Hawa wakulima wa Dar ndio wanalima wapi, mjini hakuna shamba CCM tunafeli wapi?

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amekabidhi pikipiki 25 kwa Maafisa ugani wa Kilimo Jijini Dar Es salaam, akihimiza kutumia pikipiki hizo katika kuleta tija kwenye sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Leo Ijumaa Disemba 06, 2024 wakati akikabidhi Pikipiki hizo kwa maafisa ugani, @elihurumamabelya pia amemshukuru pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa anaoendelea kuufanya kwa wananchi na hasa kutoa kipaumbele kwenye sekta muhimu zenye kujumuisha wananchi wengi.

Kwa upande wao baadhi ya Maafisa ugani waliokabidhiwa pikipiki hizo, wakizungumza na wanahabari wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji huo, wakiahidi kuwafikia zaidi wakulima wa Jiji la Dar Es salaam wanaokadiriwa kuwa takribani 100,000 wakiwa ni wale wa kwenye vikundi pamoja na mkulima mmoja mmoja.

USSR

Screenshot_20241206-173304.jpg
 
View attachment 3170590
Wakulima wale wa kando ya barabara labda wanachezea kodi za wananchi bila sababu!
 
Hii habari niliiona jana kwenye taarifa ya habari nikacheka tu, kilimo hiki cha dar cha mabustani ya michicha na chinese wamepewa usafiri, huko ndani ndani kwa wazee wa ngwasuma wanaokesha shamba sijui kama zimefika kote sijui
 
Kwa upande wao baadhi ya Maafisa ugani waliokabidhiwa pikipiki hizo, wakizungumza na wanahabari wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji huo, wakiahidi kuwafikia zaidi wakulima wa Jiji la Dar Es salaam
Lengo kuu la hiyo hafla ni promotion ya hapo pekundu
 
Watakuwa wakulima wa maua ya mahekalu ya mbweni yale 😂
 
Back
Top Bottom