Idofu
Senior Member
- Oct 24, 2022
- 116
- 199
Kwanza nikiri Kabisa Mimi ni Mkristo Kabisa!
Umetokea mtindo wa baadhi ya Wainjilisti kutoa mahubiri kwenye Daladala kila Siku, sasa ninachokijua ni kuwa sisi wakristo Kuna sehemu mahususi kwa ajili ya mahubiri na Mambo mengine ambayo yanaambatana na Mambo ya kidini, Makanisani na Kwenye Jumuia ambazo ni sehemu sahihi ya kuelimishana kwa Mambo yote ya kidini.
Sasa, nakwazika na sio kwa ubaya na hawa Wainjilisti wanaohubiri Kwenye daladala, na je ikitokea dini nyingine wakaja na utaratibu huu huu wa kutoa mahuburi kwenye vyombo vya usafiri wa umma itakuwaje?
Nawaombeni, watumishi wa Mungu mtumie Nguvu nyingi kwenye makanisa yenu, Jumuia na kwenye makongamano ndio sehemu sahihi.