USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amekabidhi pikipiki 25 kwa Maafisa ugani wa Kilimo Jijini Dar Es salaam, akihimiza kutumia pikipiki hizo katika kuleta tija kwenye sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanzania.
Leo Ijumaa Disemba 06, 2024 wakati akikabidhi Pikipiki hizo kwa maafisa ugani, @elihurumamabelya pia amemshukuru pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa anaoendelea kuufanya kwa wananchi na hasa kutoa kipaumbele kwenye sekta muhimu zenye kujumuisha wananchi wengi.
Kwa upande wao baadhi ya Maafisa ugani waliokabidhiwa pikipiki hizo, wakizungumza na wanahabari wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji huo, wakiahidi kuwafikia zaidi wakulima wa Jiji la Dar Es salaam wanaokadiriwa kuwa takribani 100,000 wakiwa ni wale wa kwenye vikundi pamoja na mkulima mmoja mmoja.