Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Pambano la pili 2005 . Alipomn'gata skio Holyfield
[/QUOTE]
Mkuu hivi kweli wewe ulikuwepo miaka hiyo Mike anapigana na Holyfield au ulihadithiwa. Nauliza hivyo kwa sababu maelezo yako unayoyatoka yako mbali mbali na uhalisia. Tyson alimng'ata Holyfield mnamo miaka ya katika ya 1996 au 1997. Kwanza kwa upand wang nakumbuka ilikuwa 97 japo tar na mwezi siukumbuki na nililifuatilia pambano lile mwanzo mwisho.
Mapambano karibia yote aliyopigana Tyson miaka 90 mimi niliyafuatilia mwanzo mwisho japo nilikuwa sijabelehe lkn akili ninayo na kufaham kila kila kilichoendelea mkuu. Hiyo 2005 ni juzi Tyson tayari alikuwa ashajiweka mbali na mambo hayo.
 
Pambano la pili 2005 . Alipomn'gata skio Holyfield.
Mkuu hivi kweli wewe ulikuwepo miaka hiyo Mike anapigana na Holyfield au ulihadithiwa. Nauliza hivyo kwa sababu maelezo yako unayoyatoka yako mbali mbali na uhalisia. Tyson alimng'ata Holyfield mnamo miaka ya katika ya 1996 au 1997. Kwanza kwa upand wang nakumbuka ilikuwa 97 japo tar na mwezi siukumbuki na nililifuatilia pambano lile mwanzo mwisho.
Mapambano karibia yote aliyopigana Tyson miaka 90 mimi niliyafuatilia mwanzo mwisho japo nilikuwa sijabelehe lkn akili ninayo na kufaham kila kila kilichoendelea mkuu. Hiyo 2005 ni juzi Tyson tayari alikuwa ashajiweka mbali na mambo hayo.
 
Pambano la pili 2005 . Alipomn'gata skio Holyfield
Mkuu japo post ya #226 haikuja vizuri lkn huu ndio ukweli halisi wa pambanao la Tyson na Holyfield. Mimi nilisahau mwez tu na tar lkn bahat nzuri nimeipata hapa
 

Attachments

  • Screenshot_20220830-093333.jpg
    Screenshot_20220830-093333.jpg
    44.7 KB · Views: 11
Huu uzi bila kumtaja Pele mchawi wa soka unapungua ladha
Pele na Mohammad Ali ndio watu waliotajwa sana ktk huu uzi mkuu. Ukibahatika kuchungulia chungulia comment utaona. Mimi na baadhi ya wafuatiliaji wa soka toka miaka hiyo tumekubaliana kuwa Pele ndio king wa mpira, ila kuna mwama amebisha na kudai king ni Mesi so ubishi ukaanzia hapo.
 
Hakika umeandika maneno mazuri sana mkuu. Muziki wetu ulianza kumezwa baada ya ujio wa kina Mr 11 (sugu) mnamo mwanzoni mwa miaka ya 90.
Jamaa alikuwa anasikiliza nyimbo za kina 2Pac afu anazibadilisha kwa kiswahili, vijana wanafurahi wanaona ujanja. Ikaenda ikaenda mwisho vijana wengi wakaingia kwenye mkumbo huo wa muziki wa wenzetu, na kuuendeleza hadi leo. Wanachofanya ni kubadili majina tu ili uonekane ni mziki wa nyumban.
Mara hip hop bongo, mara bongo fleva nk.
Wengine waliotuingiza chaka japo sio ile kivile ni hawa sijui twanga pepeta ya kina marehemu banza, ali choki, muumin mwinjuma nk.
Nao hiyo singeli ndo afadhali kidogo imesimama ktk nafasi ya mnanda au mchiriku kama wengi tulivyokuwa tunaita miaka hiyo. Mziki huu ulionekana wa kihuni, japo baadae baada ya wale vijana wa garikubwa kule mw/nyamala kuja na vibao vya akili kama vile raisi wetu hodari Ali Mwinyi, uko wapi mama nk.
Dah mziki wetu ushaondoka na ma legend wetu.

Haya huwa ni mawazo ya kizamani sana mkuu

Mziki wetu wa asili bado upo tena sana tu kwenye ngoma zetu za kiasili....... mdumamge mganda sindimba nk nk


Hii miziki ya kisasa itaendelea kubadilika hadi ukamilifu wa dahari na sio sahihi kuwalaumu wanamuziki wakati wao wanaangalia walaji wao wanataka nini

Au wewe unadhani wakongo ndio waligundua magitaa na drums...... ni hatua kwa hatua
 
1) Mohammad Ali
2) Bob Marley
3) Bruce Lee
4) Michael Jordan
5) Michael Jackson
6) 2pac Shakur
The Greatest of All Time- GOAT

Tukija Tanzania tuna hawa chini:
1) Julius Nyerere - Uhuru wa nchi yetu.
2) Marijani Rajabu - mziki
3) Madaraka Selemani - soka
4) Malkia Khadija Kopa - taarab

Hapo kwa Nyerere rudi kasome upya historia ya nchi hii mkuu
 
😂😂😂 nilikuwa nazungumzia tasnia ya michezo na music mkuu. Yuda naona ni upande wa watafuta pepo na kwenda mbinguni.
Hapana Yuda Iskariote yuko upande wa wahasibu. Hajawahi kupatikana mhasibu mwingine tena wa kuweza kuvaa viatu vyake hadi leo
 
Je ni kipi cha maana alichofanya wakati huo?
Ndio maana nimekwambia uwe unatafuta facts, sio unaleta stori. Messi kaanza kucheza Barca A akiwa na miaka 17 na impact yake ilianza kuonekana mapema tu. Niambie hao uliowataja walianza kuchezea timu kubwa wakiwa na umri gani?
 
Mkuu mbona kuna wachezaji wengi wakubwa walianza kucheza na umri mdogo. Lkn tofauti ni kwa vile wenyew walianza kuchezea club zingine sio barca.
Kumbuka Mesi amekulia ktk mji barcelona kwahiyo ilikuwa rahisi wao kumuona. Wengine walikuwa ktk nchi tofauti kwahiyo ndio maana barca ilichelewa kuwaona.
 
Mkuu mbona kuna wachezaji wengi wakubwa walianza kucheza na umri mdogo. Lkn tofauti ni kwa vile wenyew walianza kuchezea club zingine sio barca.
Kumbuka Mesi amekulia ktk mji barcelona kwahiyo ilikuwa rahisi wao kumuona. Wengine walikuwa ktk nchi tofauti kwahiyo ndio maana barca ilichelewa kuwaona.
 
Ndio maana nimekwambia uwe unatafuta facts, sio unaleta stori. Messi kaanza kucheza Barca A akiwa na miaka 17 na impact yake ilianza kuonekana mapema tu. Niambie hao uliowataja walianza kuchezea timu kubwa wakiwa na umri gani?
Mkuu nimekujibu kweny post namb #237
 
Steven kanumba- filamu
Diamond platnum- muzik
Bwana yule- Siasa
Luckdube- reggae
Mwamposa- upigaji/utapel wa dini
Babu wa loliondo- upigaji
 
Mkuu mbona kuna wachezaji wengi wakubwa walianza kucheza na umri mdogo. Lkn tofauti ni kwa vile wenyew walianza kuchezea club zingine sio barca.
Kumbuka Mesi amekulia ktk mji barcelona kwahiyo ilikuwa rahisi wao kumuona. Wengine walikuwa ktk nchi tofauti kwahiyo ndio maana barca ilichelewa kuwaona.
Bado unathibitisha kwamba huna facts. Messi kakulia Rosario, Argentina. Barcelona walifunga safari mpaka huko kwenda kumchukua akiwa na umri wa miaka 13 na kumleta Spain. Ina maana waliona ana something special.
 
Yani Bob alikufa na mika 36 tuu jamani lakini aliacha watoto kadhaa si haba
 
Za asubuhi wakuu, leo nakuja na makala ya watu maarufu duniani, ambao wameacha alama kubwa katika tasnia zao na mpaka leo hakuna alietokea kuziba mapengo yao.

1) Mohammedi Ali
Huyu ni bingwa, mbabe na mtemi wa masumbwi ulimwenguni kote. Mohammed Ali ambae alizaliwa 17 January 1942, huko Louisville, Kentucky Marekani na kufariki 3 June 2016, huko Scottsdale, Arizona Marekani. Alikuwa ni bondia wa pekee kuufanya mchezo huo uwe na wapenzi na waangaliaji wengi ulimwenguni.

Licha ya kwamba mchezo huo ulikuwepo maelfu ya miaka kabla ya ujio wake Ali, lkn ni yeye ndio aliefanya watu waanze kuupenda zaidi mchezo huo na kuchukua nafasi ya pili kwa kupendwa duniani baada ya mchezo wa mpira wa miguu. Ali ambae alikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki ulingo, kukwepa ngumi, na mwepesi wa kupiga ngumi za haraka haraka. Lakini pia alikuwa na mbinu nyingi za kuweza kumchosha na kummaliza kbs mpinzani wake wakati wowote alioutaka yeye ulingoni.

Ali alikuwa na uwezo wa kumsogezea mpinzani sura, lkn utashangaa hadi round nzima inaisha bila mpinzan wake kufanikiwa kumpiga ngumi hata 1 tu usoni (kama tuonavyo pichani) sometimes unakuta mpinzani wake anarusha ngumi (kota) na kuanguka mwenyewe, huku Ali akimtizama kwa dharau 😂😂🤣🤣

Pamoja na yote lkn kama ilivyo michezo mingine na yey kuna muda alikuwa anapoteza baadhi ya mapambano pia, aidha kwa kutokana na mchoko wa mazoezi makali anayokuwa amefanya kabla ya pambano nk. Toka Ali alipostaafu ngumi mpaka kifo chake, hakuna bondia ambae ashawahi kufikia rekodi ya upiganaji wake na vituko vyake awapo ulingoni na nje ya ulingo.

Mabondia wengi kama kina Mike Tyson, Evander, Lenox Lewis na wengineo walikuwa wanakwenda kumuona na kupata mbinu mbali mbali za kupigana ulingoni kupitia mfalme huyo wa ngumi ulimwenguni. Huyu ndio Mohammed Ali alieacha alama kubwa ktk mchezo huo maarufu wa ngumi duniani. Hakuna na hatotokea Mohammed Ali mungine, Never.
Mungu ailaze roho ya huyu Legend mahali pema peponi.

View attachment 2335340

2) Bob Marley
Bob Marley alizaliwa 6 Feb 1945, huko Nine Mile, Jamaica, na kufariki 11 May 1981, huko Florida Marekani.

Alipozaliwa aliukuta mzikiwa reggae ukiwa ulimwenguni miaka na miaka. Lkn kwa kipaji chake na uwezo wake akaanza kuleta mabadiliko makubwa katika mziki huo, hadi kufikia hatua ya kusikilizwa na viongozi wakubwa wa nchi mbali mbali. Japo kulikuwa na waimbaji wengine wakubwa kama kina Peter Tosh, Burn Spear nk, lkn ni yeye Bob Marley ndio aliefanya reggae ipendwe na walio wengi. Hadi anakufa Bob Marley aliacha muziki huo ukiwa na mamilioni ya wasikilizaji ulimwenguni.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

View attachment 2335341

3) Bruce Lee
Bruce Lee alizaliwa 27 Nov 1940, huko San Francisco, California Marekani na kufariki 20 July 1973 huko Kow loon Tong, Hong Kong.

Bruce alizaliwa na kuukuta mchezo wa kung fu au karate ulimwenguni. Lakini kwa kipaji alichozaliwa nacho, alianza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mchezo huo hadi kushawishi mamilioni ya watu ulimwenguni kuupenda na kuanza kuufuatilia mchezo huu. Bruce alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na hisia za adui na kujua ni wapi atapopiga lazima adui atakaa tu hata awe na mwili kama jumba.

Ikafika kipindi watu wakamshauri ajiunge kwenye tasnia ya uigizaji ili kuwavutia watu zaidi kuupenda mchezo huo, lkn pia kujifunza baadhi ya mbinu za upambanaji kupitia movie zake. Mpaka toka Bruce afariki mpaka leo bado anapewa heshima kubwa na magwiji wa mchezo huo wakiwemo wacheza sinema kama vile Jackie Chan, Jet Lee nk. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

View attachment 2335338

Wanaofuatia ni 👇
4) Michael Jackson king wa Pop na mitelezo.

5) 2pac Shakur king wa Hip hop aliekuwa haiogopi serikali ktk kuwatetea wamarekani weusi wenzake na jamii nyingine zilizobaguliwa nchini Marekani, pia alipambana sana na polisi kuhusu unyanyasaji wowote uliofanywa na jeshi hilo kwa vijana mbali mbali hadi alipouwawa. Aliwahi kuwa na kesi ya kuwashambulia polisi wawili na bunduki, baada ya 2pac kupita sehem na gari aliwakuta polisi wakiwa wamemfunga pingu mtu mweusi huku wanampiga, kitendo kile kilimuuzi 2pac ndipo alipoamua kutoa bastola yake na kuwashambulia polisi, japo baadae polisi wale waliwahishwa hospital na kupona.
Katika kesi ile 2pac hakuhukumiwa baada ya kuonekana kuwa wale polisi walikuwa na makosa ya kiutendaji kwa mtuhumiwa waliekuwa wamemkamata.
Mungu awalaze roho zao mahali pema peponi.

6) Michael Jordan
Mzee wa kudumbukiza kikapuni. Huyu alikuwa na uwezo wa kuruka juu zaidi na kuonekana kama ameganda kwa sekunde kadhaa hewani kabla ya kutia mpira kapuni na kushuka chini. Toka astaafu bado hajapatikana Jordan mungine, japo bwana mdogo hayati Kobe Bryant alijitahidi kwa namna fulan, lkn bado hakufikia kule alipofikia mzee wa kazi.

View attachment 2335342

Hawa ni baadhi ya watu ambae mpaka leo viatu vyao viko wazi, havijapata wa kuvivaa vikawatosha.
Amesahaulika mzee Majuto katika tasnia ya uchekeshaji. RIP mzee wetu Majuto Athumani.
 
Back
Top Bottom