Hawa ndiyo wasanii waliovuma sana mwisho wakasanda

Hawa ndiyo wasanii waliovuma sana mwisho wakasanda

Yule msanii aliyeimba wimbo "Nakuhitaji" anaitwaje?

Nakuhitaji mpenzi we nakuhitaji, unaniita?
Nakuhitaji mpenzi we nakuhitaji, unaniita?

Hapo kati kati anachanganya na kilugha kidogo, sijui kinyakyusa
 
Bongo fleva ya zamani ilikua tamu sana,lakini mziki wao haukuwalipa kiivyo tofauti na sasa muziki unalipa kweli hasa ukiwa na kipaji+promo,wasanii wa sasa kuna platform nyingi za kuprimoti na kuuza muziki tofauti na zamani hata Facebook haikuwepo,wataalamu wa biashara wanasema huenda biashara unayoifanya leo baada ya miaka mitano ikawa sio biashara tena kama utakua sio mtu wa kubadilika,alafu wasanii wa zamani ukikutana nae hata leo huwa wanaamini bado watarudi kwenye game tena,unakuta mtu alihit miaka kumi iliyopita lakini mpaka leo anaamini atahit tena,huko ni kujidanganya ni bora kutafuta shughuli nyingine za kufanya,kuna msanii wa zamani nilikutana nae anaendesha Bajaji kule Tabata yaani nilifurahi sana aisee,nikaona ana akili kajiongeza kaona hapa mambo ya kutegemea muziki kwa sasa siwezi tena,muziki una wenyewe kina WCB kwa sasa,.....wasanii wa zamani hawakua na management zenye akili na kuwashauri tofauti na sasa,alafu kipindi kile walionewa sana media maana ndio ilikua kimbilio lao,wimbo upigwe redioni ili upate show,tofauti na sasa vinaangaliwa vitu vingi kama Video kali,kipaji,promo, fan base,kiki,social media na u team fulani....leo hii wewe hata ukiwa msanii mchovu ukipelekwa pale WCB ukatoa wimbo eti unakuta wimbo wako una viewers milioni,muziki wa sasa kuna muda unaangalia alietoa wimbo ni nani,kuna madogo yana vipaji huko kitaa kumzidi hata Harmonize au Diamond lakini hawana platform za kuweza kuhit,....ni rahisi sana msanii mwenye pesa kutoa ngoma mbaya na ikapendwa,na ni ngumu vilevile kwa msanii mwenye kipaji lakini hana pesa kutoa ngoma na ikahit japo wapo ila sio wengi....leo hii ni kazi sana mtu kama Diamond kushuka kimuziki kama ilivyokua kwa Juma Nature au Mr Nice(do you know why?), Diamond kashajiimalisha kila sector kwahiyo sasa muziki wake hautegemei kitu kimoja tu kiitwacho kipaji no no,yeye kwa sasa ameweka mazingira ya kusikika taka usitake,ukimkosa you tube utamkuta Wasafi Tv,Wasafi Redio,now kaanzisha Wasafi Festival,kwaiyo mtu kama huyo hawezi kushuka kirahisi,tofauti na zamani msanii huna chochote zaidi ya sauti yako,ila yote kwa yote hawa jamaa siji acha kuwapongeza,Mwana Fa,Ay,Jide,Fid Q,hawa jamaa wame maintain muziki wao,mimi nilikua mshabiki wa FA toka anatoa Ingekua vipi hajawahi niangusha!
mwisho nasema:Wasanii wa zamani hawakua na platform na management nzuri za kuwasimamia ili muziki wao uwalipe na waendelee kuhit,tofauti na sasa!
 
Back
Top Bottom