Hawa Standup Comedy wa Tanzania, nyie wana JF wanawachekeshaga?

Hata Mimi hata Huwa siwaelewi, itakuwa kweli kuna tatizo la afya za akili nchini...kuna wakati huoni kinachochekesha ila watu wanachoka tu. Ni sawa ni kule bungeni kuna wakati huoni pointi ila unasikia wabunge wakigonga meza yaani shida ni kubwa mno ndugu yangu. Zaidi Bora wale wanaoogelea kwenye maji kuliko kwenda kusikiliza hao jamaa
 
Kuna yule Steve Mweusi ukimkuta mahali yupo kwenye stage unaweza kumsikiliza nusu saa nzima ukajua ni hotuba kumbe mwenzako ndo yupo kuchekesha hapo.....
 
Mkuu wabongo wengi wana km kamtindio ka ubongo,,, kuna yule dogo anaitwa Mc Mboneke akijipaka vumbi na kujibinua kamwili kake watu wanaanza kucheka... just imagine
 
Mwanaume hacheki bali ana smile kidogo tu.
Kuna watu wanajua kuchekesha bila kujali jinsia yako. Pia, jokes inategemea mchekeshwaji yupo ktk wakati gani. Kwa mfano zamani Tom na Jery ilikuwa inanichekesha sana lakini kadri ninavyozidi kujua naona ni za kawaida. Stand up comedy unatakiwa uwe na uwezo wa juu sana na akili sana. Pia, kuna wakati content zako zinaisha unahitaji kuziongezea. Kuna watu kadhaa washakamatwa wakikopi jokes kutoka kwa wenzao. Ila mtu akilipia tamasha halafu hacheki huyo ni mjinga. Make your money count Cheka mpka mwisho usipicheka haisaisii hela yako
 
Kuna watu wamezaliwa na vipaji vya kuchekesha ila sio comedians.

1. Makongoro Nyerere
2. Pastor Mgogo
3. Yoweri Museveni
4. Heche
5. Loveness Malinzi Diva (huyu anaongeaga vitu vya kusadikika vinavyokera na kuchekesha hapohapo.)
Heche amekuchekesha wapi
 
πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ’₯
 
Sayansi inasema watu wenye ubongo wenye uwezo mdogo wa ku process (kuchakata mambo) wanacheka kwa urahisi zaidi kuliko wenye ubongo wenye uwezo mkubwa wa ku process mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…