Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Yani Bob alikufa na mika 36 tuu jamani lakini aliacha watoto kadhaa si haba
Bob Marley alikufa akaacha watoto 12 wanaotambulika kisheria. Aliacha watoto wa kiume 7, na wa kike 5.
Watoto wa kiume alioacha ni πŸ‘‡

1) Ziggy Marley
2) Damian Marley
3) Rohan Marley
4) Stephen Marley
5) Ky- Mani Marley
6) Julian Marley
7) Robert Marley

Na wa kike alioacha ni πŸ‘‡

1) Cedalla Marley
2) Sharon Marley
3) Stephanie Marley
4) Karen Marley
5) Makeda Jahnesta Marley

Hao ni wale wanaofahamika kweny public, sasa haijulikani kama pembeni aliacha wangapi.
 
Alikua shababi
 
Bruce nae alikufa mdogo sana nini kilimuua huyu mwamba?
Huyu mwamba Bruce Lee inasemekana aliwekewa sumu, japo mpaka leo haijathibitishwa aliwekewajwe wekewajwe sumu? Na nani? Na kwa malengo gani?
Kila mtu anaongea lake, ila mwamba na yey aliacha watoto wawili. Wa kiume mmoja alieitwa Brandon Lee (marehemu) na wa kike mmoja anaeitwa Shannon Lee.
 
Alikua shababi
Huyu kila kiungo chake kilikuwa na kazi yake.
I) kichwa kilitunga nyimbo
2) mikono iliandika
3) mdomo uliimba
4) kiuno kilileta watoto πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
5) miguu ilitembea na kucheza reggae kwa style yake mwenyewe.
 
Mnamuachaje ndala kasheba aisee
Ya mwamba alikuwa vizuri ila bado alikumbana na vichwa vikubwa kama kina Marijani Rajabu, Mbaraka Mwinshehe nk. Hao niliowataja walikuwa ni moto wa kuotea mbali sana.
Ukifuatilia kwa makini utagundua kuna mambo mengi yalioimbwa na Marijani ndio yanatokea sasa.
Jamaa ni kama vile alikuwa akitabiri mambo mengi na yakatokea na zingine ni visa vya kweli vilivyomgusa yeye binafsi, rafiki au ndugu zake, so ni vigumu ndala kuweka mguu kwa huyu mwamba wa Jojina, usia wa baba, mwanameka, sadiki, masudi, ndoa ya mateso, dunia uwanja wa fujo nk.
 
[emoji15] Hapa namuweka Shaaban Yohana "WANTED huyu mwamba kwa TZ ni habari nyingine.
 
[emoji15] Hapa namuweka Shaaban Yohana "WANTED huyu mwamba kwa TZ ni habari nyingine.
Ya ni kweli, huyu mwamba nae aliacha legacy kubwa kwenye tasnia ya mzikj wetu. RIP Shaban Wanted.
 
Hapo kwa Bob Male
nadhani umemsahau Lucky Dube alivivaa na vikamtosha kabisa sema wenye roho mbaya wanapitia kipindi cha pili dakika ya 89.5
 
Hapo kwa Bob Male
nadhani umemsahau Lucky Dube alivivaa na vikamtosha kabisa sema wenye roho mbaya wanapitia kipindi cha pili dakika ya 89.5
Lucky alifanya mambo makubwa kweny mziki wa reggae mpaka waJamaika walianza kumchukia bila sababu. Waliona jamaa anawapoteza katika ulimwengu wa reggae.
 
Wengine wote sawa, ila kwa 2Pac umechemka.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hakuna king wawili kwenye tasnia. Hapo kwenye mpira tayari kaishabana mzee Pele wa brazil toka miaka hiyo. Hata waliotaka na Maradonna aongezwe walichemsha, sembuse ije kuwa bwana mdogo Mesi??
RIP gwiji na mfalme wa mpira wa miguu Edson Arantes do Nascimento aka "Pele". Dunia itakukumbuka kwa umahiri wako wa kulisakata kabumbu na kushinda mabao mengi zaidi katika historia ya mchezo huu wa mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…