Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa kweli wanachokifanya hawa watatu si vichekesho peke yake bali ni kufru kwa dini yao na ni kuwafedhehesha wenzao.Wapo wengi ambao wamefanya kama hivyo lakini hawa wako juu katika orodha hiyo
Kwanza ni Saudi Arabia ambayo mwanzoni mwa vita iliitisha mkutano mkubwa sana wa mataifa ya kiarabu na yenye waislamu wengi.Kilichotokea ni kuundwa kwa tume ya mawiziri wa nje wa nchi chache kati yao kwenda kuishtaki Israel kwa China.Baada ya hapo Saudia imepiga kimya kabisa huku wananchi wa Palestina wakiuliwa bila utetezi.
Wa pili ni Jordan ambapo raisi wake alikwenda Marekani kwa raisi Biden akiwa mikono nyuma kama raisi Ruto wa Kenya akatoa malalamiko yake kwa kiongozi huyo.Hakuna hata moja kati ya aliyoyazungumza lililosikilizwa kwani hata vituo vya Jordan vya kutoa misaada ya matibabu kule Gaza navyo viliangamizwa na wao hakuna walichokifanya zaidi ya kuendelea kulalamika kuwa Israel imehusika.
Wa tatu ni Uturuki chini ya raisi wake kigeugeu,Erdogan.Nchi hiyo ni kati ya mataifa ya kiislamu yenye teknolojia kubwa za kijeshi na silaha bora sana lakini muda wote wa vita haijaweza kutoa msaada wowote wa maana zaidi ya kutoa majina mabaya kwa Netanyahu kama vile Hitler au fashisti ambayo wala hayakuizuia Israel kupiga mahospitali yanayofadhiliwa na Uturuki ndani ya Gaza.
Kwa ajili hiyo kwa sasa kinachosubiriwa ni kipigo cha aina yake kwa Israel na mataifa hayo ya kinafiki ya kiislamu kutoka kwa Allah baada ya wote kushindwa mtihani na kufanya kibri kilichopitiliza.