Hawa ndo mashujaa waliouawa kwa kupinga ukoloni na kujitoa muhanga kuilinda ardhi ya Tanganyika

Hawa ndo mashujaa waliouawa kwa kupinga ukoloni na kujitoa muhanga kuilinda ardhi ya Tanganyika

Maendeleo kwako wewe ni kitu gani.Ni hizi takwimu wanatoa NBS?Ni ustawi wa mtu(kukizi mahitaji yake?Basic needs(food,shelter and housing)) au ni massive investment au kwako maendeleo ni kitu gani?
,😁😁
 
1. Mangi Meli wa Wachaga (Aliuawa mwaka 1900)

Kiongozi wa Wachaga wa Kilimanjaro aliyepinga ukoloni wa Wajerumani.

Alikamatwa na Wajerumani, akahukumiwa na kunyongwa hadharani Moshi

Hadithi zake zimeendelea kuenziwa kama shujaa wa mapambano dhidi ya ukoloni.

2. Kinjeketile Ngwale (Aliuawa mwaka 1905)

Kiongozi wa kiroho na kijeshi wa Vita ya Maji Maji (1905-1907). Aliwahamasisha watu kwa imani ya maji ya uchawi ("maji maji") ambayo ilisemekana ingeweza kuzuia risasi za Wajerumani. Alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani mwaka 1905.

3. Chief Songea Mbano (Aliuawa mwaka 1906)
Kiongozi wa kabila la Wangoni aliyeshiriki katika Vita ya Maji Maji.
Alikamatwa na Wajerumani, akateswa na hatimaye kunyongwa hadharani pamoja na viongozi wengine wa Wangoni.
Baada ya kuuawa, jina lake likawa sehemu ya mji wa Songea

4. Mkwawa wa Wahehe (Aliuawa mwaka 1898)
Chifu wa Wahehe aliyepambana na Wajerumani kwa miaka mingi, akiwashinda katika Vita ya Lugalo (1891). Baada ya mashambulizi makali ya Wajerumani, alikataa kukamatwa na akajitoa uhai mwaka 1898.

Kichwa chake kilikatwa na kupelekwa Ujerumani, lakini baadaye kilirejeshwa Tanzania mwaka 1954.

Viongozi hawa walikuwa sehemu ya harakati kubwa ya upinzani dhidi ya utawala wa Wajerumani, na wengi wao waliuawa kwa njia ya ukatili kama kunyongwa, kupigwa risasi, au mateso makali.

Kanda pendwa walikua wapi enzi hizo wanaume wa shoka wapo mzigoni
Kinjekitile alisababisha tunachekwa hadi leo. Aidha, kimsingi Wazungu walikuwa ni kama wasimamizi wa vita, ila Waafrika walipogana wao kwa wao.
 
Mme
Mjerumani kasaini mikataba ya amani na mtemi Kahigi au hulijui hili(soma historia kidato cha tatu wanafundisha).Kipindi hicho nadhani mababu zenu ata hizi a,e,i,o,u walikuwa wanaona mazingaombwe

Mjerumani kakuta tayari wahaya wana practise formal education(uliza Rubya seminary ni ya lini?(utapewa jibu la 1905 lakini ilikuepo kabla hata mkutano wa Berlin kufanyika))
Mmekuja watu wenye majigambo mengi ila wenye mji wa hovyo kabisa wa BK.
 
Wahaya wamekuwa civilised kabla hata hao wakoloni kufika.Hizo translation za text za bible kwenda lugha ya kihaya unadhani alifanya mkoloni? Organisation ya holy mass katika mtindo wa kihaya alifanya mkoloni sio?(Hii pekee inakutosha kuona earliest civilisation in buhaya kingdom before intruders)

We managed to trade with people of Buganda kingdom(do you know how far it is?just interregion trade).Traveling long distance by that time with advanced means of transportation to exchange advanced technologies and commodities.We were civilised am telling you brother
Translation za bible kwenda kwenye vernacular languages hapa tz zimefanyika uhayani tu!!??
 
Translation za bible kwenda kwenye vernacular languages hapa tz zimefanyika uhayani tu!!??
Sijui kiongozi hapa naongelea before colonisation japo nliwahi kusikia wanyakyusa pia lakini hii ni after uhuru
 
Wazee wa kariakoo hawana lolote wala si chochote.
Walimhifadhi Mwalimu mjini; wakampa uongozi wa harakati; wakamsafirisha kwenda UNO; wakamchangia harakati za uhuru; wakamzindika; wakamtawaza rais wa Tanganyika.
 
Beira,
Wapo Waislam labda kama mtu hajui historia zao.
Yupo Kinjiketile Ngwale, Abdulrauf Songea Mbano, Mtwa Abdallah Mkwawa.

Walisahauliwa ni Khadija Mkomanile, Abushiri bin Salim Al Harith, Omar Kinyalanyala na Hassan Omar Makunganya.

Makamanda Waislam walionyongwa na Wajerumani waliletewa Padri Yohannes Hafliger kutoka Peramiho aje kuwabatiza na walipozikwa majina yao ya Kiislam yakafutwa yakaandikwa yale majina waliyopewa na Hafliger.

Hii historia ni ndefu inataka wasaa kuieleza yote kwa ukamilifu lakini tosheka na hayo niliyoeleza hapo juu.

Nyongeza:
Nawashukuru ndugu zangu kupita kiasi.

Kila siku wananikumbuka na kuniletea vitabu ama wavitume au kuja wenyewe maktaba kwa miguu yao.
Abdulaziz Ali Khamis yeye anatoka Mombasa.

Mara kwa mara huja nitembelea Maktaba.
Safari hii alikuja Tanzania akafika hadi Songea kutembelea Makumbusho ya Vita Vya Maji Maji.

Hapo kuna duka la vitabu basi akaninunulia kizigo cha vitabu kaniletea.

Kitabu kilichogusa moyo wangu ni hicho nilichoshika kitabu cha Nduna Abdulrauf Songea Mbano kiongozi wa Wangoni.

Wanahistoria hupenda kumwita Songea Mbano wakaliacha jina la Abdulrauf.
Mimi hupenda kumwita kwa majina yake kamili: Nduna Abdulrauf Songea Mbano.

Alinyongwa na Wajerumani na kukata kichwa chake wakakipeleka Ujerumani.

View attachment 3283257
Bora walikubali kubatizwa walikimbia ghilba za mabikira 72.
 
Walimhifadhi Mwalimu mjini; wakampa uongozi wa harakati; wakamsafirisha kwenda UNO; wakamchangia harakati za uhuru; wakamzindika; wakamtawaza rais wa Tanganyika.
Mwl Nyerere anahifadhiwa vipi mtu kapita viunga vya Makerere Kampala & UK 🇬🇧!.
 
Wanavyodai wenyewe Nyerere katolewa porini huko na wazee wa Kariakoo kahifadhiwa nyumbani kwa Sykes for years.
Yeyote aweza kusema atakacho .

The question is ithibati iliyo thibitika ni ipi?

Ithibati yaweza kuthibitika ,thibitishwa kuelekea mrengo Fulani...

Uongo ukisemwa sana unakuwa ukweli..

Hivi unajua ya kuwa wapo wenye uwezo wa kumiliki ithibati iliyo thibitishwa .. wakaimanipulate to their Intersests??


Noam Chomsky my friend
 
Back
Top Bottom