Kwa ngazi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Kama chama tawala kinachoomba ridhaa ya miaka mitano mingine, tukeshe tukiomba kuwa hawa wafuatao wasiende kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu. Wakienda na wakipiga kura, CCM hatutakuwa na chetu. Watapiga kura za uchungu na kuukataa uchungu zaidi. Zitakuwa kura za kuponya mioyo yao kwakuwa watakuwa wametoa maumivu yao kupitia kukataa.
Hawa wakienda kupiga kura, CCM lazima ije na mbinu mbadala kuliko daladala. Wataikataa CCM na wagombea wake mchana peupe. Wataikataa CCM na wagombea wake kwa kutumia kadi zao za kupigia kura, kwenda kwao kupiga kura. CCM itakataliwa kwa maumivu yaliyotokana na matendo na maneno ya Serikali iliyoundwa nao. Nawataja wa uchache watu hao ambao kama CCM tunapaswa kukesha tukiomba wasiende kupiga kura.
Waliobomolewa nyumba na biashara zao bila kulipwa fidia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofukuzwa kazi kwa sakata la vyeti bila kupewa hata sumni pamoja na kufanya kazi kwa miongo kadhaa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliopatwa na majanga ya asili bila kupata msaada wa kiserikali pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofungiwa biashara na shughuli zao za kiuchumi kwa njia za kibabe pamoja na wategemezi wao.
Na wote ambao wameoisoma namba kwa namna moja au nyingine!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)
Sawa kabisa kwa hao wakienda kupiga kura. Ila hawa ni uhakika wataenda kupiga kura maana wao na familia zao imewatendea yaliyostahili, na wanahitaji Rais Magufuli aendelee kuwepo ili miradi mikubwa ikamilike:-
√ Wafanya biashara ambao mgao wa umeme ulikuwa unaathiri shughuli zao. Kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Mwl. Nyerere ni tegemeo lenye neema kwa uhakika wa umeme wenye bei nafuu;
√ Wafanya biashara wasafirishaji wa mizigo mbalimbali kwa njia ya barabara, maji, reli na anga. Miundombinu hiyi siyo tu inaboreshwa nchi nzima ila inaongezwa yenye uimara ubora wa yhakika;
√ Wakulima walioshindwa kuuza mazao yao kwa sababu ya uchakavu na/au kutukuwepo miundombinu;
√ Wakazi wa miji mikubwa, km DSM, ambao foleni za magari zimekuwa zukagaribubratiba za shughuli za kijamii na maendeleo;
√ Wafanya biashara ndogondogo (machinga na mama nitilie) waliokuwa wakisumbuliwa na mamlaka kupewa vitambulisho vyenye kulipiwa 60/= kwa siku. Sasa wanafanya biashara zao kwa amani kabisa na kiasi wanaotembeza wamepungua;
√ Wachimbaji madini wadogo wadogo kupewa nafasi za kufanya hivyo bika bufhuza na masoko ya uhakika la madini yao yalitojengwa kwenye maeneo yao;
√ Wakulima na wauza mazao ya shambani ambao walisumbuliwa na uwepo wa mageti barabarani, sasa rukhsa kusafirisha hayo mazao yasiyozidi Tani1, bila bughuza;
√ Wakina mama wajawazito waliosogezewa huduma karibu na makazi yao baada ya kujengewa au kuboreshewa zahanati, vituo vya afya na hispitali;
√ Wazazi wasio na uwezo wa kulipia ada sasa watoto wanaendelea na masomo;
√ Wasomi walio na sifa za kuajiriwa wakaziba pengo la wale waliondolewa kwa kutokuwa na sifa; nk
Idadi hii, yenye uhakika wa kupiga kura ni kubwa maradufu kulinganisha na hiyo uliyotaja, Mkuu
VUTA-NKUVUTE, na hata ukiongeza na hao wanaoshawishika hakuna Uhuru na Haki, ati kutakuwepo maendeleo ya watu.
VITUKO