Hawa ndo mashujaa waliouawa kwa kupinga ukoloni na kujitoa muhanga kuilinda ardhi ya Tanganyika

Hawa ndo mashujaa waliouawa kwa kupinga ukoloni na kujitoa muhanga kuilinda ardhi ya Tanganyika

1. Mangi Meli wa Wachaga (Aliuawa mwaka 1900)

Kiongozi wa Wachaga wa Kilimanjaro aliyepinga ukoloni wa Wajerumani.

Alikamatwa na Wajerumani, akahukumiwa na kunyongwa hadharani Moshi

Hadithi zake zimeendelea kuenziwa kama shujaa wa mapambano dhidi ya ukoloni.

2. Kinjeketile Ngwale (Aliuawa mwaka 1905)

Kiongozi wa kiroho na kijeshi wa Vita ya Maji Maji (1905-1907). Aliwahamasisha watu kwa imani ya maji ya uchawi ("maji maji") ambayo ilisemekana ingeweza kuzuia risasi za Wajerumani. Alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani mwaka 1905.

3. Chief Songea Mbano (Aliuawa mwaka 1906)
Kiongozi wa kabila la Wangoni aliyeshiriki katika Vita ya Maji Maji.
Alikamatwa na Wajerumani, akateswa na hatimaye kunyongwa hadharani pamoja na viongozi wengine wa Wangoni.
Baada ya kuuawa, jina lake likawa sehemu ya mji wa Songea

4. Mkwawa wa Wahehe (Aliuawa mwaka 1898)
Chifu wa Wahehe aliyepambana na Wajerumani kwa miaka mingi, akiwashinda katika Vita ya Lugalo (1891). Baada ya mashambulizi makali ya Wajerumani, alikataa kukamatwa na akajitoa uhai mwaka 1898.

Kichwa chake kilikatwa na kupelekwa Ujerumani, lakini baadaye kilirejeshwa Tanzania mwaka 1954.

Viongozi hawa walikuwa sehemu ya harakati kubwa ya upinzani dhidi ya utawala wa Wajerumani, na wengi wao waliuawa kwa njia ya ukatili kama kunyongwa, kupigwa risasi, au mateso makali.

Kanda pendwa walikua wapi enzi hizo wanaume wa shoka wapo mzigoni
Ongeza JPM
 
Wanavyodai wenyewe Nyerere katolewa porini huko na wazee wa Kariakoo kahifadhiwa nyumbani kwa Sykes for years.
So wanavyodai,Nyerere mwenyewe kaandika yote haya kwenye vitabu vyake vinavyoelezea historia yake
 
Kwa kweli wakifufuka watashangaa sana,waliokuwa wanakataa leo vijukuu vyao wanaenda wenyewe huko ulaya kuwabebeleza waje kuwekeza.
2.waliwagomea kwenda Ulaya,leo vijana wanajipeleka wenyewe,badala wake wajenge nchi yao ije kuwa kama huko Ulaya.

Aliyemloga mtu mweusi alituweza
 
3. Chief Songea Mbano (Aliuawa mwaka 1906)
Kiongozi wa kabila la Wangoni aliyeshiriki katika Vita ya Maji Maji.
Alikamatwa na Wajerumani, akateswa na hatimaye kunyongwa hadharani pamoja na viongozi wengine wa Wangoni.
Baada ya kuuawa, jina lake likawa sehemu ya mji wa Songea

01 October 2025

Urithi wa utawala wa kikoloni wa kikatili wa Ujerumani barani Afrika | Shahidi Documentary​


View: https://m.youtube.com/watch?v=yq2hHZLssL4

Wakili John Mbano yuko kazini. Baba wa Babu yake, mzee Songea Mbano, kiongozi wa Wangoni kusini mwa Tanzania, aliuawa na jeshi la kikoloni la Wajerumani mwaka 1906, na kichwa chake kilipelekwa Ujerumani kwa ajili ya utafiti wa kisayansi wa kibaguzi. Vizazi vya familia vimeandamwa na kiwewe hiki hadi leo. John na mkewe, Cesilia, mwalimu wa historia, wanaanza safari ya kubadilisha maisha hadi Berlin kutafuta fuvu la babu yao, wakitumaini kwamba linaweza kuzikwa kwa heshima huko nyumbani. The Empty Grave ni filamu ya hali halisi ya Agnes Lisa Wegner na Cece Mlay.
 
Umekuwa mbaguzi.
Mango Meli na Mkwawa umewataja machifu wa watu gani au toka maeneo gani.
Tutajie akina Kinjikitile Ngwale na Chief Songea wa wapi au waliongoza watu wa wapi?
 
Wote hao walitandikwa

Ni chifu moja tu alieweza, Chief Malkia Liti wa Singida,
We hujasoma battle la Mbeya huko Rungwe milimani,wajerumani walichapika vizuri tu na mamluki wao toka wahehe,na wangoni walichapwa mpk wakaomba poo maridhiano.
Ndio kuanza kushirikiana kujenga makanisa.
 
Back
Top Bottom