Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Naongezea Diblo Dibala, Dally Kimoko, bila kumsahau Francoo wa Mario
Naongezea Diblo Dibala, Dally Kimoko, bila kumsahau Francoo wa Mario
Franco Luambo Makiadi huyu hakuwa na mpinzani kwa kweli. Hata hao kina Madilu, Papa Wemba, Pepe Kale, Diblo na wengineo walijifunza mengi kupitia mziki wake.
Dah.. rip Luambo
 
Salute mkuu, kwa Marijani Shaaban(rip)nipo nawe 100%,Kumbuka ule wimbo wa mwanameka ulitokea kwenye swahili paper, yeah nchi hii kuna mtu alituelekeza siko, nchi haina mziki wake wa kuipambanua labda singeli!,hawa akina almasi, tembo etc etc wanakesi ya kujibu, wamevuruga mila na utamaduni wetu,kenge kabisa hawa
 
Hakika umeandika maneno mazuri sana mkuu. Muziki wetu ulianza kumezwa baada ya ujio wa kina Mr 11 (sugu) mnamo mwanzoni mwa miaka ya 90.
Jamaa alikuwa anasikiliza nyimbo za kina 2Pac afu anazibadilisha kwa kiswahili, vijana wanafurahi wanaona ujanja. Ikaenda ikaenda mwisho vijana wengi wakaingia kwenye mkumbo huo wa muziki wa wenzetu, na kuuendeleza hadi leo. Wanachofanya ni kubadili majina tu ili uonekane ni mziki wa nyumban.
Mara hip hop bongo, mara bongo fleva nk.
Wengine waliotuingiza chaka japo sio ile kivile ni hawa sijui twanga pepeta ya kina marehemu banza, ali choki, muumin mwinjuma nk.
Nao hiyo singeli ndo afadhali kidogo imesimama ktk nafasi ya mnanda au mchiriku kama wengi tulivyokuwa tunaita miaka hiyo. Mziki huu ulionekana wa kihuni, japo baadae baada ya wale vijana wa garikubwa kule mw/nyamala kuja na vibao vya akili kama vile raisi wetu hodari Ali Mwinyi, uko wapi mama nk.
Dah mziki wetu ushaondoka na ma legend wetu.
 
It's so sad mkuu,nyimbo zetu hata majirani zetu hasa DRC walikua wanazipenda na sometimes wanazipiga kama uke wimbo wa nairobi &Lagos by nite, solo la karenga lilikua linakabana koo na solo la mzee Franco, ushenzi ulioingia hii late 90s ni vurugu tupu, kipindi kokote ukiwa duniani wimbo ukipigwa kwenye radio huulizi unajua hiyo ni Tanzanian music na hao ni msondo...eti leo tunapiga amapiano!!,DJ Tira, Osikodo, etc ndio asili yao na ndio music wao ambao ni mwendelezo wa kwaito wapige nini?,eti nipo polokwane nasikiliza wimbo wa amapiano uliopigwa na Tembo from Tanzania!!,kenge kabisa hii
 
Tx moshi alitulia, mwishoni alitunga vitu noma saana
 
Ni simanzi sana mkuu, yani uliyoandika bado nayapa 100% kwa vile ndio uhalisia wenyewe. Nakumbuka hata wimbo wa Kilwa jazz uliwahi kurudiwa na bendi fulan ya Congo jina la bendi nimelisahau.
Afu wasanii wa sasa hivi ndo hovyo kbs, hawana pumzi, hawajui kufuata mziki unavyokwenda yani wao muda wote mtu kashika mbele ya zipu yake anazunguka zunguka ukumbini utafikiri ni mtu aliebanwa na mkojo kumbe ndo style yao ya ku perfom stejini 😂😂🤣🤣
 
😂😂😂 hakuna king wawili kwenye tasnia. Hapo kwenye mpira tayari kaishabana mzee Pele wa brazil toka miaka hiyo. Hata waliotaka na Maradonna aongezwe walichemsha, sembuse ije kuwa bwana mdogo Mesi??
Wakati Pele anacheza soka hakukua hata na sheria ya Offside,alikua anatupia tu kambani,

MESSI ndio mfalme wa soka hata makocha wakubwa wanatambua hilo,

Ila ruksa kwako kuamini kua Pele ndio King.
 
Wakati Pele anacheza soka hakukua hata na sheria ya Offside,alikua anatupia tu kambani,

MESSI ndio mfalme wa soka hata makocha wakubwa wanatambua hilo,

Ila ruksa kwako kuamini kua Pele ndio King.
Mkuu sikatai kwamba Messi yuko mbali sana kimpira ukimlinganisha na Pele wa miaka ile.
Pele hakuwahi kufanya yale yaliofanywa na ma legend wengine kama vile Ronaldo de Lima, Ronaldinho, Zinedine Zidane, Bebeto, mkongwe Rivaldo nk.
Lkn kwa vile tasnia ya soka imeamua kumuona yey anafaa kupewa heshima aliyopewa, basi ndo ishakuwa hivyo hivyo.
Ingekuwa utambulisho huo unabadilika badilika basi, kina Maradonna, Ronaldo de Lima nk wangekuwa ma king ktk nyakati tofauti tofauti maana kila mmoja kafanya makubwa kwa nyakati zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…