Hawa Wainjilisti kwenye Daladala wako sahihi kweli?

Nakubaliana na wewe!!

Nijuavyo Uinjilisti ni hatua ya kupanda kwenda kwenye uchungaji!!,hawa mafunzo yao yote wanatakiwa wajifunzie Makanisani na sio kwenye daladala !!
Uinjilisti na uchungaji ni huduma mbili tofauti.Ukristo una huduma tano.
Uinjilisti, ualimu,uchungaji,utume na unabii
 
Uhuru wa kueneza dini upo kikatiba. Waache watu, kama ni kero wenye daladala watawazuia.
 
Kwanza nikiri Kabisa Mimi ni Mkristo Kabisa!

Umetokea mtindo wa baadhi ya Wainjilisti kutoa mahubiri kwenye Daladala kila Siku, sasa ninachokijua ni kuwa sisi wakristo Kuna sehemu mahususi kwa ajili ya mahubiri na Mambo mengine ambayo yanaambatana na Mambo ya kidini, Makanisani na Kwenye Jumuia ambazo ni sehemu sahihi ya kuelimishana kwa Mambo yote ya kidini.

Sasa, nakwazika na sio kwa ubaya na hawa Wainjilisti wanaohubiri Kwenye daladala, na je ikitokea dini nyingine wakaja na utaratibu huu huu wa kutoa mahuburi kwenye vyombo vya usafiri wa umma itakuwaje?

Nawaombeni, watumishi wa Mungu mtumie Nguvu nyingi kwenye makanisa yenu, Jumuia na kwenye makongamano ndio sehemu sahihi.
Mimi nilichokuwa nashauli wasitutoze sadaka
 
Mimi hua wakianza makelele yao naweka head phones naweka mzikiwangu wa kisukuma kwa sauti ya juu sana.

HOJA YANGU
Mkuu Ushimen ukiwa umebakiwa na dakika chache kabla ye kwenda mbele ya haki, utawatafuta hao Wahubiri kwa simu na watakuwa hawapatikani.
 
Huu ni usumbufu mkubwa sana kwenye magari ya umma, kuna wakati nilipanda basi halafu mmoja akawa anatoa mahubiri karibu yangu huku anatema mate sana.
 
Mimi hua wakianza makelele yao naweka head phones naweka mzikiwangu wa kisukuma kwa sauti ya juu sana.

HOJA YANGU
Mkuu Ushimen ukiwa umebakiwa na dakika chache kabla ye kwenda mbele ya haki, utawatafuta hao Wahubiri kwa simu na watakuwa hawapatikani.
Mind set
 
Yesu hakusema mahubiri yafanywe ndani ya Kanisa pekee...
Hata hivyo siyo Wakristo pekee, Labda hujakutana tu na wengine.

Marko 16:15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Kwahiyo Yesu aliwapa maelekezo ya kufanya mahubiri mpaka kwenye daladala sio? hii ni kero hakuna cha maelekezo, ata hivyo hayo yalikuwa maelekezo kwa wanafunzi wa Yesu sio hawa wachumia tumbo.

Sema tu sina mamlaka ya kiserikali ila siku nayapata kuanzia hawa wanaofanya maombi kwenye vituo vya daladala mpaka ndani ya hizo daladala watapelekwa kwenye mkono wa sheria.Huu ni usumbufu,kuna kitu wanasema kwamba chumvi ni nzuri ikiwa kiasi lakini kiwango kikiwa kikubwa inakuwa shida pia.

Najua kuna watu hapa wataeleza sijui imeandikwa tutanyanyaswa sana kwa ajili ya huduma.Swali ni kwamba una uhakika huo ufunuo unakuhusu wewe?hawa watu ni washenzi sana ni vile hakuna anayeweza kuona nyuma ya pazia ya hawa wanaojifanya walimu wa dini na wahubiri
 
Kwanza nikiri Kabisa Mimi ni Mkristo Kabisa!

Umetokea mtindo wa baadhi ya Wainjilisti kutoa mahubiri kwenye Daladala kila Siku, sasa ninachokijua ni kuwa sisi wakristo Kuna sehemu mahususi kwa ajili ya mahubiri na Mambo mengine ambayo yanaambatana na Mambo ya kidini, Makanisani na Kwenye Jumuia ambazo ni sehemu sahihi ya kuelimishana kwa Mambo yote ya kidini.

Sasa, nakwazika na sio kwa ubaya na hawa Wainjilisti wanaohubiri Kwenye daladala, na je ikitokea dini nyingine wakaja na utaratibu huu huu wa kutoa mahuburi kwenye vyombo vya usafiri wa umma itakuwaje?

Nawaombeni, watumishi wa Mungu mtumie Nguvu nyingi kwenye makanisa yenu, Jumuia na kwenye makongamano ndio sehemu sahihi.

Mathayo 24:14 SRUV​

Tena Habari Njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
 
Wengine hawana nafasi ya kuingia nyumba za Ibada japo wanatamani hivyo wanapata neno la uzima.
Unafiki mtupu. Walokole wengi wamekuwa matapeli kupitiliza. Wanaofuata misingi ya ulokole ni wachache sana.
 
Daladala zilikuwepo enzi za Yesu, Hebu kuwa makini hata kidogo
Ndio nauliza wao kufanya hivyo wana maana gani? concern yangu hapa sio kujua nini kilikuepo lini na kwanini, nachotaka kusema hapa, kwanini ni wapumbavu kiasi hiki mpaka hawajui ni wapi wafanye hayo mahubiri yao?.Daladala sio sehemu ya kufanyia injili otherwise kuna Yesu mwingine alikupa hayo maelekezo.
 
Kwanza nikiri Kabisa Mimi ni Mkristo Kabisa!

Umetokea mtindo wa baadhi ya Wainjilisti kutoa mahubiri kwenye Daladala kila Siku, sasa ninachokijua ni kuwa sisi wakristo Kuna sehemu mahususi kwa ajili ya mahubiri na Mambo mengine ambayo yanaambatana na Mambo ya kidini, Makanisani na Kwenye Jumuia ambazo ni sehemu sahihi ya kuelimishana kwa Mambo yote ya kidini.

Sasa, nakwazika na sio kwa ubaya na hawa Wainjilisti wanaohubiri Kwenye daladala, na je ikitokea dini nyingine wakaja na utaratibu huu huu wa kutoa mahuburi kwenye vyombo vya usafiri wa umma itakuwaje?

Nawaombeni, watumishi wa Mungu mtumie Nguvu nyingi kwenye makanisa yenu, Jumuia na kwenye makongamano ndio sehemu sahihi.
Tofautisha wainjilisti na wachungaji mkuu
 
Back
Top Bottom