au kuandika jambo, hata mimi kuna wakati nafanya haya makosa.
 
Hamna mwenye pesa hapa katika wote uliowaorodhesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…