1. Dr. nyambura moremi
View attachment 1755243
Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.
Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.
Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.
Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.
2. Dr Mwele Ntuli malecela
View attachment 1755245
Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR).
Kipindi kumeibuka na ugonjwa usiojulikana uliohusishwa na ugonjwa wa homa ya dengue jijini Dar es Salaam, Dr mwele chini ya taasisi aliyoiongoza(NIMR) walifanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika ndipo akatangazia umma ili watu wachukue tahadhari ya kujikinga na kujilinda dhidi ya ugonjwa huo. Lakini kitendo hicho kilionekana kuwa chukizo kwa hayati magufuli akaamua kumfukuza kazi huku akimtuhumu kwamba anatumiwa na mataifa ya nje (mabeberu kama alivyopendelea kuwaita) bila ushahidi wowote wa kuthibitisha kauli yake hiyo.
Hata hivyo inasadikika kuwa kutumbuliwa kwa Dr mwele ulikuwa ni mwendelezo wa chuki binafsi ya hayati magufuli na familia ya malecela kwani hapo kabla aliwahi kumfuta kazi ya ukuu wa mkoa mama yake mwele( anne kilango malecela) kipindi cha sakata la watumishi hewa.
3. Dr Ave maria semakafu
View attachment 1755246
Alikuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.
Alitumbuliwa kwa kosa la kutaka kuboresha elimu ambapo awali alitangaza kufuta mafunzo na ualimu wa cheti jambo ambalo hayati magufuli aliita ni uamuzi wa kipumbavu na baadaye akamfuta kazi.
Hata hivyo, Dr semakafu alitumbuliwa kimakosa kutokana na sababu za kisiasa kwani kwa wakati huo kampeni zilikuwa zimepamba moto hivyo hayati magufuli alifikia uamuzi wa kumfukuza Dr semakafu kama njia ya kujitafutia kura kwa wananchi ila suala la kuboresha elimu ni miongoni mwa sera zilizoko kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) 2020-2025 ambayo hayati mwenyewe alizunguka kuinadi nchi nzima.